UCHUNGUZI KUTOKA POLISI: Jacky Daniel" imechangia kifo cha Kanumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UCHUNGUZI KUTOKA POLISI: Jacky Daniel" imechangia kifo cha Kanumba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 12, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  RPC wa Kinondoni-Charles Kenyela

  POMBE kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha kifo cha mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam. wa Polisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi, ili kujua zaidi.


  ACP Kenyela amesema kwamba Kanumba wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa
  kwanza katika tukio hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu' na katika maelelezo
  yake amekanusha kumsukuma Kanumba. Vyombo vingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana akisema kwamba Lulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao wa wivu wa kimapenzi hadi akaanguka na kufariki dunia.


  Akizungumza kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema kwamba; ugomvi wao ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu."Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa nini alitoka nje kupokea simu,huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.


  Baada ya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje ya geti, lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,"alisema Kamanda huyo.


  [​IMG]

  Akiendelea kumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; "Baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini,"alisema. Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.

  Kwa Hisani ya Father Kidevu Blog
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Only Jack can mingle U...
   
 3. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  jaman kesi c iko mahakaman?
   
 4. andate

  andate JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 2,655
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Lulu anaweza kuwa muhusika na vilevile anaweza asiwe muhusika, hii kesi ni ngumu kujua kosa liko wapi. Maelezo ya awali kutoka kwa mdogo wa marehemu yana-imply kua marehemu hakuwa fit 100%. Kauli yake ya kusema "huyo ni daktari wake tunaemuitaga marehemu akizidiwa" ina weza kuleta picha kuwa marehemu alikuwa na tatizo la mara kwa mara. Na kitendo chake cha kuficha kunywa pombe hadharani ni pengine kuepusha feed back kwenda kwa watu waliompa masharti hayo (esp. daktari).
  inawezekana jamaa alikuwa anatumia dawa za matibabu yeyote ambazo haziruhusu pombe na akanywa jackdaniels, na jackdaniel sio pombe cha mtoto(na ikiwa ni ya mchina ndio usiseme).
  Kitendo cha kumkimbiza lulu na kumrudisha ndani kwa nguvu pengine kiliongeza mapigo ya moyo na ukijumlisha na vitu vingine alivyotumia vinaweza kumlegeza kweli na kumdondosha.(walevi wangapi wanaanguka bila kusukumwa na watu hawahoji au kwa vile sio ma-star?)
  kwa kuzingatia size ya lulu na size ya marehemu jaribu kupata picha ni kisukumo cha aina gani lulu anaweza kumpa marehemu hadi kupelekea kufariki.(kila siku kuna wapenzi wanasukumana na wanatwangana haswa kwa maana halisi ya kutwangana na hakuna anayekufa)
  Ukiangalia vifo vya ghafla vya mastaa wengi wengine utakuta ni kutofuata masharti kwenye utumiaji wa madawa either ya kulevya au mengine.
  Baadhi ya mastaa hudhani kuwa wao wako tofauti pia kimwili (mfumo wa mwili wa binadamu) kulinganisha na binadamu wengine, hivyo wanakiuka tu.
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kifupi ni kwamba lulu atatoka, mwakani hauishi atapata nolle. hana hatia wala hakuna na nia ovu hata kama angekuwa alikuwa alisababisha, hakuna na malice afore thought kuua yule mtoto aisee. naomwombea atoke haraka.
   
 6. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kakojoe ukalele
   
 7. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Jacky daniel ndio nini? Mimi najua whisky iitwayo Jack Daniel's
   
 8. b

  bob giza JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wee ndo ukakojoe ukalale....maake kwa jinsi ulivoijibu msg ya jamaa inaonekana kabisa ndo unajifunza kufikiria...
   
 9. b

  bob giza JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  jack Daniel's ni whisky inayoitwa Jack Daniel's wee mamdogo..
   
 10. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwahiyo wewe apo ndiyo umefikiria
   
 11. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Nina maswali kuhusiana na hii report ya awali:

  - Kwa nini report kamili isingojwe?
  - huu ni uchunguzi au maelezo ya lulu?
  - hii report ya kipuuzi Kwa nini mda wote huu? could have given the same report same day Kanumba died!

  Kwa kweli niliposoma kichwa cha habari nilitegemea kusikia uchunguzi wa mwili wa marehemu umeonyesha course ya death ya Kanumba na siyo mahojiano na mtuhumiwa!

  Tangu lini majibu ya mtuhumiwa yanakuwa report ya police? Tanzania goverance yaweza ingia into world wandours bila kuipigia kura
   
 12. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  nadhani umebandika huu uzi ukiwa umeshiba JACK DANIELS, maana haielezeki unapost few minutes to midnite habari yenye umri wa miezi kadhaa as if tukio limetokea jana. Huu mtirirrko unatia chefuchefu. Hongera jackdaniels.
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  HIYO ndio POLICE yetu IMARA; Hawana Forensic Investigation Gadgets... Sijui watawezaje kujua sababu ya KIFO
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Habari haina UZEE; Habari haswa kuletwa humu NDANI YA JAMII FORUMS ni Kutaka kujadiliwa na Sio Uzamani wa Habari... Kwako wewe Masaa labda yalikuwa ni MIDNIGHT lakini fikiria wengine hii ni ya kila mtu Ulimwenguni sio lazima tuwe Masaa Sawasawa; Kwa Wengine Sio USIKU... Na ni kutaka kujua ni jinsi gani walijua ni JACK DANIELS wakati wanasema hawana FORENSIC INVESTIGATIONS GADGETS???
   
 15. MST

  MST Member

  #15
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanashindwa tu kusema polisi kuwa huu ndo ukweli - kesi inazuia hata watu wenye taarifa kushindwa kuzianika hadharani, lkn ukweli ni kwamba chanzo cha kifo hiki ni pombe - na ushahidi upo lkn umekaliwa.
   
 16. kadagala1

  kadagala1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2017
  Joined: Nov 23, 2016
  Messages: 4,553
  Likes Received: 4,121
  Trophy Points: 280
  Ndio anaianza safari dah.
   
 17. ras jeff kapita

  ras jeff kapita JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2017
  Joined: Jan 4, 2015
  Messages: 5,672
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  Hawezi toka atafungwa huyo
   
 18. m

  miwani ya maisha JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2017
  Joined: Dec 30, 2015
  Messages: 881
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 180
  POLISI WANATAMANI WAO WAWE NDIO MAHAKAMA
   
Loading...