Udaku wa wiki

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
14,524
17,154
Kuimarisha Demokrasia
Mheshimiwa Spika,
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tumeshuhudia kukua na kustawi kwa demokrasia nchini.
...yaani demokrasia ambayo inahakikisha kuwa CCM itabaki madarakani kwa namna yoyote hata kama wapiga kura hawataki?
Vyama vya siasa vimeongezeka kwa idadi na kuimarika katika kufanya kazi za siasa. Asasi za kidemokrasia kama vile Bunge na Mabaraza ya Madiwani zimeendelea kutimiza kwa ufanisi zaidi wajibu wao wa kuwa vyombo vya uwakilishi wa wananchi vya kutumainiwa. Hali kadhalika sauti ya asasi za kiraia imeendelea kusikika kutoa maoni juu ya masuala muhimu kwa taifa letu na watu wake. Vyombo vya habari navyo vimeendelea kufanya kazi zake kwa uhuru.

Mheshimiwa Spika;

Ni makusudio yangu na yetu Serikalini kuona kuwa demokrasia inazidi kustawi na raia wanapata fursa ya kutoa maoni kwa uhuru na uhuru wa vyombo vya habari unaheshimiwa. Tutaendelea kusaidia na kuliwezesha Bunge na Mabaraza ya Halmashauri kutimiza wajibu wao ipasavyo. Tumefanya hivyo miaka mitano iliyopita, naahidi kuwa tutajitahidi kufanya vizuri zaidi katika miaka mitano ijayo.

Utawala Bora
Mheshimiwa Spika;
Katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba, 2005, niliahidi kuwa Serikali nitakayoiunda itahakikisha kuwa demokrasia inastawi, itazingatia utawala bora, utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu. Pia niliahidi kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa na maovu katika jamii. Nafurahi kwamba katika miaka mitano iliyopita tumetimiza ahadi zetu kwa kiasi kikubwa. Natambua wajibu wa kuimarisha mafanikio tuliyoyapata na kuongeza juhudi pale ambapo hatuna budi kufanya vizuri zaidi. Natambua, pia, haja ya kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji Serikalini: katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali na, katika Halmashauri za Wilaya na Miji.

Tumejitahidi sana katika miaka mitano iliyopita kutoa mafunzo na kusisitiza nidhamu, uwajibikaji na ufanisi zaidi. Lakini bado hatujafika pale tunapopataka. Naahidi kuwa tutajipanga vizuri zaidi na kusukuma kwa nguvu zaidi nidhamu na uwajibikaji katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Naahidi pia kwamba tutaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa maana ya mishahara, marupurupu, malipo ya uzeeni na mazingira ya kazi.

Mapambano Dhidi ya Rushwa
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa mapambano dhidi ya rushwa katika miaka mitano iliyopita tumechukua hatua muafaka za kujenga uwezo wa kisheria, kimfumo na kitaasisi wa kupambana na rushwa nchini.
yaani una maana mradi wa CCM unaosimamiwa na Kosea ndiyo taasisi imara ya kupambada na rushwa?
Tumetunga sheria mpya kali zaidi na yenye upeo mpana zaidi wa kukabili tatizo hili. Pia tumetunga Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya kuzuia na kupambana na rushwa wakati wa uchaguzi. Tumeunda chombo kipya cha kuzuia na kupambana na rushwa, TAKUKURU, chenye mamlaka zaidi kisheria na chenye uwezo mkubwa zaidi wa rasilimali watu na vifaa wa kutekelezea majukumu yake.

Mheshimiwa Spika;

Ni ukweli ulio wazi kuwa katika kipindi hiki tuhuma nyingi zimeibuliwa, kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani. Watuhumiwa wengi zaidi wamepatikana na hatia na kuhukumiwa.
.... ni akina nani hao waliohukumiwa, yaani yule mzee wa BOT aliyekuzidi kete kwa demu fulani ambaye sasa ni mheshimiwa mbunge?
Rushwa kubwa zimeshughulikiwa na vigogo wamewajibishwa bila kuonewa muhali. Pamoja na hayo bado ipo haja ya kufanya zaidi kwani tatizo la rushwa bado ni kubwa.

Nimesikia, tumesikia na wamesikia kilio cha wananchi cha kutaka tufanye vizuri zaidi. Tutaongeza bidii katika mapambano haya. Naomba wananchi waendelee kutuunga mkono na kututia moyo na hasa TAKUKURU. Kauli za pongezi pale wanapofanya vizuri zinawaongezea ari vijana wetu ya kufanya vizuri zaidi. Lakini, tabia za kubeza hata pale walipofanya vizuri zinawavunja moyo, kuwakatisha tamaa na kushuhsa morali wao wa kazi. Tuwapongeze wanapofanya vizuri, tuwakosoe wanapokosea na lililo muhimu zaidi tuwape ushauri juu ya njia bora ya kupata ufanisi. Tukifanya hivyo tunajenga, kinyume chake tunabomoa.

Utawala wa Sheria
Mheshimiwa Spika;
Tutaendelea kuimarisha na kuboresha mfumo wetu wa utoaji haki nchini.......
Mliimarisha nini katika utoaji haki ambacho unataka kuendelea kuimarish?
Serikali itashirikiana na Mahakama kupanga na kutekeleza mipango ya kuongeza uwezo wa vyombo vya kutoa haki ili vitimize ipasavyo wajibu wao. Tutaendelea kuongeza bajeti ya Mahakama nchini. Tutakamilisha mchakato wa kuanzisha mfuko wa Mahakama ambao utaongeza uhuru na uwezo kwa masuala ya fedha na rasilimali. Tutaendelea kuongeza Majaji, Mahakimu na Mawakili wa Serikali. Aidha, tutahakikisha kuwa mchakato wa kuboresha mfumo wa utawala katika Mahakama nchini unakamilishwa.

Mheshimiwa Spika;

Katika miaka mitano hii tutalivalia njuga na kulipatia ufumbuzi muafaka tatizo kubwa la mlundikano wa wafungwa na mahabusu magerezani. Mapema iwezekanavyo nakusudia kukutana na wahusika katika Wizara ya Mambo ya Ndani na Idara ya Magereza kuelewana juu ya hatua za kuchukua .

Udaku wangu wa Wiki:

Kwani kanuni za bunge hazifanyi kazi kwa wengine? Ninajua kuwa ni kosa kwa mtu yeyote kusema uwongo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiyo maana Zitto alikuwa suspended kipindi fulani. Je inakuwaje wanamruhusu Kikwete kusema uwongo wote huo kwa muda mrefu vile bila kumchukulia hatua?

Huwezi kutenganisha ccm na uwongo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom