Uchunguzi wangu mfupi wa kitaa Uzunguni-unapingana na dhana ya kuwa 'Wazungu pekee ndio watu waliojaliwa kuwa na uwezo mkubwa kiakili'

Heaven Seeker

JF-Expert Member
May 12, 2017
478
1,047
Nilipokuwa mdogo niliamini dhana ya kwamba..

i) Wazungu wote ni watu wenye waliojaliwa kuwa na uwezo mkubwa kiakili kuliko akina sisi wa kwa Mtogole na Buza kwa Mama Kibonge..

Kabla sijatembelea nchi za Ulaya niliamini dhana hii. Lakini baada ya kufika Ulaya na kusoma nao darasa moja nimegundua dhana hiyo si ya kweli. Kwanza, kama ilivyo Bongo kwa mfano, kwamba tuna watu wenye akili za kawaida na wale wenye vipaji maalumu.

Ndio maana hapo mwanzo kukawa na shule kama Tabora boys, Kibaha, Mzumbe n.k kwa ajili ya vijana wenye vipaji maalumu, ndivyo ilivyo hata kwa Wazungu. Hata kwa Wazungu kuna vijana wenye vipaji maalumu na wenye akili za kawaida kama akina sisi tuliotokea huko kwenye shule za kucheza mpira vumbini.

Kinachotutofautisha kati yetu na wao ni kuwa, mazingira yao yanafanya watoto wenye akili za kawaida waweze kuwa active zaidi. Hii inachangiwa zaidi na aina ya malezi na mazingira yao. Kingine ni kuwa mfumo wao wa elimu wameufanya mwanafunzi aelewe na kufikiri zaidi kuliko kukariri vitu. Tukibadilisha mfumo wetu nasisi ukajikita kumfanya mwanafunzi kufikiri zaidi na kuelewa kuliko kukariri nakuhakikishia wabongo akina sisi wa kwa Mtogole tutakuwa na uwezo mkubwa tena sana tu.

Mfano mzuri ni kumlinganisha mtoto wa mjini na yule wa kijijini. Obviously, mtoto wa mjini unakuta akili yake imechangamka zaidi kuliko yule wa kijijini kutokana na utofauti wa mazingira. Hiki ndicho kinachowabeba Wazungu. Unakuta mtoto akiwa tangu mdogo mwenye umri wa miaka 3 anazoezeshwa vitu vya kumfanya akili yake iwe active mapema zaidi. Mfano ni mtoto wa miaka 4 kuendesha baiskeli kwenye barabara kuu wanakopita watu wengine wakubwa. Mfano mwingine niliona mtoto mdogo mwenye umri wa miaka kama minne anajua code za kufungulia mlango nyumbani kwao.

Kwahiyo unakuta akili yake inachangamshwa akiwa bado mdogo kabisa. Kwahiyo malezi yanakuwa yamechangia. Ambapo sisi watoto wetu wakiwa wadogo kila saa wanafungiwa ndani na kuambiwa acha acha kwa kila kitu. Hapo akili lazima ifubae tu. Labda awe miongoni mwa wale wenye vipaji maalumu ambapo ni hali ya kurithi ama asili.

Hoja yangu kwa kuhitimisha ni kuwa, ni kweli kuna watu waliozaliwa na uwezo mkubwa kiakili ikiwa ni akili za asili, na kuna watu waliozaliwa na akili za kawaida.

Hii ni hali ya kawaida kwa watu wote Duniani isipokuwa mazingira na malezi huchangia zaidi kuifanya akili ya mtu kuwa active ama kubakia imelala. Kwahiyo hata sisi Wabongo tunaweza kuwa na uwezo mkubwa kama ilivyo Wazungu na siyo kwamba Wazungu pekee ndio watu waliojaliwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi.

Hivyo wewe mzazi wa Buza kwa mama Kibonge, Sumbawanga, Ileje, Namanyere, Nyamiriro, Itabagumba, Liwale, Ngorongoro, n.k usikate tamaa ukadhani mwanao hawezi kuwa na uwezo mkubwa kiakili. Muhimu zingatia lishe, malezi na kumtengenezea mazingira ya kuifanya akili ya mwanao kuwa active akiwa bado mdogo.

Kwa kumalizia kabisa, hata Wazungu kuna baadhi yao uwezo wao kiakili ni wa kawaida tu.
 
Waafrica wapo wengi magenius ,sema waafrica tumejaaliwa roho ya ubinafsi na tamaa ndio hatusongi mbele...
Nakubaliana na wewe mkuu. Sema kitu kingine tunachotakiwa kukifanya ama kukipa kipaumbele upande wetu ni kuhusu mindset transformation.

Watu wajengewe uwezo wa kujiamini, kuwajali watu wengine, kuwa na mawazo chanya na ku-apply soft skills nyingine kama team player, kutoku-entartain masuala ya gossiping, kujali muda, effective communication n.k. Tukifanikiwa hayo tutapiga hatua kubwa sana.
 
Tatizo la ngozi nyeusi ni ubinafsi uliopitiliza, ukionyesha uwezo watu wanatafuta namana ya kukukwamisha au kukuroga. Kwa wazungu hao wenye uwezo wanakuwa appreciated na kupewa fursa zaidi za kuonyesha uwezo wao.....
 
The fact is white people are more intelligent that black people, there is huge gape between us and them by the way we can't be in same level intelligently.
 
Mkuu inabidi ku fact-check hii argument yako. Kwamba wazungu genetically wapo more intelligent kuliko other races?

Ukiachana na wale ambao ni genius naturally, nadhani watu wengine tupo sawa bila kujalisha rangi zetu, ila kinachotutofautisha ni mazingira, lishe na malezi ya namna tunavyozaliwa mpaka kukua.

Mie nimesoma na Wazungu darasani wenye uwezo wa kawaida tu. Tena darasani unakuta sometimes unafaulu kuliko hata baadhi yao.

Na hapo mie nimetokea vumbini schools na siyo kwamba nipo kwenye class ya 'Genius people'.

What if na mie ningetokea mazingira wezeshi yenye kunifanya niwe the best tangia utotoni?
 
Nilipokuwa mdogo niliamini dhana ya kwamba..

i) Wazungu wote ni watu wenye waliojaliwa kuwa na uwezo mkubwa kiakili kuliko akina sisi wa kwa Mtogole na Buza kwa Mama Kibonge..

Kabla sijatembelea nchi za Ulaya niliamini dhana hii. Lakini baada ya kufika Ulaya na kusoma nao darasa moja nimegundua dhana hiyo si ya kweli. Kwanza, kama ilivyo Bongo kwa mfano, kwamba tuna watu wenye akili za kawaida na wale wenye vipaji maalumu.

Ndio maana hapo mwanzo kukawa na shule kama Tabora boys, Kibaha, Mzumbe n.k kwa ajili ya vijana wenye vipaji maalumu, ndivyo ilivyo hata kwa Wazungu. Hata kwa Wazungu kuna vijana wenye vipaji maalumu na wenye akili za kawaida kama akina sisi tuliotokea huko kwenye shule za kucheza mpira vumbini.

Kinachotutofautisha kati yetu na wao ni kuwa, mazingira yao yanafanya watoto wenye akili za kawaida waweze kuwa active zaidi. Hii inachangiwa zaidi na aina ya malezi na mazingira yao. Kingine ni kuwa mfumo wao wa elimu wameufanya mwanafunzi aelewe na kufikiri zaidi kuliko kukariri vitu. Tukibadilisha mfumo wetu nasisi ukajikita kumfanya mwanafunzi kufikiri zaidi na kuelewa kuliko kukariri nakuhakikishia wabongo akina sisi wa kwa Mtogole tutakuwa na uwezo mkubwa tena sana tu.

Mfano mzuri ni kumlinganisha mtoto wa mjini na yule wa kijijini. Obviously, mtoto wa mjini unakuta akili yake imechangamka zaidi kuliko yule wa kijijini kutokana na utofauti wa mazingira. Hiki ndicho kinachowabeba Wazungu. Unakuta mtoto akiwa tangu mdogo mwenye umri wa miaka 3 anazoezeshwa vitu vya kumfanya akili yake iwe active mapema zaidi. Mfano ni mtoto wa miaka 4 kuendesha baiskeli kwenye barabara kuu wanakopita watu wengine wakubwa. Mfano mwingine niliona mtoto mdogo mwenye umri wa miaka kama minne anajua code za kufungulia mlango nyumbani kwao.

Kwahiyo unakuta akili yake inachangamshwa akiwa bado mdogo kabisa. Kwahiyo malezi yanakuwa yamechangia. Ambapo sisi watoto wetu wakiwa wadogo kila saa wanafungiwa ndani na kuambiwa acha acha kwa kila kitu. Hapo akili lazima ifubae tu. Labda awe miongoni mwa wale wenye vipaji maalumu ambapo ni hali ya kurithi ama asili.

Hoja yangu kwa kuhitimisha ni kuwa, ni kweli kuna watu waliozaliwa na uwezo mkubwa kiakili ikiwa ni akili za asili, na kuna watu waliozaliwa na akili za kawaida.

Hii ni hali ya kawaida kwa watu wote Duniani isipokuwa mazingira na malezi huchangia zaidi kuifanya akili ya mtu kuwa active ama kubakia imelala. Kwahiyo hata sisi Wabongo tunaweza kuwa na uwezo mkubwa kama ilivyo Wazungu na siyo kwamba Wazungu pekee ndio watu waliojaliwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi.

Hivyo wewe mzazi wa Buza kwa mama Kibonge, Sumbawanga, Ileje, Namanyere, Nyamiriro, Itabagumba, Liwale, Ngorongoro, n.k usikate tamaa ukadhani mwanao hawezi kuwa na uwezo mkubwa kiakili. Muhimu zingatia lishe, malezi na kumtengenezea mazingira ya kuifanya akili ya mwanao kuwa active akiwa bado mdogo.

Kwa kumalizia kabisa, hata Wazungu kuna baadhi yao uwezo wao kiakili ni wa kawaida tu.
Huna jipya, Darwin aliliona hili miaka 300 iliyopita
 
Back
Top Bottom