Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,290
- 33,873
JAMANI
Nafikiria na kufaraki kuhusu hili sakata la aibu na uzalendo wa kifisadi dhidi ya nchi yangu na watu wake. Ni kweli kwamba sasa hata mkulima kijijini ameshagundua kwa nini gharama za usafirishaji na usindikaji zinapanda kila kukicha. Ni kweli kwamba aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania alikuwa anakwenda huko vijijini na kuwa-bullying maafisa wa serikali mbele ya kadamnasi ili ionekane kwamba hawafanyi chochote. na zaidi sana sana ambapo alitia fora ni pale alaipoamua (JK alikuwa marekani) kuwatawanya mawaziri waende mikoani kuelezea ubora (uozo) wa bajeti na watwana wake wakaambulia kuzomewa na kukebehiwa na wananchi kila waendapo (due to the BOT saga iliyoshtakiwa kwa wananchi kutoka kwa vyama vingi). Kumbe kulikuwa ni upotoshaji na uongo wa hali ya juu, i mean ni uuaji na ukosefu wa utu wa kiwango cha kutisha. Leo hii tunapata ukweli ambao ulikuwa ni kawaida kuwa nyuma ya pazia (wengi wamehusika).
Kuhusishwa kwa moja kwa moja Waziri mkuu ktk kashfa ya kuliangamiza taifa ni zaidi ya uhujumu au uhaini, Ni sawa na kuliua Taifa ili apate faida yeye na mafisadi wenzake. Pamoja na kwamba ameikebehi ofisi ya waziri mkuu, pia amefanya kitendo cha ujasiri wa kifisadi ambapo anakuwa ni kiongozi wa juu wa kwanza afrika kutuhumiwa na kuwajibishwa akiwa madarakani (kama sikosei). Nashindwa kuelewa na nakataa kuzikubali kauli zake zoote alizowahi kuzitoa awali kuhusu maendeleo ya nchi ama akiwa bungeni au kokote pale. Alikuwa anatupuuza mno huyu baba. Hata wakati ripoti ya kamati teule inasomwa kuna wasaidizi wake mfano chenge na kingunge ambao walisema kuwa ripoti imejaa ubabaishaji na taarifa za uongo. Hii ni dhahiri kulinda heshima ya kifisadi ambapo ule msemo wa uwajibikaji wa pamoja wanautumia vibaya, yaani kumlinda mtuhumiwa ambaye ni kizito ktk serikali wanayoiibia. Na kwa mshangao wangu katika wooote waliotangaza kujiuzulu jana hakuna hata mmoja aliyekiri kuhusika ktk sakata hilo, ina maana mkataba huu ulijiendesha automatik mpaka kusainia na kuhaulisha kwa dowans????? Hii ni kashfa kuliko zoooote nchini, naamini kuwa wahusika hawa wana conspiracy nyingine zaidi ya hii. Nashawishika kuamini kuwa hata ripoti ya BOT ilikuwa inasubiri matokeo ya richmond ili wanaokwenda na maji waache uwanja mpana kuishighulikia pasipo wao kuingilia upekuzi yakinifu wa wanaohusika na mienendo-fisadi ktk BOT na mikataba mingineyo. Naamini sana kuwa huu ni mwanzo. Nakumbuka ktk thread moja hapa ktk JF tulikuwa tunajadili hazina kukaukiwa hela, na nikahoji kuwa hao wataalam wa bajeti kwa nini walilidanganya bunge na serikali kwa kutoa bajeti ya uongo isiyo na uhalisia?? wakaja watu hapa na utetezi mwiiiingi kuwa hakuna kosa na bajeti ni sahihi. lakini kumbe walikuw wanajua kuwa wanatetea uozo wa mawaziri na hazina kutuibia kodi zetu.
Nina habari za uhakika kuwa kule keko kuna mahabusi imekarabatiwa na kuwekewa viyoyozi na huduma za kihoteli ambapo nashawishika kuamini kuwa Rais anajua alitendalo na kuna wanene wataenda kupanga kule. Natamani aanze Lowasa (aoneshe njia) na wengine wamfate. Nakumbuka niliahidi kupika pilau endapo baraza litavunjwa nitapika pilau, nawaalika ktk sherehe ya pilau wana JF
Hapa nina maswali magumu ayanayonitatiza, Je hizo fweza za Richmond zingeokolewa na kufanyiwa kitu cha maana je
zingejenga au kuboresha
SWALI
je Lowasa na wenzake wafanywe nini?? na hatua zipi muafaka kwao zaidi ya kujiuzulu?
nina uchungu haswa.

- zahanati ngapi?
- madaraza mangapi?
- mishahara ya walimu wangapi?
- wanafunzi wangapi wa vyuo wangekopa? (mkopo wa kurejesha)
- madakitari wangapi wangeajiriwa?
- barabara ngapi zingekamilika?
- nyumba ngapi za polisi?
- magari mangapi ya zimamoto yangenunuliwa?
- pembejeo zingekosekana?