Udadisi na ukweli kutainusuru jamii na habari za uongo

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Katika kukabiliana na habari za uongo zinazosambazwa katika jamii, Watanzania wametakiwa kutumia taarifa zilizothibitishwa na vyanzo vya habari vinavyotambulika kisheria.

Kutokana na kukuwa kwa teknolojia ya mawasiliano, baadhi ya watu duniani wanatumia fursa hiyo kutengeneza habari za uongo (Fake News ) ambazo zina lengo la kupotosha au kuibua taharuki na kuathiri watu katika jamii.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika mdaharo ulioandaliwa na Idhaa ya Kiswahili ya Dutch Velle (DW), amesema habari za uongo ni zile ambazo hazijapitia mchakato wa kitaalamu na kuchujwa maudhui yake mpaka kumfikia mtumiaji ambaye ni mwananchi wa kawaida. Anaeleza kuwa habari hizo zisipodhibitiwa zinaweza kusababisha madhara kwa wananchi na kuvuruga utaratibu wa kuishi katika jamii.

“ Ili taarifa iwe habari inakuwa imepitia mchakato wa aina fulani, kuchujwa na kuhakikiwa lakini information ni taarifa za ujumla” amesema Dkt. Mwakyembe na kuongeza kuwa,

“Kutokana na kukua kwa utandawazi taarifa za uongo zimeongezeka. Tunahitaji kujenga misingi yetu ya kitaifa ili kuepuka athari za taarifa za uongo”

Licha ya taarifa za uongo kusambazwa na vyombo vya habari, mitandao ya kijamii kama njia rahisi na ya haraka ya kupata taarifa inatajwa kutumiwa kusambaza taarifa za uongo ambazo zinalenga kupotosha ukweli wa mambo kwa manufaa ya watu wachache kujipatia faida au umaarufu.

“Naomba niulize hivi mitandao ya kijamii ni vyombo vya habari? Jibu langu ni hapana hivyo ni vyombo vya taarifa. Taarifa za mitandao ya kijamii zikifikia vyombo vya habari na zikifanyiwa mchakato ndio zinakuwa habari” amesema Dkt. Mwakyembe.

Hivi karibuni Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) liliingia katika mtego wa kutangaza habari ya uongo iliyokuwa imewekwa kwenye mitandao ambapo ilikuwa inaeleza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri ya kupambana na rushwa.

Habari hiyo iliibua mjadala miongoni mwa watanzania kwasababu haikuwa na maudhui yenye kuashiria kwamba ilikuwa habari ya ukweli na ililenga kupotosha umma. Hata hivyo watangazaji wa TBC bila kujiridhisha na kuzingatia vigezo vya habari waliitangaza kwa wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba amesema wao kama shirika ni waathirika wa habari za uongo na ameitaka jamii kuwa makini kwa kufanya utafiti kabla ya kutumia taarifa au habari iliyotolewa na chanzo ambacho wanakitilia shaka.

“Habari za uongo ni dhana pana na mpya, ni taarifa ambazo zinaweza kuwa nzuri au mbaya kulingana na mtu aliyezisambaza. Sisi kama TBC ni waathirika wakubwa wa habari za uongo ndio maana tumeboresha misingi ya kusimamia taarifa’, ameeleza Dkt. Rioba.

Zaidi, soma hapa => Udadisi na ukweli kutainusuru jamii na habari za uongo | FikraPevu
 
Back
Top Bottom