Udanganyifu unaofanywa kwenye michezo ya kubahatisha na kamari

Baada ya miaka kadhaa kutakuwa na hali ya umasikini mkubwa kwa vijana na watu wa rika la kati ambao ni wadau wakubwa wa hiyo michezo ya kamari kwa sura ya Betting. Sababu kubwa ni dhuluma na mzunguko wa pesa isiyo halali kutoka kwa wengi kwenda kwa wachache. Kuna dini zimekataza kabisa michezo ya kamari kwenye vitabu vyao vitakatifu kuilinda jamii na vitendo vya dhuluma. Kwa hivi sasa hapa nchini vitendo hivi vimeshamiri kiasi ambacho jumla ya kamari iliyokuwa ikichezwa kwa mwaka mzima katika miaka ya 90, hii leo inachezwa kwa siku moja tu na saa kadhaa. Kama ni janga kubwa kwa kizazi kilichopo na vijavyo. Pia, betting inapunguza vipaji vingi vya michezo kwa watoto wetu siku hizi ambao badala ya kutumia muda mwingi kwenye mazoezi wao hutumia katika betting. Aibu!
 
Huo ndo ukweli na mbaya zaidi ni 1 kati ya 1000 wanaojua kuhusu hili na hii ni sababu ya kukosa maarifa.
 
2854258fae13fb6416721432ca1e696e.jpg
 
Naunga mkono hoja.
Miaka ya nyuma niliwahi kuwa na ukaribu sana wa kibiashara na dada mmoja raia wa kigeni aliyekuwa mwandamizi kwenye kampuni mama ya kampuni kadhaa ndogo ndogo za casino, kamari, na michezo ya kubahatisha ndani na nje ya Bongo. Siku moja tulikuwa na ahadi ya kukutana ofisini kwake, nilipofika tu akaniomba nimsubiri maana alikuwa anamalizia kikao na wageni fulani hivi. Badala ya kumsubiri nikaamua kusogea upande wa casino 'kupoteza muda', kushangaa shangaa' na kujaribu kucheza kamari. Kilichotokea siku ile, sitakisahau, maana tangu siku ile kamari na michezo ya kubahatisha kwangu ni sumu ya kukaa nayo mbali kabisa. Huyu dada kwa upendo kabisa alinishauri nisiwe na mazoea kabisa ya kushiriki kwa namna yoyote ile katika kucheza kamari au michezo ya kubahatisha. Alinipa lecture kali kwamba 95% ya wacheza kamari na michezo ya kubahatisha, hupoteza fedha zao na kiwango kikubwa kuliko wanachopata wao. Namzungumzia afisa mwandamizi wa kampuni iliyokuwa ikitengeneza fedha/faida kutokana na kuliwa fedha kutoka kwa wateja washiriki walioliwa fedha zao kwenye kamari. Ni sawasawa na muuza sigara wa jumla akikataza mwanawe asivute, au mmiliki wa baa akimsihi mwanawe asipate kinywaji.

Njia bora ya kutengeza fedha ni kufanya kazi/shughuli halali, kwa bidii na maarifa na kujiwekea malengo, na sio kwa kucheza kamari.
 
kibaya zaidi ni pale aliyeshinda anayo hojiwa kabla ya kutangazwa mshindi...

kutokana na kuenea kwa janga hili la wasio na ajira imefikia hata ajira ni bahat nasibu kuipata..

sera ya biashara na mipango mingine ya ujasiria mali na kujiajiri imekuwa kama bahat nasibu kifanikiwa..

wadau wa maendeleo ni jukumu lao sasa kukaa na kitathmini kwa namna gani jamii itawekeza na kufaidika bila kuingiza ubahati nasibu..

mwisho, ulevi wa bahat nasibu ndo ulevi mbaya kuliko nyilevi zote na wenye hatar kubwa kuliko zote, unaweza kuwa na dhana kuwa ukitusua utaacha lakini ukitusua na ukabahatika kuwa na zile formula na elimu ya kutusua na wakakundua watakununua.. ili upunguze hasara kwenye kampuni.

fungua chuo cha kubet uone usipofungwa kwa fitina utauliwa au utanunuliwa.

jingine la mwisho ni kwamba kutoka na hawa watu kuwa na fedha nyingi wamefanikiwa ku control kila nyanja ya mawasiliano hivyo ukijidai unaingia google unaenda kujiua mwenye maana wao ndo wenye info.. kwa wa incredible , talent wenye formula huwezi kuwaona huko labda uwe mahiri kwenye data analysts na some technic ambazo ukizijua kwao wao ni hasara.
 
Niko mbali na hiyo michezo kiasi kwamba naona yote uliyosema hapo ni kitu kimoja tu- kamari. Sijui tofauti yake ni nini
Basi kuwa kwako mbali kusikufanye uongee bila utafiti hasa kwa vitu usivyo vijua maana unaoneka unapiga kitu ambacho hata wewe hukijui vizur.

Mimi mwenye shahid namba moja na nimeshinda milion 1 mara mbili na nimeshinda laki tano na ushehe mara 1 na leo nimetoka kuingiziwa elfu 37 baada ya kupata mechi 11 za jana na kuwa miongoni mwa watu 49 tulio fanikiwa huku wenzetu 8 walio win mechi zote 12 wakilamba milion 19 kila mtu katika kinyang'anyiro cha mil mia naa kupitia **********

Usiwe shahidi wa vitu usivyo vifanyia uhakiki , hayo labda ongelea huko kwenye BIKO na hao TATU MZUKA lakin sio sports beting hata kama ni kamali lakin unaliwa kihalali kutokana na utabiri wako wa mechi na una win kihalali kutokana na utabiri wako pia hakuna longo longo.
 
Mmeshinda 19 ila waliocheza nchi nzima walikua wangapi? Huoni kwamba idadi ya washindi ni negligible kama ukiweka idadi ya washiriki wote? Hatusemi Hakuna washindi, wenye bahati Kama wewe wapo na mnashinda ila waliolia ni wengi zaidi yenu.
 
Tatu mzuka ni kweli mi juz kati nilicheza 1000 nikalinganisha no zote 3
Nikashinda 200000 ila wakakata makodi yao wakantumia laki na themanini na chenchi
 
I'm grateful to John McCain Magufully for his lifetime of service to our country. Congratulations, John, on receiving this year's Liberty Medal."
 
Kamali unaanza kama mchezo lakini unageuka ugonjwa,nakumbuka miaka 1973 pale Mkwawa Iringa,mwalimu wa kizungu alicheza kamali na wakulima wa kizungu,aliweka gari mmoja ndogo akarudi na magari manne na pikipiki ya vespa.
Lakini hakuachia hapo aliendelea kucheza mwisho alibakia na vespa.
 
Basi kuwa kwako mbali kusikufanye uongee bila utafiti hasa kwa vitu usivyo vijua maana unaoneka unapiga kitu ambacho hata wewe hukijui vizur.

Mimi mwenye shahid namba moja na nimeshinda milion 1 mara mbili na nimeshinda laki tano na ushehe mara 1 na leo nimetoka kuingiziwa elfu 37 baada ya kupata mechi 11 za jana na kuwa miongoni mwa watu 49 tulio fanikiwa huku wenzetu 8 walio win mechi zote 12 wakilamba milion 19 kila mtu katika kinyang'anyiro cha mil mia naa kupitia **********

Usiwe shahidi wa vitu usivyo vifanyia uhakiki , hayo labda ongelea huko kwenye BIKO na hao TATU MZUKA lakin sio sports beting hata kama ni kamali lakin unaliwa kihalali kutokana na utabiri wako wa mechi na una win kihalali kutokana na utabiri wako pia hakuna longo longo.

Kushinda hata kwa kiwango cha mamilioni SIO TIJA, kamari ni ULEVI, wewe umeshinda vilaki kadhaa, je wengine? unajua athari kiasi imeshaleta. Ina athari za kisaikolojia za muda mrefu maishani mwako, haijalishi unashinda ama hushindi, haijalishi kama inahusisha michezo au ni kamari ya moja kwa moja, zote aina za kamari, mojawapo ya athari zake ni kukufanya uwe tegemezi wa kamari na kupunguza ufanisi na ubunifu wako katika shughuli za uzalishaji. Lakini pia inategemea na umri wako, kamari ni mbaya zaidi kwa vijana, inawajengea kitu kibaya sana akilini mwao, inaharibu akili zao, muda mwingi wanafika mahali wakidhani kwamba hawahitaji kuweka juhudi na ubunifu kuboresha maisha yao kwasababu watapata fedha kirahisi kwenye kamari. Ulevi wa kamari una athari hadi kwenye familia, kwamba fedha ambayo ingetumika kwenye matumuzi ya msingi ya ki familia inaishia kwenye kamari. Kamari inawafanya watu waamini kwamba wataweza kuyatatua mataizo yako ya kifedha kwa NJIA YA MKATO - KIRAHISI kwa kucheza kamari.
 
Ila mikeka kushinda ni we mwenyewe. Maana mechi zinachezwa zake huko ulaya na hawawez panga matokeo ya mechi zote....ndo maana mimi naamini mkeka wangu tu maana najua mshindi hatokan na mashine......ila Mzee baba nachezeaga za USO......
 
Miye nashangaa nimeenda kwa babu tumechunguria akanipa namba ya bahati nikacheza nikaa na matumauni mwisho wa Siku sijashinda hivi kwanini mshana jr hivi vitu kamari na nguvu ya giza havihusiani
 
Miye nashangaa nimeenda kwa babu tumechunguria akanipa namba ya bahati nikacheza nikaa na matumauni mwisho wa Siku sijashinda hivi kwanini mshana jr hivi vitu kamari na nguvu ya giza havihusiani
vinahusiana pakubwa sana tatizo ni kwamba mnatofautiana makafara kati ya mmiliki mchezo na wewe mchezahi..
Yeye kafara lake ni sawa na engine ya train, wakati kafara lako si sawa na engine ya passo.. Utachomoka kweli hapo?
 
Bahat nasibu za Biko,3 mzuka and Co pamoja na betting zote ni kamari.
Kamari ni kharam kwa waislam
 
Back
Top Bottom