Uchumi wa Tanzania

Ukweliii

Member
Feb 10, 2008
58
0
Ni suala lililowazi kuwa uchumi wa Tanzania umeshikiliwa na watu ambao siwananchi. Angalia majina Bakhresa, premji, dewji, rostam na wapo wengine wengi. Ndio maana kuna skandali kila siku na majina haya yanahusika (Hawana uchungu) Hakuna hata haja ya kutaja hizo skandali lakini hii ya sasa ya Richmond imenikera sana maana hata jeuri wanayoonyesha kwa kuwa wana washikilia wanasiasa na viongozi wa TZ. Ninapatwa na simanzi haswa ukifikiria kwamba kwenye skandali zote huwa wanatoka wakiwa matajiri zaidi na wanaolia ni hao wanasiasa na wananchi.

Richmond imemdondosha Waziri Mkuu alikuwa na dhamana kubwa sana. Lakini lakini kaingizwa kwenye mkenge na HAOOO. Sawa ni tamaa zake au whatever lakini nani antakaefuata, RAIS??
Aibu Kubwa sana
Wakati umefika kwa wananchi kudai na kuchukua Uchumi wa TZ. Haiwezekani wakulima wa korosho na pamba waendelee kulipia hizi skandali zinazowatajirisha HAOOO
 
Ndugu Ukweliii,

Hao watu ni raia. Sasa lakini, inawezekana kuwa raia bila kuwa mwananchi. Hao si WANA wa nchi yetu, lakini ni raia. Wako mguu mmoja Tanzania na mguu mmoja nje. Wana pasi mbili kama Balali. Ni ajabu kwamba kuwa na pasi ya Tanzania na pasi ya nchi nyingine ni kinyume cha sheria za Tanzania, lakini Balali alikuwa na pasi mbili na bado akapewa Ugavana wa BoT.

Watu wa aina hii walianza tangu hata wakati wa Mwalimu. Angalia Amir Jamal aliondoka kwenda Canada mara alipoaacha kuvuna. Alikuwa raia lakini sio mwananchi. Kuna watakaosema aliondoka kwa ajili ya ugonjwa, lakini hiyo ni danganya toto. Tulikuwa na waziri wa afya wakati wa siku za mwanzo ambaye asili yake ni mzungu. Huyo alibadilika akawa mwananchi, tena wa Manzese. Kuna raia na wananchi.

Wahindi, na Wairan (kama Rostam) wanajua kwamba kuna mafisadi wako katika ngazi za juu CCM. Wanajiunga na CCM ili kushirikiana nao kukamua wananchi. Wanalindwa kwa karibu na viongozi wa juu wa CCM. wamekuwa marafiki wao wakubwa.
 
Watu wengine wana mawazo na siasa za chuki na ubaguzi, awe na jina na rangi yeyote ile, ili mradi ni mtanzania basi asibaguliwe kwa rangi, jina au dini yake.

Leo, watanzania wangapi wanaoishi nje ya Tanzania na wengi tu wamechukuwa uraia wa nchi wanazoishi na wengi tu wamekwenda kwenye hizo nchi bila hata ya msingi au kuwekeza na wengi ni matajiri huko waliko.

Besides, historia ya Afrika mashariki haionyeshi ni lini muhindi, au muarabu wa kwanza alikuwepo katika ardhi hii ya Tanzania, tunajuwa wazungu tuu (1497).

Utanzania au Uafrika wa mtu haupo kwa rangi au jina lake. Hapa Tanzania kwa mfano kuna wa-Iraq (Mbulu) inasemekana asili yao ni kutoka Iraq, jee leo tuseme wao si watanzania? au kina nyerere ambao kwa mujibu wa habari za hapa na pale inasemekana si wenye asili yao huko butiama, jee na wao si watanzania? wakina mkapa, inasemekana ni wamakonde na asili yao ni msumbiji, jee tuseme na wao si watanzania? wangoni inasemekana walihamia kukimbia vita huko south afrika (enzi hizo sijui ilikuwa inaitwaje), jee hao nao si watanzania? wengi tuu, kuna wangazija, kuna wanubi, mifano ni mingi na pengine wewe uliyeanzisha hii thread ukitutajiya kabila yako tunaweza kujuwa asili yako ni wapi, lakini hatuta-kubaguwa kwa hilo.

Wacheni fitna na siasa za kibaguzi ambazo hazina kujenga bali kubomowa.

KUMBUKA, kwa miaka mingi sasa pande kubwa la budjet yetu linatoka nje ya Tanzania na hao wanaochangia budjet yetu sidhani kama ni wananchi wa Tanzania. Au huo si uchumi?
 
Nakubalina nanyi kwamba siasa za ubaguzi wa rangi sio nzuri. Wako Wahindi na Waarabu wengi ambao wanaipenda nchi yao ya Tanzania kwa dhati. Wako vile vile mafisadi wengi ambao si Wahindi wala Waarabu.

I may have misspoken. Hata hivyo, hali halisi inafanya wengi wadhani kwamba wafanya biashara wakubwa Tanzania karibu wote ni corrupt. Na karibu wote ni Wahindi. Ukienda duka kubwa la spea za magari au la vifaa vya ujenzi litakuwa la Mhindi, na atakupa chaguo kati ya bei mbili: au ununue kwa bei ya bila risiti (na hivyo bila kodi) au akupe risiti lakini ulipe zaidi. Inakuwa ni kuendekeza corruption.

Wafanyabiashra wasio Wahindi nao karibu wote ni corrupt. Inawezekana wameiga Wahindi na Waarabu.

Kwa vyovyote vile nakubali kwamba ufisadi hauna rangi.
 
Hoja yangu kama mkiiangalia kwa makini haina UBAGUZI ila ukweli wa hali ilivyo. Wananchi wenye nguvu za kiuchumi TZ ni ndio hao. Hili halipingiki!!
Kihistoria hili lina uhusiano na siasa ya UJAMAA. Suala ni kuwa juhudi za wazi na makusudi zinatakiwa ilikuwawezesha waTZ waliokumbatia ujamaa waweze kupata nguvu za kiuchumi. Sasa hivi " the playing field is not level".
Wachangiaji wengi wa hoja hii wanatoa hoja za wanasiasa wa TZ wasio na mtazamo wa mbali na kukataa madhara ya UJAMAA.
Ninalinganisha na madhara ya Ubaguzi wa Afrika ya Kusini (Si mfano mzuri) bali wazungu wachache walinufaika kwa kuwa na nguvu za kiuchumi. TZ wale ambao hawakuwa na kijiji, hawakunufaika na UJAMAA na hawakukumbatia UJAMAA, ndio leo wanye nguvu za kiuchumi. Affirmative action si ubaguzi. Bali ni juhudi za ku- redress the effects of a historically popular Policy.
Hii inahitaji kueleweka kwa wananchi wenyewe na wao kuchukua hatua na pia serikali kuwa na sera za uwezeshaji.

Hoja yangu haina nia ya kumnyang'anya mtu chochote bali kumuwezesha aliyen amini na kutekeleza sera ya ujamaa. Kuuzia wananchi hisa za makampuni ya umma haitoshi. Nchi nyingine za Kijamaa wamefanya zaidi ya hivyo (Urusi)
 
Kwa upande wangu naona hapa kun vitu viwili kama si vitatu,(UZALENDO,'URAIA&UBAGUZI')
Kwa wale ambao ni wazalendo ni wale ambao Tanzania ni wao na wao ndiyo Tanzania,huwezi kuwatofautisha wao na Tanzania au Tanzania na wao.Wanalia,wanaumia,wanasononeka wanapoona Mtanzania anataabika,anaburuzwa,hawezeshwi n.k Watu hawa Tanzania kwanza kisha wao,waadilifu kwa Taifa lao,waaminifu above all can offer almost everything for the sake of building the nation.
Uraia ni tofauti na uzalendo (is all about rules,laws,rights &responsibilities za kuishi mahali husika)raia ndiyo hao utasikia wala rushwa,mafisadi,wakwepa kodi,wabinafsi,wamimi&wasisi n.k
HIVYO BASI UBAGUZI TUUFANYAO SI WA RANGI,DINI,KABILA,JINSIA BALI WA "MZALENDO &SI-MZALENDO"
HOPE NIMEELEWEKA!
"WATU HAWA MOST OF THEM SI WAZALENDO JAPO NI RAIA>>>>!!!!
 
Naomba nitofautiane na maoni ya mtoa mada kwa kusema kwamba haijalishi hata kidogo nani ana nguvu ya kiuchumi, rangi, asili, au uraia wake.

Binadamu wote tunaweka maslahi yetu mbele kabla ya maslahi ya taifa. Hivyo basi tutafanya kila njia, zikiwepo njia ambazo haziendani na maslahi ya nchi katika kuhakikisha kwamba maslahi yetu binafsi yanatimizwa. Na ndio maana tukaona umuhimu wa kuwa na serikali ili maslahi ya nchi yatimizwe sambamba na ya maslahi binafsi. Ili wanyonge na wasio na nguvu za kupigania maslahi yao wawe na mtetezi. Ili maeneo yasiyo na nguvu za kiuchumi yawezeshwe.

Inapotokea wahindi au watu wakikundi au kabila fulani kuwa na nguvu kubwa mno ya kiuchumi kulingo wengine kiasi cha kuathiri standard ya maisha katika nchi, manake serikali imeshindwa kutimiza wajibu. Tukilaumu wahindi tunakosea na hatuwatendei haki kwasababu wao kama sisi kwanza wana act on self-interest.

Jibu hapa ni KODI KODI KODI KODI. Pili ni matumizi ya kodi hizi. Kwenye nchi za wezentu kodi hazikwepeki na kadri mtu anajaribu kuwa na nguvu zaidi za kiuchumi ndivyo kodi inavyombana na kumfanya awe sambamba na na watu wengine wakaiwada. Usawa wa maisha hautokani na kuwanyang'anya wahindi mali zao bali unatokana na kodi zitakazowafanya waone kwamba kumbe kadri wanavyojilimbikizia mali ndivyo wanavyoinufanisha nchi kwa kodi.

Vile vile kama matumizi ya kodi hizi hayalengi katika kuleta uwiano wa kimaisha baina na wenye nguvu na wasio na nguvu ya kiuchumi ni kazi bure. Again, hapa wakulaumiwa sio wahindi, bali ni uongozi ambo umewekwa kuleta na kutetea maslahi ya nchi.

Hakuna ubaya kwa wachache kuwa na nguvu ya kiuchumi kwasababu hao ndio watakao kuwa na uwezo mkubwa kulipa kodi inayoendana na kipato chao. Ubaya unakuja tu pale uongozi unaposhindwa kulifanya taifa linufaike kutoka kwa wachache wenye nguvu.

Katika dunia ya leo isiyo na mipaka ya kiuchumi, uraia na uzawa hauna nafasi. Tumeona wamarekani viwanda vya USA vinahamishiwa India ili kupata wafanyakazi wa bei poa, kadhalika Tz tupo na EAC ambayo pamoja na mambo mengine italeta makampuni kadhaa kutoka nchi wanachama. Sasa leo kama tunawalalamikia wahindi tuliokuwa nao hata kabla ya uhuru, tutasema nini kwa makampuni yatakayokuwa yanaingia Tz na kuchuma machoni mwetu? Je napo tutaomba makampuni hayo yatoke Tz au kuyanyang'anya mali?

Wahindi wanahitajika sambamba na wawekezaji wa nje. Tunachohitaji ni system itakayo hakikisha kwamba maslahi ya nchi yanatetewa vilivyo. Kuhakikisha kwamba mwananchi wakawaida ananufaika kupitia fedha zitokanazo na kodi na mikataba.

Pili kusema kwamba lazima tufanye playing field is iwe leveled kutokana na athari za siasa za ujamaa ni kujirudisha nyuma hatua tisini na kenda. Uchumi wa soko huria una automatic self-mechanism ya kufanya playing field iwe somewhat leveled. Kwa mantiki kwamba mwenye zaidi ya kile alichonacho mwananchi wakawaida kitapokonywa kwa kodi itakayokuwa sambamba na kipato chake. Kwa hiyo basi affirmative action in addition to taxation ni sawa na kumvua nguo mwendawazimu (mana angezivuwa anayways).
 
Back
Top Bottom