Uchunguzi huru: Ifikapo 2060 Asilimia 60 watu Watakuwa Wachawi, 90% Watakuwa Washirikina

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,879
IFIKAPO 2060; ASILIMIA 60 WATAKUWA WACHAWI, 90% WATAKUWA WASHIRIKINA TZ

Na, Robert Heriel

Hobby yangu ni udadisi, uchunguzi, utafiti na mambo yote yahusuyo upelelezi. Kwa namna hiyo kwangu kujua mambo mbalimbali ni ishu ya kawaida Sana.

Hobby yangu hiyo Inategemea zaidi Kusoma vitabu, vijarida, mitandaoni; pia kukaa vijiweni na vilinge kupata dondoo mbalimbali. Vyanzo vingine ni pamoja na Redio, luninga na hata filamu.

Kwa uchunguzi huru nilioufanya Maeneo mbalimbali Kama nilivyotaja hapo juu, ninachelea kusema kuwa Ifikapo 2060 kutakuwa na Ongezeko kubwa la Wachawi litakalofikia 60% huku Washirikina wakifika 90%

Hali ilivyo sasa ya Uchawi na Ushirikina mtaani.

1. Kwa sasa Wachawi ndani ya jamii sio wengi
Katika ulizia ulizia yangu nikabaini kuwa Tanzania, wachawi ni Kama Asilimia 8%. Nilibaini kuwa kwenye kwenye familia au kila koo, basi lazima awepo mtu mmoja anayetuhumiwa Kwa uchawi au mchawi Kwa dhahiri. Hata hivyo ni koo chache Sana zilizokosa mchawi hata mmoja kulingana na Sample nilizozihoji. Uchunguzi wangu unaonyesha kwenye Koo Kumi basi Koo nane sikuweza kuwa na walau mchawi mmoja. Mbili hazikuwa na Wachawi.

2. Kuhusu Waganga ambapo nayo ni Aina ya uchawi, ni Asilimia ndogo Sana

Hata hivyo miaka ya hivi karibu Kumetokea Ongezeko la Waganga kutokana na maslahi ya kazi hiyo. Hata hivyo uchunguzi wangu ulibaini kuwa Waganga wengi walioingia Zama hizi wamebobea zaidi kwenye Fani ya Ramli alimaarufu Kama kuchora, kuchungulia, au kutazama. Wengi hawawezi kutibu wala kutoa mafanikio.

3. Wachawi wengine wamejiingiza katika Dini
Wapo Wachawi wachungaji na masheikhe ambao hujifanya watumishi lakini upande wa nyuma ni Wachawi vigagula. Uchawi wao umejikita zaidi kuloga Fikra za wateja wao ambao huitwa waumini wao.

Wachawi hawa wakishaloga Fikra/Akili ya wateja wao huwezi muambia tena muumini kuhusu mchungaji wao.

USHIRIKINA

1. Kwa upande wa ushirikina hili kundi ndio wapo wengi.
Kwa sasa Ushirikina ni Asilimia 40.

Katika uliza uliza zangu. Kwenye watu kumi, wenye umri wa utafutaji maisha yaani kuanzia miaka 25+, watu wanne wameshawahi kwenda kwa Waganga WA kienyeji na wanaamini katika Ushirikina.

2. Kundi hili linaamini huwezi kufanikiwa bila Kwenda Kusafisha au Kubusti nyota yako Kwa Waganga WA kienyeji.

3. Kundi hili pia linaamini kuwa Kufeli kimaisha kunachangiwa na kulogwa.

4. Kundi hili limejawa zaidi na wanawake, Wafanyabiashara, wanasiasa, na Wafanyakazi WA umma.

Hali itakavyokuwa

UCHAWI NA USHIRIKINA MWAKA 2060

1. Wachawi wataongezeka kutoka 8% mpaka 60% ya watu wenye umri wa utafutaji.

2. Watu wengi watatumia ule uchawi rahisi kwani uchawi mkubwa ni gharama na unahitaji pesa nyingi kuzimiliki

3. Wachungaji watapungua hasa Wale wasio na uchawi mkubwa, watabaki Wale wenye uchawi mkubwa wenye gharama.
Hawa wachungaji wadogo soko Lao litadorora kutokana waumini wengi nao watakuwa wanauchawi mwepesi unaolingana nao.

4. Madhehebu makuu za Ukristo na uislam Kama vile Ukatoliki, Ulutheri, Usabato yatapoteza mvuto Kwa sababu hazitakuwa na uwezo wa kutatua kero na changamoto za wateja wao ambao huitwa Waumini.

Wachungaji wa madhehebu haya yatajikita zaidi kwenye fundisho la hizi ni siku za mwisho wa Dunia ilhali Dunia haitakuwa na mwisho isipokuwa Madhehebu yao ndio yanaufikia mwisho wake.

5. Pesa zitakuwa nyingi, karibu kila mtu atakuwa na pesa lakini zitaendana na uuzaji wa roho. Kutokana na watu wengi kuwa na uchawi mwepesi, Sarafu za kichawi na kuzimu zitabadilishwa na Sarafu za kibinadamu yaani Sarafu za kawaida.

6. Kutokana na Teknolojia ya kisayansi itakuwa juu, hii itazidisha gharama za vifaa na Zana za uchawi na Ushirikina kuwa juu. Uchawi utakuwa na gharama kuliko gharama ya Teknolojia.

7. Siasa za wakati huo, kutokana na Watu wengi kuwa na self awareness kuhusu Masuala ya roho kwenye Uchawi, serikali itajikita katika Sera za kulinda maslahi ya Wachawi ikiwemo Sarafu yao.

Haitakuwa rahisi kuwa Mwanasiasa bila kuwa Mchawi, na pasipo kutumia Sarafu yao.

8. Kwa vile miaka ya 2060 Nusu yetu wanaweza easier hai. Kizazi hiki wengi watauza Roho zao wapate Sarafu ya Kuzimu ambayo ikibadilishwa na Sarafu ya kibinadamu ni hela nyingi.
Ni kusema kizazi Hilo wengi watakuwa wameuza roho zao.

9. Mkakati wa kukidhibiti kifo utaanzishwa. Kwa kushirikiana na Teknolojia ya uchawi na Teknolojia ya kibinadamu, Kifo kitadhibitiwa lakini Mradi huo utaanza Kwa waliojiunga na Uchawi Kwanza. Hiyo itakuwa miaka ya 2120.

10. Ili kubadilisha 40% ya watu ambao sio Wachawi kuwa Wachawi, itaundwa njama ya kuleta ugonjwa unaotokana na kuota ndoto mbaya ukilala usiku ambapo mtu akishaota ndoto hizo huamka akiwa amepagawa au anakifafa, ndoto hizi zitaratibiwa na Falme za kichawi. Kutokana na Watu hawa watakuwa hawaamini katika uchawi wataenda kwenye Hospitali kupata matibabu lakini Teknolojia ya kibinadamu itashindwa. Hivyo Wachawi watachukua advantage. Usipojiunga na uchawi basi utaendelea kuugua Kwa majuma kadhaa mpaka utakapokufa.

11. Baada ya ugonjwa kuisha, na hii ni kutokana na Kifo kudhibitiwa vilivyo, ni wazi Dunia nzima itakuwa under Falme za Kuzimu.

12. Nikirudi kwenye miaka ya 2060;
Wengi wataingia kwenye Uchawi kutokana na Upweke na maisha kuwa magumu.

14. Magonjwa ya wakati huu yanatokana na Mabadiliko ya tabia ya nchi, uchafuzi wa mazingira, na lishe, lakini miaka hiyo magonjwa mengi yatakuwa yanatokana na Nafsi na Roho. Ambapo ili yatibike haitahitajika Teknolojia ya kibinadamu.

15. Uhusiano wa watu;
Bado Muafrika atakuwa chini ya utumwa.
Mataifa Makubwa yatatukia gharama kubwa kuhodhi Uchawi kutoka Maeneo mbalimbali Kwenye sayari na nyota zingine. Na yatakuwa na Akiba ya kutosha ya Uchawi huku Waafrika wakibaki na uchawi mwepesi.

16. Baadaye Sana, Teknolojia ya Uchawi itajenga daraja linalounganisha Dunia ya waliohai na Kuzimu
Watu Waliohai watakuwa na uwezo wa kwenda na kurudi Kuzimu, na wafu watakuwa wanakuja Duniani na kurudi Kuzimu pasipo shida yoyote. Automatic kifo kitakuwa kimedhibitiwa.

Hata hivyo daraja hili litatumiwa na wanachama pekee.

17. Dunia itakuwa kwenye Giza Kwa Karne 6, tangu miaka 2060
Giza la uchawi na ufalme wa Kuzimu.

18. Watu watajaa wengi kutokana na Kifo kudhibitiwa

19. Vyombo vya Teknolojia vya kibinadamu na kichawi vitajienda kwenye Nyota za mbali, mpaka nyota ya Tibeli
Hapo ndipo anguko la uchawi litatokea.

Uchunguzi huru umeishia hapa. Sitaki maswali.

Ulikuwa nami, mwana kutoka Tibeli, nyota yenye Mbawa mbili, ing'aayo

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
๐Ÿ™‡๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ๐Ÿ™‡๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ๐Ÿ™‡๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ๐Ÿ™‡๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ
 
Kwahiyo 2060, Mungu hatakua na nafasi duniani bali uchawi ndio utatamalaki??

Na hiyo tafiti ingeonesha tulikotoka, tulipo na hiyo 2060 ingekua bomba sana. Wewe umeeleza wakati tulipo mpaka 2060. Umewezaje kukadiria bila kujua trend ya nyuma ilikuaje mpaka kufikia hiyo 8% na kutabiri yajayo??
 
Nakubaliana na wewe mtafiti.

Ni muhimu kila mtu achague atatumia nguvu gani, nguvu za nuru ama nguvu za giza.
 
Lakini 100% watakuwa WAZINIFU
Hadi saa nikiwa na simu hii ya itel nikiandika ni 85%

Kama unataka kujua angali thread wazochangia
1. Kula Tunda kimasihara
2. Nafuta mme au mke
3. Ndoa yangu iko...
Yaani nyuzi zote zenye Neno mbususu, mshedede, makalio, kibamia n.k zinachangiwa mno

Ukiandika Uzi wa Kilimo hupati like, reaction au comment nyingi na wengi kwa kutaka followers wanaandika hizo
 
Inawezekana,maana wanawake walivyokazana kuroga(limbwata) wapenz na waume wao tena bila kificho...I swear twifwa
 
Back
Top Bottom