UDA: Connetion ya Robert Kisena na msharika wake Ridhiwani Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDA: Connetion ya Robert Kisena na msharika wake Ridhiwani Kikwete!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, Jul 31, 2011.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  1. uhusiano wa kibiashara kati ya Ridhiwani Kikwete na Robert Kisena ..yamekuwa yakiongelewa kwa muda sasa....kuanzia kwenye ununuzi wa pamba [kisena akilaumiwa kuwapusha mzani wakulima]...hadi biashara ya kupeleka mafuta migodini...na uchakachuaji wa mafuta.....katika hali inayoendelea ni wazi kila mtu atajiuliza Robert Kisena ni nani hadi aweze kumilikishwa UDA ...Kwa kiasi cha shilingi milioni 250 tu.....

  Ukizingatia mali zinazohamishika na zisizohamishika...za mabilioni ya shilingi ..ikiwemo yard kubwa sana jirani na bandarini.........imeshangaza sana kuwa uda inauzwa asilimia 52% kwa bilioni 1.4 ,Robert anatoa 250 million na anapewa ..haki zote....tena bila kufuata taratibu za Public Procurement...nani hapa ameona tangazo la UDA kutafuta mbia ..na taratibu zimefuatwa???

  Tunapenda kuwa na wawekezaji wazawa lakini ..kitendo kinachodhaniwa kufanywa na mtoto wa rais kupenyeza rafiki zake kama kivuli cha kujimilikisha UDA hakikubaliki kabisa ...kwani kila mtu anajuwa uhusiano wa kibiashara kati ya Robert na Ridhiwani ...hii ilipelekea hadi kwa ushawishi wake Roberty akapitishwa kugombea Ubunge Maswa ..hata baada ya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Shibuda,na Joseph......hii ilipelekea CCM ...Kupoteza jimbo...serikali ya kishkaji
  !


  UDA yauzwa kwa bei chee, Ofisi zake Zavamiwa - Page 4


  MGOMBEA WA CCM AMPIGA OCD,RIDHIWANI AMDHAMINI......


  "Mgombea huyo (Kisena) ametiwa nguvuni kutokana na mzozo wake na OCD wa Maswa juzi kituoni hapo na kumpiga OCD," alisema Kamanda Siasi, ambaye mwishoni mwa wiki alikaririwa akisema kuwa suala la shambulizi hilo ni la OCD Ndunguru na si Jeshi la Polisi na kufafanua kuwa ofisa wake ndiye aliyetakiwa kuamua au kutoamua kumshtaki mgombea huyo kwa tuhuma hizo za kufanya jinai.

  Akizungumza kwa njia ya simu siku ya tukio, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliyeambatana na viongozi wa chama hicho walifikika polisi na kuuliza mahali alipo Shibuda, lakini kabla ya kujibiwa Kisena alimrukia OCD na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

  “Alinirukia na kunipiga,” alieleza OCD, lakini 'bosi' wake, ambaye ni Kamanda Siasi, akasema kuwa “Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji  THE driver of the Chama Cha Mapinduzi (CCM) parliamentary aspirant for Maswa West Constituency, Mr Steven Kuilasa (16), was attacked and killed on Friday by Chadema supporters. The deceased was the driver of Maswa aspirant Mr Robert Kisena.
  [h=1]Mwekezaji mpya UDA lawamani[/h][h=2]Meneja Uda aliyesimamishwa kazi amjibu Meya Masaburi[/h]
  Meneja wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), Victor Milanzi, aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhirifu , amekanusha kuhusika na ubadhilifu wa Sh.millioni 200 zilizopotea na badala yake amemtaka Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, alisema Masaburi anaficha ukweli kwa sababu anashirikiana na mmiliki wa Kampuni ya Simon Group Robert Kisena kumchafua ili malengo yao yatimie.“Meya Masaburi akishirikiana na wamiliki wa Simion Group ambao ni vigogo mbalimbali akiwemo Waziri wa muda mrefu wameapa kuichukua Uda kwa nguvu ili waigeuze Container Terminal ili kukidhi matakwa yao binafsi,” alisema Milanzi.Milanzi alisema Meya Masaburi aliitisha kikao Juni 10 mwaka huu na kubariki maamuzi ya bodi ya Uda kwa kufanya kikao na mmiliki wa kampuni ya Simon Group huku akijua kuwa bodi ilikosea kwa kuwa ilikuwa haikuwahusisha wanahisa wakubwa.Aidha, Milanzi alisema Meya katika kikao hicho alipitisha maamuzi hayo akijifanya yeye ni Mwenyekiti na Robert Kisena mmiliki wa Simion Group kuwa katibu na kufanya maamuzi batili bila ridhaa ya baraza la madiwani na wanahisa wakubwa.Hata hivyo, uchafu huo ulikamilika pale alipomkabidhi kampuni ya Uda siku hiyo hiyo Simion Kisena kwa vile alilipa milioni 285 sawa na asilimia 12.5 ya hisa zote za Uda na kumtangaza mbele ya wafanyakazi.Alidai kuwa mmiliki wa kampuni hiyo Juni 22, saa 2:00 ya usiku alivunja ofisi za umma za Meneja Mkuu wa Uda na kuiba nyaraka muhimu zikiwemo hati miliki ya majengo na kuitaka serikali isikae kimya wakiangalia mali za Uda zikiporwa kwani wao ndio mmiliki.Awali Meya alitangaza kuunda tume mbili kwa ajili ya kuchunguza fedha zilizopotea Uda na mkataba uliopo pia kuchunguza matatizo yanayopatikana katika kituo cha Ubungo na kwamba zitagharimu milioni tisa hadi watakapo maliza uchunguzi.Meya alisema Sh. milioni 200 zilikuwa zimepotea na hazikuonyesha matumizi yake yoyote na ameipa tume mwezi mmoja ili kuweza kujua ukweli wa jambo hilo.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  huyo huyo SIMION GROUP analalamikiwa na wananchi wa ruvuma kwa kupewa monopoly ya kusafirisha mahindi kwenda arusha na dar kwa mgongo wa hifadhi ya taifa ya chakula!
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Taifa la walalamikaji, legelege.......!
   
 4. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hii nchi ikitokea vita ndipo heshima itarudi maana nao wajinga ni wengi sana nawanalewa madaraka kila kukicha
   
 5. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ridhiwani si mbadhirifu ila watu wasiomtakia mema wamemjengea chuki bila sababu yoyote. Mtoa hoja hear and say is not an evidence. Unapo toa hoja tafadhali toa ushahidi mahiri ili usionekane una chuki binafsi.
   
 6. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Phillemon Tafuta article ya Mwanakijiji juu ya UDA humu JF uisome unganisheni nguvu na Wabunge wa CDM ili wapate taarifa na wafanyie kazi hili swala, kuna jambo la ajabu hapo. Hata sijui kwanini Watanzania tumekuwa wajinga kiasi hiki, tunataka mtu atutie vidole ndio tuamke!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mtoto wa RAIS anafanya anavyotaka ten yrs si miaka ningi historia itamhukumu vibaya sana. mungu ibariki Tanzania
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Ni lazima Igwana ujuwe kuwa watu hapa tuko serious .....hatuleti hoja za kufikirika...au hoja zinazoongelewa magengeni uswahilini....tunakupa hoja za yanayongelewa na kweli unaona yanatokea kwenye corridors of power..yaani kwenye idara na maofisi nyeti ya serikali....!!!masuali yanazuka..

  1] Imekuwaje UDA inauzwa bila hata tangazo kutolewa ...ili kama mbia apatikane kwa ushindani...

  2]Imekuwaje Robert apewe umiliki wa kampuni tena kwa nguvu hata baada ya kushindwa kulipa bei chee aliyouziwa ya 1.4 Billioni..hadi expiration ya muda wa ku deposit ukafika.[amelipia milioni 250 tu kati ya hizo hadi muda unaisha]...kitaaluma angetakiwa kurudishiwa pesa yake atangazwe kutafutwa mbia mwingine.

  3]Nini kilisukuma meya kwenda kuwaingiza ofisini kina robert kwa nguvu.....?

  4]Ridhwani ataweza vipi kukana usharika wake na Kisena leo....

  Hatujamuhukumu Ridhiwani kwa kujikwapulia UDA.[wala hatutamuhukumu yeyote iwe baba yake,mama yake wa kufikia ,shemeji yake au yeyote..ni kazi ya mahakama]...lakini its just a matter of time tutajuwa the un-touchable force behind Robert Kisena....na ijulikane wazi kuwa Rais anao watoto wengi tu ...kwaniini iwe mmoja tu anatuhumiwa kila mara..ingekuwa chuki basi na wengine pia wangechafuliwa..tusi divert attention kwa hoja za kutetea uovu...
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Wapo huku wamekusikia ...nina imani kubwa kuwa ndani ya wiki ijayo HOJA YA UDA itaibuka bungeni,,......maana huu unaoendelea sasa ni ukwapuaji.......wa mali chache zilizobakia.....
   
 10. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145


  hiyo red ni swali gumu huyo bwana yeye tu kila kona ndiye anakula tenda

  Lakini hii issue ya UDA kuna sababu kuifanya mfano kama vile EPA wabunge wa CHADEMA waingize ili suhala bungeni kama
  hatua za mwanzo kuleta mapambano hakuna sababu za kufumbia macho huu uozo,

  Mkuu Phillemon Mikael
  tunaomba hii kitu chama kikifanyie kazi kwa sasa CHADEMA ni mwongozo katika ukombozi wa taifa
   
 11. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  hilo ndilo suruhisho kwa tatizo lakini hawa washughulikiwe kwa nguvu ya umma
  kama wakigoma bungeni basi UMMA UTAHAMUA hii kufumbia macho waporaji tutakwisha watazoea kupora
  kila siku kanuni zinavunja kutajirisha watu
   
 12. MWAGONA

  MWAGONA Member

  #12
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi tusubiri mda utafika liziwani tutamuhukumu sisi watanzania kinga ya baba yake ndiyo inayo mlinda, najua mda si mrefu ita expire na uvumilivu utapo tushinda sisi wa tanzania ndipo tutapo amua kuichoma hata kwa moto hiyo kinga au kuiombea.
   
 13. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Dogo ajiangalie, kachafuka utadhani ana umri wa miaka sabini?
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Mbona Mama Mkapa hajafanywa kitu kuchukua maflat ya ilala na kuyaita Lamada Appartment au bado ana kinga ya Uraisi wa Mkapa? na mali nyingi walizojichukulia na mkapa!! Riz1 keshanusa Watanzania ni watu wa Kusahau mapema!
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Duh Usanii kama kawa from WhiteHouse,,,
   
 16. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  tutadili na moja moja lakini hayo majengo yalipigwa mnada kwa kufuata utaratibu kama kuna rafu
  hapo kati NBC wawajibishwe
   
 17. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya matatizo kila kukicha mbona hawa watu hawajirekebishi? Inauma sana na hili ni tatizo kuu kwa kweli inachosha masikioni mwa wanaoitakia mema nchi hii.
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Duduwasha,
  Ulitaka nani amchukulie Mama Mkapa hatua? Kikwete? Hawa wote mbona wanaelewana kwenye mashua ya ufisadi? Hatujasahau. Tunahitaji kuirudisha nchi kwenye utawala wa kisheria.
   
 19. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  "Ufisadi" ni wimbo wa sumu ambao Watanzania hatujaamua kwa dhati kuukomesha kwa sababu hakuna wa kumfunga paka kengele.
   
 20. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Ishatoka hiyo ikiludi ni pancha. Full kusahau na walioshirikishwa hawatokuwepo kutoa ushahidi na na wakitoa hakimu atawaachia ushahidi hautoshi
   
Loading...