Uchunguzi mpya wa TAKUKURU kwa vyama vya siasa kuhusu fedha za jimbo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Wakati Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) ikiendelea kuichunguza Chadema kutokana na malalamiko ya waliokuwa wabunge wake kuhusu matumizi mabaya ya michango yao, imesema itafuatilia mifuko ya majimbo kwa vyama vilivyokuwa na wabunge katika Bunge la 11.

Tangu Juni, Takukuru imekuwa ikiwahoji wabunge wa CHADEMA baada ya kupata malalamiko ya matumizi mabada ya michango wanayotoa.

Hata hivyo, viongozi wa Chadema akiwamo katibu mkuu, John Mnyika wamesema hatua hiyo inalenga kukidhoofisha chama hicho kwani michango ipo kwa mujibu wa katiba.

Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema uchunguzi wao utafika hadi kwenye mfuko ya jimbo.

“Kimsingi kilichofanya tuanze na Chadema ni malalamiko ya fedha ambazo wabunge walichanga,” alisema Mbungo alipoulizwa kama kuna uchunguzi kwa vyama vingine.

“Tunafanya kwa vyama vyote, hakuna anayebaki salama au anaachwa kuchunguzwa pale ambapo kuna matumizi mabaya ya fedha, iwe ya majimbo au michango, vyama vyote vinachunguzwa,” alisema.

Alipoulizwa sababu ya kuchelewa kwa uchunguzi wa Chadema, Mbungo alisema kunatokana na kutanua uchunguzi.

“Ingawa muda umekwenda, bado uchunguzi huo unaendelea. Uchunguzi hauna mipaka wala mwanzo. Hilo suala bado lipo linaendelea kuchunguzwa na likikamilika kwa kweli mtajua tu,” alisema.

Aliendelea kusema kuwa uchunguzi huo ulihusisha idadi kubwa ya wabunge na sasa utahusisha mifuko ya majimbo.

“Kwa sababu linahusu mambo mengi, kwa mfano michango ya wabunge na matumizi yake. Kuwachunguza zaidi ya wabunge 70 siyo kitu chepesi. Nikuhakikishie, uchunguzi bado haujafungwa, mtapata matokeo,” alisema.

Katika Bunge lililopita, Chadema ilikuwa na wabunge 70 wakiwamo 34 wa kuchaguliwa na 36 wa viti maalum. Hata hivyo, wabunge 16 wa chama hicho walihamia CCM kuunga mkono juhudui za Serikali huku baadhi wakilalamika kukatwa mishahara kuchangia chama.

Juhudi za kuupata uongozi wa Chadema kuzungumzia uchunguzi huo haukufanikiwa, kwani simu za baadhi ya viongozi ziliita bila kupokelewa na hawakujibu ujumbe wa maandishi.

Akizungumzia uchunguzi huo, naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya alisema hawajapata taarifa ila wapo tayari.

“Hatujapata taarifa yoyote ya kuchunguzwa, lakini ni sahihi tu kwa sababu fedha za mfuko wa jimbo ni za walipakodi. Huwa zinakaguliwa na CAG (Mkaguzi wa Hesabu wa Serikali), sijajua kwa nini Takukuru wanataka kuzichunguza,” alisema Sakaya.

Sakaya aliyekuwa mbunge wa Kaliuwa alisema uchunguzi huo haupaswi kuingilia uhuru wa vyama.

“Kama wanakagua mfuko wa jimbo ni sawa lakini sioni kama ni sahihi kukagua michango ya wanachama kwa sababu kila chama kina uhuru wa kuchangisha na wabunge ndiyo wanasaidia,” alisema.

Katika Bunge lililopita CUF ilikuwa na wabunge 32 wa kuchaguliwa na 10 wa viti maalum lakini watatu kati yao walihamia CCM.

Naye katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alisema hawajapata taarifa ya kuchunguzwa na Takukuru.

“Hatujapata taarifa ya kuchunguzwa na Takukuru ila masuala yanayohusu uwajibikaji sisi tuko tayari kutoa ushirikiano. Tumekuwa tukitoa ushirikiano kwa Takukuru mara nyingi tu na hata sasa tuko tayari kushirikiana nao,” alisema Shaibu.

ACT Wazalendo ilikuwa na mbunge mmoja tu ambaye ni kiongozi wa chama hicho, Zitto kabwe katika Jimbo la Kigoma Mjini ambalo sasa limechukuliwa na CCM.
 
Tangu Juni, Takukuru imekuwa ikiwahoji wabunge wa Chadema baada ya kupata malalamiko ya matumizi mabada ya michango wanayotoa.

Hivyo uchunguzi huko ACT - "Wazalendo", inaweza kuwa kazi ya saa chache tu au siyo!?
 
Hakuna uchaguzi ambao ccm imetumia fedha nyingi kama mwaka huu, takururu fanyeni uchunguzi hizo fedha wamezipata wapi?
 
Wakati Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) ikiendelea kuichunguza Chadema kutokana na malalamiko ya waliokuwa wabunge wake kuhusu matumizi mabaya ya michango yao, imesema itafuatilia mifuko ya majimbo kwa vyama vilivyokuwa na wabunge katika Bunge la 11.

Tangu Juni, Takukuru imekuwa ikiwahoji wabunge wa CHADEMA baada ya kupata malalamiko ya matumizi mabada ya michango wanayotoa.

Hata hivyo, viongozi wa Chadema akiwamo katibu mkuu, John Mnyika wamesema hatua hiyo inalenga kukidhoofisha chama hicho kwani michango ipo kwa mujibu wa katiba.

Mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema uchunguzi wao utafika hadi kwenye mfuko ya jimbo.

“Kimsingi kilichofanya tuanze na Chadema ni malalamiko ya fedha ambazo wabunge walichanga,” alisema Mbungo alipoulizwa kama kuna uchunguzi kwa vyama vingine.

“Tunafanya kwa vyama vyote, hakuna anayebaki salama au anaachwa kuchunguzwa pale ambapo kuna matumizi mabaya ya fedha, iwe ya majimbo au michango, vyama vyote vinachunguzwa,” alisema.

Alipoulizwa sababu ya kuchelewa kwa uchunguzi wa Chadema, Mbungo alisema kunatokana na kutanua uchunguzi.

“Ingawa muda umekwenda, bado uchunguzi huo unaendelea. Uchunguzi hauna mipaka wala mwanzo. Hilo suala bado lipo linaendelea kuchunguzwa na likikamilika kwa kweli mtajua tu,” alisema.

Aliendelea kusema kuwa uchunguzi huo ulihusisha idadi kubwa ya wabunge na sasa utahusisha mifuko ya majimbo.

“Kwa sababu linahusu mambo mengi, kwa mfano michango ya wabunge na matumizi yake. Kuwachunguza zaidi ya wabunge 70 siyo kitu chepesi. Nikuhakikishie, uchunguzi bado haujafungwa, mtapata matokeo,” alisema.

Katika Bunge lililopita, Chadema ilikuwa na wabunge 70 wakiwamo 34 wa kuchaguliwa na 36 wa viti maalum. Hata hivyo, wabunge 16 wa chama hicho walihamia CCM kuunga mkono juhudui za Serikali huku baadhi wakilalamika kukatwa mishahara kuchangia chama.

Juhudi za kuupata uongozi wa Chadema kuzungumzia uchunguzi huo haukufanikiwa, kwani simu za baadhi ya viongozi ziliita bila kupokelewa na hawakujibu ujumbe wa maandishi.

Akizungumzia uchunguzi huo, naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya alisema hawajapata taarifa ila wapo tayari.

“Hatujapata taarifa yoyote ya kuchunguzwa, lakini ni sahihi tu kwa sababu fedha za mfuko wa jimbo ni za walipakodi. Huwa zinakaguliwa na CAG (Mkaguzi wa Hesabu wa Serikali), sijajua kwa nini Takukuru wanataka kuzichunguza,” alisema Sakaya.

Sakaya aliyekuwa mbunge wa Kaliuwa alisema uchunguzi huo haupaswi kuingilia uhuru wa vyama.

“Kama wanakagua mfuko wa jimbo ni sawa lakini sioni kama ni sahihi kukagua michango ya wanachama kwa sababu kila chama kina uhuru wa kuchangisha na wabunge ndiyo wanasaidia,” alisema.

Katika Bunge lililopita CUF ilikuwa na wabunge 32 wa kuchaguliwa na 10 wa viti maalum lakini watatu kati yao walihamia CCM.

Naye katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alisema hawajapata taarifa ya kuchunguzwa na Takukuru.

“Hatujapata taarifa ya kuchunguzwa na Takukuru ila masuala yanayohusu uwajibikaji sisi tuko tayari kutoa ushirikiano. Tumekuwa tukitoa ushirikiano kwa Takukuru mara nyingi tu na hata sasa tuko tayari kushirikiana nao,” alisema Shaibu.

ACT Wazalendo ilikuwa na mbunge mmoja tu ambaye ni kiongozi wa chama hicho, Zitto kabwe katika Jimbo la Kigoma Mjini ambalo sasa limechukuliwa na CCM.
Lazima wachunguzwe haraka ukweli ujulikane, chadema janja janja nyingi sana eti Haki duuu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom