Uchunguzi wa uzoefu; Wanaume huwa serious zaidi -25, Wanawake +30

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
2,344
4,167
Katika makuzi yangu naweza kusema wanaume wanapokuwa katika rika dogo hutilia maanani sana mahusiano yao na huweka malengo ya muda mrefu na wenzi wao kwa kuwa fikra ya mwanaume ndiyo huanza kuchanua na kujiona ni mtu anayeweza kutimiza majukumu yoyote yatakayomkabili. Na jambo la kufahamu mienendo ya mwanaume katika rika hilo huchagizwa sana na ukaribu wa mwanamke ampendaye kwake, kama mwanamke aliye naye atampa chachu na pia maendeleo ya mwanaume huonekana ila ikiwa kinyume chake mwanaume hukata tamaa na haamini kama kuna mbadala wa mwanamke aliyekuwa naye utatokea. Hapa sasa akili ya mwanaume ikishavurugwa ule utayari na uthubutu wote hupungua na maisha atakayoishi ni ya mazoea

Mtoto wa kike ni kama bamia, linapokuwa teke thamani yake huwa kubwa kuliko maelezo na hapa ndipo wasichana wengine wanapokosa utimamu binafsi wa akili kwa kudhani nyakati wanazozishuhudia kipindi hicho hudumu. Kuna kipindi msichana anaweza shuhudia hadi wanaume watatu wanaoweza kumwaga machozi mbele yake kwa ajili yake lakini yeye anaamini thamani yake ni ya milele jambo linalopelekea kutoangalia ya mbele, kadri muda unavyokwenda ndio bamia hupoteza ubora wake na kila mlaji hupoteza uhitaji nalo, ndivyo kwa wadada wanapokuwa rika kubwa huanza kuwa serious kwa kurejea kumbukumbu za nyakati za nyuma.

Migongano iko hapa, kipindi mtoto wa kiume anapokuwa serious mtoto wa kike hajali na haelewi (Under 25) ila kipindi ambacho mwanamke anapokuwa serious mwanaume alishakata tamaa na wengi huwa wachafuzi (Over 30) na hapa ndo wadada hupata tabu sana na zile kauli za "Wanaume wote mbwa tu" huwa nyingi sana
 
Hili lina ukweli kwasababu... kuna maamuzi wanayoyafanya hawa ndugu zetu baada ya muda wanapokuja kutambua ule uhalisia wenyewe wengi huishia kwenye mikono isiyo salama...

Wengi wao huamini ubora walio nao sasa utadumu siku zote....
 
Yaani nadhani shida sijui ipo wapi labda asili maana vizazi na vizazi hurithishana tabia moja
 
Kilicho semwa hapa nahisi kimenilenga aisee.. Maana nilijitahidi kutafuta mwanamke nitakae inuka nae nimeambulia kibuti Jana.. Kamchagua MTU alie mjua kwa wiki 3 kaniacha Mimi wa miaka minne.. Nikifikiria nilivyo jitoa kwake nakata tamaa kabisa kuwekeza kwa mwanamke
Katika makuzi yangu naweza kusema wanaume wanapokuwa katika rika dogo hutilia maanani sana mahusiano yao na huweka malengo ya muda mrefu na wenzi wao kwa kuwa fikra ya mwanaume ndiyo huanza kuchanua na kujiona ni mtu anayeweza kutimiza majukumu yoyote yatakayomkabili. Na jambo la kufahamu mienendo ya mwanaume katika rika hilo huchagizwa sana na ukaribu wa mwanamke ampendaye kwake, kama mwanamke aliye naye atampa chachu na pia maendeleo ya mwanaume huonekana ila ikiwa kinyume chake mwanaume hukata tamaa na haamini kama kuna mbadala wa mwanamke aliyekuwa naye utatokea. Hapa sasa akili ya mwanaume ikishavurugwa ule utayari na uthubutu wote hupungua na maisha atakayoishi ni ya mazoea

Mtoto wa kike ni kama bamia, linapokuwa teke thamani yake huwa kubwa kuliko maelezo na hapa ndipo wasichana wengine wanapokosa utimamu binafsi wa akili kwa kudhani nyakati wanazozishuhudia kipindi hicho hudumu. Kuna kipindi msichana anaweza shuhudia hadi wanaume watatu wanaoweza kumwaga machozi mbele yake kwa ajili yake lakini yeye anaamini thamani yake ni ya milele jambo linalopelekea kutoangalia ya mbele, kadri muda unavyokwenda ndio bamia hupoteza ubora wake na kila mlaji hupoteza uhitaji nalo, ndivyo kwa wadada wanapokuwa rika kubwa huanza kuwa serious kwa kurejea kumbukumbu za nyakati za nyuma.

Migongano iko hapa, kipindi mtoto wa kiume anapokuwa serious mtoto wa kike hajali na haelewi (Under 25) ila kipindi ambacho mwanamke anapokuwa serious mwanaume alishakata tamaa na wengi huwa wachafuzi (Over 30) na hapa ndo wadada hupata tabu sana na zile kauli za "Wanaume wote mbwa tu" huwa nyingi sana
 
Kilicho semwa hapa nahisi kimenilenga aisee.. Maana nilijitahidi kutafuta mwanamke nitakae inuka nae nimeambulia kibuti Jana.. Kamchagua MTU alie mjua kwa wiki 3 kaniacha Mimi wa miaka minne.. Nikifikiria nilivyo jitoa kwake nakata tamaa kabisa kuwekeza kwa mwanamke
Yaani hadi jambo linasemwa ujue ni sehemu ya maisha yetu ndugu

Pole sana, na usifikiri kwamba maisha ndi yamefika mwisho cha kufanya acha wakati ukuamulie furaha na hatma yako, haitoshangaza sana huyo binti kuja kukutafuta tena hapo baadae ila hupaswi tena kuwa na kumbukumbu yoyote inayimhusu.
Wewe ni wa thamani sana na wa juu kuna wanawake wengi sana wanatamani walau sekunde wakusemeshe sasa yanini kudhani mtu mmoja anaweza kukuharibia maisha?

Vaa vizuri, pendeza haswaa, kama ni mpenzi wa mpira fuatilia sana, sikiliza muziki tafuta kampani na tabasamu muda wote kila kitu kitakuwa ni cha kawaida kwenye maisha
 
Shukran sana.. Maana for the first time nilijikuta naenda kunywa bia mpaka kulewa ninajitahidi kuji keep busy kama unavyo sema imenisaidia sana
 
Nlishawah mkimbiza mwanamke takriban miaka miwili hivi enz za A-level akanikataa, juz kati nimeenda mbeya nimeambiwa kaolewa na jamaa ni dereva na stail alompata alimpata club kwenye mapombe mwanamke alivyoona hapati wa kumwoa akaamua awe anashinda city pub( kwa wanaojua mbeya) kapata jamaa anasura ngumu alafu najua hampend alikuwa anataka atimize ndoto yakuolewa sikuiz akiniona anaona aibu sasa sijui kwanini...daaah maisha haya
 
Kilicho semwa hapa nahisi kimenilenga aisee.. Maana nilijitahidi kutafuta mwanamke nitakae inuka nae nimeambulia kibuti Jana.. Kamchagua MTU alie mjua kwa wiki 3 kaniacha Mimi wa miaka minne.. Nikifikiria nilivyo jitoa kwake nakata tamaa kabisa kuwekeza kwa mwanamke
Pole bro,i feel you..
 
Hili lina ukweli na wengi wao huishia mahali pabaya sana maana hujuta maisha yao yote ,kawa liza wengi wenye malengo na yeye af ana kuja kukubali kwa aliye mtamani na kuamini huyo ndo yule alie kuwa aki muota ndugu yangu hapo ndipo wanapo feli, akiangalia life ya wawili walee alio wakataa walio kuwa na nia thabiti ya kumweka ndani wana ishi kwa raha sana huwa wana umia na hujuta sana!
 
Kosa lako lilianzia hapo, usirudie tena hili Mkuu wale inabidi uishi nao tu kama masela ila ukijikuta umeingia mazima lazima yakukute hayo.

Next time: Kadri unavokuwa karibu na mwanamke ndio kadri yeye anavokuwa mbali na wewe
Thank me later
Shukran kwa ushauri mkuu
 
Daaah mkuu, umenena kabisaaa mana hata mimi yamenikuta juzi kati hapa daah....ila four to three years to come nijenge uchumi niwe jemedali haswaa...mana hawa viumbe wakati mwingine ndio wanatufanya tuonekane tuna roho mbaya, kipindi unataka ujenge maisha na mtu flani inashindikana kwakuwa yeye hujiona wa thaman zaid
 
Shukran sana.. Maana for the first time nilijikuta naenda kunywa bia mpaka kulewa ninajitahidi kuji keep busy kama unavyo sema imenisaidia sana
naam hata bia husaidia ila usitilie maanani cha muhimu ni kujikinaisha na nyakati nzuri zote mlizotumia pamoja
 
Back
Top Bottom