Udadisi: Matamko ni ya CCM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Baada tu ya Zitto,Kitila na Mwigamba kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya CHADEMA,kumekuwa na msururu wa Matamko kutoka kwa wanaojipambanua kama 'Wanaolaani Maamuzi ya Kamati Kuu'. Matamko yametokea sehemu mbalimbali za nchi. Kwa udadisi wangu binafsi,naona kuwa Matamko yote kama si kuandaliwa na CCM basi yanawahusisha CCM moja kwa moja. Nina sababu za udadisi huu:

Kwanza, Matamko yote yametolewa na watu waliojichanganya sana. Wapo waliojipa vyeo visivyokuwepo mfano Chitanda wa Mtwara na yule wa Mwanza. Haraka CHADEMA inaingia na kuumbua. Kutokana na kujisingizia vyeo na hadhi chamani, si ngumu kuona hizi ni porojo na propaganda. Udadisi unanielekeza kuwa CCM yahusika.

Pili, Matamko yote:lile la Mtwara,Dar Es Salaam na Mwnza,yamejaa kashfa mpya,tuhuma mbichi na vitisho. Hayajajielekeza kwenye uamuzi hasa wa Kamati Kuu. Yametaka kuvuruga tu amani ya kwenye chama. Hizi ni njia zitumiwazo hasa na CCM dhidi ya CHADEMA. Kumbebasi, matamko haya ni ya CCM.

Tatu, mara baada ya kutolewa matamko hayo,wa kwanza kuweka mitandaoni ni wana-CCM. Baada ya kuweka hujaa kujadili kwa kusifu matamko na kukandia tu CHADEMA.Ni kukandia tu bila ya kujenga mantiki yoyote. Udadisi wangu unanieleza kuwa Matamko haya ni ya CCM!

Nne,Matamko hayo ya 'watu wa CHADEMA' yamepokelewa kwa bashasha sana na magazeti ya Serikali ya CCM na magazeti ya chama,yaani CCM.Yamepata kurasa za mbele haraka na kupambwa kiuandishi. Udadisi wangu unanilazimisha kuamini kuwa CCM wanahusika na Matamko haya.

Kwahiyo, CCM inahusika na Matamko haya.Udadisi wangu unasema kwa sauti kuu kuwa watoa Matamko waliandaliwa kwa ustadi mkubwa ingawa wameangukia pua. Watoa Matamko wameumbuka haraka hata kabla. Ni aibu iliyoje. CCM inahusika na Matamko haya.Ni udadisi tu waungwana!
 
Haya matamko yamesaidia kujua MTANDAO wa wasaliti upo je na ni akina nani....kwa sababu ya kuchanganyikiwa na kupanic wametoa matamko hovyo...na kurahisisha kazi ya kuwajua...siku 14 hizo.....hata zito kutapa tapa zake kwenye media kumesaidia kuonesha dhamira yake kwa uwazi kidogo.....lakini pia imeonesha wasaliti wengi ni vilaza watu wenye political arrogance....ambao wanaonekana hata kama walikua na mpango huo mpango walikua wakiufanya kwa pupa na jazba kubwa.......ni watu ambao wamepewa siku 14 tu hata hazijaisha wamesema kila kitu.....na ni watu ambao hawakuwa na agenda mpya sana zile tulizo zoea zilizo feli za UDINI, UKABILA ,UKANDA...kwa ujulma zito alifanya kazi na VILAZA
 
Baada tu ya Zitto,Kitila na Mwigamba kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya CHADEMA,kumekuwa na msururu wa Matamko kutoka kwa wanaojipambanua kama 'Wanaolaani Maamuzi ya Kamati Kuu'. Matamko yametokea sehemu mbalimbali za nchi. Kwa udadisi wangu binafsi,naona kuwa Matamko yote kama si kuandaliwa na CCM basi yanawahusisha CCM moja kwa moja. Nina sababu za udadisi huu:

Kwanza, Matamko yote yametolewa na watu waliojichanganya sana. Wapo waliojipa vyeo visivyokuwepo mfano Chitanda wa Mtwara na yule wa Mwanza. Haraka CHADEMA inaingia na kuumbua. Kutokana na kujisingizia vyeo na hadhi chamani, si ngumu kuona hizi ni porojo na propaganda. Udadisi unanielekeza kuwa CCM yahusika.

Pili, Matamko yote:lile la Mtwara,Dar Es Salaam na Mwnza,yamejaa kashfa mpya,tuhuma mbichi na vitisho. Hayajajielekeza kwenye uamuzi hasa wa Kamati Kuu. Yametaka kuvuruga tu amani ya kwenye chama. Hizi ni njia zitumiwazo hasa na CCM dhidi ya CHADEMA. Kumbebasi, matamko haya ni ya CCM.

Tatu, mara baada ya kutolewa matamko hayo,wa kwanza kuweka mitandaoni ni wana-CCM. Baada ya kuweka hujaa kujadili kwa kusifu matamko na kukandia tu CHADEMA.Ni kukandia tu bila ya kujenga mantiki yoyote. Udadisi wangu unanieleza kuwa Matamko haya ni ya CCM!

Nne,Matamko hayo ya 'watu wa CHADEMA' yamepokelewa kwa bashasha sana na magazeti ya Serikali ya CCM na magazeti ya chama,yaani CCM.Yamepata kurasa za mbele haraka na kupambwa kiuandishi. Udadisi wangu unanilazimisha kuamini kuwa CCM wanahusika na Matamko haya.

Kwahiyo, CCM inahusika na Matamko haya.Udadisi wangu unasema kwa sauti kuu kuwa watoa Matamko waliandaliwa kwa ustadi mkubwa ingawa wameangukia pua. Watoa Matamko wameumbuka haraka hata kabla. Ni aibu iliyoje. CCM inahusika na Matamko haya.Ni udadisi tu waungwana!

hujui kuandika mashairi
 
Hapa kinachotakiwa ni Chadema kumfukuza Zitto haraka sana kusudi CCM wampokee mtu wao kama wanamtaka. Na mimi nilishasema hapa kwa nini wanaomtetea Zitto sana sana ni wale wenye mlengo wa CCM.
 
Sasa pamepoa kidogo.Mbinu hiyo imeonekana kushindwa.Hongereni CHADEMA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom