Uchunguzi wa Kitabibu Unaofanywa na Askofu Gamanywa

Nkamu

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
223
84
Salamu Wakuu!

Naomba kujuzwa kuhusu huu uchunguzi wa kitabibu unaofanywa na vituo hivyi vya tiba mbadala (SNS)vinavyosimamiwa na Askofu Gamanywa, je ni salama kwa afya za watumiaji? Na vinatumia teknologia gani kufanya huu uchunguzi pasipo kutoa sampuli za damu wala mkojo?

Naomba kujua tafadhali!
 
Jf hakuna madaktari? Mbona kimya? Au ndio mnatafakari kauli ya JK kwamba ataashughulikia waliosababisha waziri kuwajibishwa?
 
Mimi si Daktari but hii tiba mbadala ni salama ukitaka kuelewa zaidi sikia vipindi vyake kwenye radio ya Wapo radio ambapo unaweza kumpigia simu na hata kuongea na watu waliotumia au tibiwa wakapata nafuu.
 
hawa madakitari wa tiba mbadala kipimo wanachokitumia kama massage lakini kulinga na elimu walizo nazo hubaini kuwa unatatizo gani sehemu fulani maana huwa wana ngusa sehemu mbalimbali hasa za miguu na mikono na hiubaini kuwa kunatatizo gani na sehemu ipi. Ninaimani ni salama maana mke wangu nilimpeleka kwa Dr. mmoja pale Moro alitumia njia hii na ni rahisi haina complication nyingi na ni muda mfupi unakuwa umeshapata result.
 
na mkipata end stage diseases ndo mnakuja hospitali. Hivi watu mko kwenye globalized word mbona huko wanakotengeneza hivyo vifaa madaktari wanadili na wanatafutwa sana? Uchani kudanganywa na ujinga wa psychological relief jamani! Kungekuwa na hizo tech kusingekuwa na advancement mpaka kufikia laparascopic surgeries au ct,mri zisingekuwa zinatengenezwa. Nyie endeleeni kuamini miujiza isiyokuwepo, mkishachoka njooni hospital mpate palliative care.
 
hakuna lolote ni wizi mtupu,mi kuna jamaa yangu alikwenda,pale wapo radio kurasini,ndio makao makuu yao,wakampima eti kwa ku2mia computer,wakamtoa sumu mwilini,wakampa dawa za kama laki 2,hakupata hata nafuu yoyote,aliporudi kuwauliza kulikoni wakamjibu mponyaji ni Mungu,wao ni wawezeshaji 2!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom