Wana JF, itakumbukwa ya kuwa miezi kadhaa nyuma baada ya Mengi kuwatuhumu maofisa wa Polisi kutaka kumbambikizia mtoto wake madawa ya kulevya na kuwataja kwa majina na kiasi cha mgawo kilichopita kama advance, IGP aliahidi kuanzisha uchunguzi na kutoa majibu mapema iwezekanavyo. Inawezekana mimi majibu haya yalinipita maana mpaka leo sijui kinachoendelea. Je kuna mtu anaweza kunujuza mwisho ulikuwaje? Je RM alionekana muongo au uchunguzi bado unaendelea?