Uchumi wetu unaweza kuanza kuanguka mwishoni mwa 2023: Rais Samia anahitaji "National Security Advisor" aliyebobea sana

Fatma-Zehra

Senior Member
Oct 18, 2020
192
1,062
Shikamoo mama. Pole na majukumu. Bado ninaamini kuwa wewe una utu. Endelea kuwa na utu na siyo ulegevu. Majizi ni mengi kuliko idadi za pikipiki zilizoko mkoa wa Katavi. I love you. Naomba nikupe ushauri.

Data zinaonyesha mambo yafuatayo:

1. Mwaka 2022 yawezekana kukawa na njaa Kali sana nchini.
2. Maisha yamepanda sana kwa sasa. Kwa sasa wafanyabiashara wanapandisha bei ya vitu namna wanavyotaka na wanavyojisikia.
3. Biashara nyingi ambazo ni formal zinasinyaa lakini taratibu sana tena sana.
4. Jitihada za kuipunguza na kui-manage informal sector hazipo tena. Kumbuka hii informal sector yetu ina athari mbaya zaidi kwenye uchumi, hasa mapato.
5. "Covid ya 2022" imekaribia.
6. Kodi zinaushambulia uchumi wakati uzalishaji umepungua.

Tusipotafuta majawabu ya hizi hatari sita hapo juu, kuna hatari ya uchumi wetu kuanza kuanguka mwanzoni mwa October 2023 na inaweza kutuchukua muda mrefu kurudi katika hali ya kawaida. Naomba nikupe tips zitakazokusaidia katika majadiliano ya kutafuta solutions. Ninaweza kuwa niko wrong pia.

1. Food security ni neno pana sana. Food security ni usalama wa taifa. Kama ningekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa let's say 2005, ningekuwa na mpango wa ku-forestate taifa kwa angalau miti bilion moja kwa miaka 16. Ningetengeneza misitu mikubwa sana ya kitaifa na maziwa makubwa (siyo ya kwangu. Namaanisha lakes) ambayo ni artificial. Ningetafuta masoko ya kudumu ya chakula nje ya nchi kwa miaka 16 kwa bei ambayo ni nafuu sana. Leo tungekuwa na "investors wa kati na wakubwa" wenye production capacity kubwa ya mazao ya kilimo. Ingawa tumechelewa, njia ya haraka ni investment ya serikali kwa wakulima wakubwa na wa kati wanaoweza kuzalisha chakula. Majeshi yetu yangeweza kufanya hii kazi kwa kuanza na vijana wa JKT na wale wanaozurura mijini bila kazi.

2. Kama usipoweka policy na sheria pamoja na mikakati madhubuti ya kupunguza gharama za maisha hasa bei za vitu, tutajuta kama taifa muda si mrefu.

3. Tuweke mfumo mpya wa kutambua transactions na ku-document supply chain kwenye uchumi wetu.

4. Pesa zetu za ndani zisitumike kwenye mbinu za covid zilizofail. Pesa za ndani ni pamoja na mikopo kutoka kwa wazungu. Usije ukafunga uchumi hata kidogo kisa covid. Taifa litasinyaa. Usalama wa nchi yetu utayumba kabisa au kuanguka.

5. Sina uhakika kama nchi yetu ina mtu anayeitwa "National Security Advisor". Kama yupo, kuna haja ya kumfukuza kazi. Ila kama hayupo, teua haraka. Yeye ata-design mpango wa muda mfupi kwa ajili ya 2022 to 2024 akilenga kutatua hizi changamoto zilizofungamana na masuala ya usalama wa nchi. Lakini atatengeneza mpango wa muda mrefu, yaani wenye phase mbili za utekelezaji wa miaka minane minane. Hata hivyo, njia pekee ya kumpata mtu wa namna hiyo, ni lazima iwe ya uwazi na isiyo na upendeleo wa aina yeyote.

Siku njema. Ngoja nipate kwanza breakfast.
 
Inashangaza sana pale ambapo kupanda kwa bei za vitu kunahusishwa na kufungua nchi, mfano; mazao kuuzwa nje ya nchi kulilenga kuongeza pato kwa mkulima, lakini ajabu bei ya mbolea nayo inapanda kila siku, sasa hapa kuna haja gani ya kuhangaika kuzunguka dunia yote kwa kisingizio cha kufungua nchi wakati hapa ndani mambo ndio kwanza yanazidi kujifunga?

Namshauri Rais aache kufanya kazi kwa kukariri, habari ya kufungua nchi sasa imeshafeli; kuna tatizo kubwa sana la ukosefu wa ajira, halafu on top of that gharama za maisha zinazidi kupanda, atulie chini na wataalamu wa uchumi wamuoneshe namna mambo yanavyotakiwa kwenda, kuliko kuendelea kupanda ndege kila siku wakati impact ya hizo safari zake kwa mtanzania wa kawaida ni zero.

Kikwete licha ya kupanda ndege miaka yake yote bado uchumi wa nchi ulikuwa mbaya na nchi ikageuzwa shamba la bibi, huu ushauri anaopewa ni vyema sasa atulie chini achanganye na zake, atuoneshe yeye kama yeye ana kitu gani kwenye kichwa chake, anataka kuiona Tanzania inaelekea wapi kwa mipango mipya ipi, sio hii ya kufungua nchi kila siku na kuhutubia kila aendako huku mambo yetu ndani yanazidi kuwa magumu.
 
2023 mbali hivo, miezi 6 tuu ijayo patakiwa hapatoshi.

Refer:

Bei ya mbolea kupanda.
Bei ya vifaa vya ujenzi kupanda.
Bei ya mazao kushuka.
Umeme usio na uhakika.
Ukame unaoendelea kushika kasi.
Watumishi kutoongezewa mishahara.
Wafanyabiashara wadogodogo kufukuzwa kwenye maeneo yaliyokuwa na mzunguko mkubwa wa biashara
Ukiona pembejeo za kilimo zina mfumuko wa bei lakini mazao hayana thamani basi ujue kuna kitu hakiko sawa na uchumi unaweza collapse muda wowote.
 
v4N.jpg
 
Kuna mtu alisema advisor ni Bill Clinton labda kama zilikuwa story za mtaani.

Mengi uliyoweka naunga mkono kwa kugonga kistuli changu maana sina meza ningegonga kama wabunge. Sijasikia ukigusia bandari ya Bagamoyo itakayokuwa na miundo mbinu ya kisasa kuliko zote nchini.

Naona kama tunaingizwa mkenge kiasi kwamba ikisha kamilika mchina ataanza kudai deni lake la sivyo tumalizane kwa kufunga bandari zote na kumwachia yeye peke yake. Naona mbeleni mchina akiwa anaingiza bidhaa kutoka nchini kwake na kuzitawanya nchini huku akizuia uzalishaji wa ndani unaofanana na bidhaa anazotaka ziingie.

Mpaka sasa haijulikani nani mkweli kati ya waziri Mwambe aliyesema mkataba haukuwepo, JK (Aliyeweka jiwe la msingi, na Magu(RIP) aliyesema mkataba ni mbovu.
 
Kwenye food security ni rahisi kwa sababu tayari tuna NFRA. Cha kufanya ni kuhakikisha inawajibika katika najukumu yake ipasavyo. Ikiwezekana iundwe upya kwa kupeleka mswada bungeni na kupeleka watu wenye sifa na wanaoweza kuchapa kazi na kuhakikisha nchi ina akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya kusupply kwenye uchumi pale panapotokea uhaba.
 
Ushauri toka kwa mama kwenda kwa mama. Mi ninachojua hata njaa ipige kiasi gani ukiwa na pesa hakuna matata. Somalia ni jangwa lakini kupitia utekaji wa meli watu wanashiba. Muhimu kila mtu atafute pesa kwa bidii zaidi ya jana na leo, serikali ni mimi na wewe.

Madam Fetty, so far umeotesha miti mingapi wewe kama wewe? Au mpaka tukupe Li V8
 
Zamaini watawala walikuwa wanaangalia uongo wa miaka mitano hadi kumi kudanganyia wapiga kura, sasa watu wameelevuka na kila fix inayopigwa wanaing'amua. Matokeo yake ukiwaeleza ya mwaka 2023 wanaona unazingua maana wengi siku hizi wanawaza ya leo, mwenye 'akili' zaidi anawaza ya juma lijalo.
 
Hizo ndio data au wewe ndio unaombea huo uchuro ambao kamwe hauwezi kuja kutokea hapa Tzn 😄😄

Tafuta kiki nyingine,hatari pekee iliyokuwepo ilikuwa ni mafuta nayo yamedhibitiwa, pili alikuta forex imeshuka kwa mda mfupi imeongezeka kutokana na exports kuongezeka na mwisho investors wanamiminika.

Hicho unachotaka kitokee kitatokea ufipa huko sio Tzn ya Samia, never, labda wapumbavu wenzio ndio watakuunga mguu.Banks kwa mda mfupi zimepata faida kubwa na zimeongeza ukopeshaji.

Kwa taarifa yako official statistics kutoka Serikalini na Mashirika ya kimataifa yanatoa positive trend na rebound kwenye uchumi..Na ukame mlioombea imekula kwenu mvua zimeanza kunuesha kote na kilimo kinaendelea sasa. Kama ndoto zako hazikutimia lala uote tena.

Uchumi haukuanguka kwenye nchi hizi hapa sembuse Tanzania?🤣🤣

Screenshot_20211022-185621.png


Screenshot_20211022-185717.png
 
Kwenye national security advisor, muundo wa taasisi ya ujasusi na usalama Tanzania, ni wa siri. Na majukumu mahsusi ya mtu sio lazima yatajwe huko. Lakini kuna watu ambao majukumu yao yanafanana na hilo la nationa security advisor. Lkn pia ni swala la miundo katika nchi za Jumuiya ya Madola na nchi ndogi zetu hizi ambazo sio kubwa kama USA au China au Canada.
 
Back
Top Bottom