Uchumi wa Tanzania unakuwa Vizuri:Benki ya Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumi wa Tanzania unakuwa Vizuri:Benki ya Dunia

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Bajabiri, Jul 8, 2011.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Benki ya Dunia imesema kuwa uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi sana,kwa mujibu wa mchumi wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika bwana Shanta Devarajan amesema kuwa uchumi wa Tanzania umekuwa kutoka asilimia 3.5 mwaka 1996 hadi kufikia aslimia 7.8, amesema kuwa ili uchumi ukue zaidi inapaswa kuhakikisha kuwa watanzania wanawezeshwa kwenye sekta ya Kilimo,na pia nishati ya umeme inapatikana kwa watanzania wengi

  Source:Swahili-radio tehran,pitia kwenye wall yao ya face book.

  My take: Sidhan kama kuna mtanzania anepaswa kusikia habari hizi wakati anaona mambo ni tyt kwake,hawa WB huwa wanafanya risech au wanapewa ripoti na kuziamini? Maana serikali haishindwi kuandaa a good report ili wapewe loan
   
 2. I

  Iron-rock Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli unaku....!
  Kama kila kitu kina VAT na ni nchi inayo ongoza kwa kutoza kodi duniani,na peke inayo samehe kodi ya makampuni ya kiuwekezaji!.
  kwanini usikue...!
  We imagine hapa loliondo vijijini sukari kg1 inauzwa 2400 sindo kukua kwa uchumi huko! Au sio?...!
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  na bado wanapeana tu hizo point za uchumi kukuwa ili khali ni matatizo makubwa...
   
 4. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  hii rate ya ukuaji ni ya juu mno, ni kama Waziri mkuu aliyejiuzulu Mh. Dr. Edward Lowassa alivyosema kuwa kwa takwimu za serukari tuna uwezo wa kujenga upya reli ya kati na kukarabati bandari zote wenyewe lakini yote yanasomeka kwenye makaratasi tu. Na sio rahisi kujustify kilichopaisha uchumi hivyo!
  Nadhani location ya research ya WB ilikuwa Masaki na Tegeta beach na shopping walienda Shoppers Plaza na Mlimani City.
   
 5. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  wanatuchezesha sindimba....na kama tunacheza, kwa nini wasiendelee kutuchezesha? Si tunakopa na kulipa, shida iko wapi?...wenzenu wana vijisenti nje....wazungu hawaelewi kama kuna sehemu tanzania watu wanaishi hakuna umeme kabisa, wanadhani ni hifadhi za taifa.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Aaaah,hiyo bei mbona inatisha sana?????
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hahahahaaaaaa........mdau wewe upo kwenye sekta ya UTALII????
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nahisi hawa wanapelekewa ripoti za kupikwa
   
 9. u

  ureni JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Unajua kwa tajiri yeyote ambaye amekuona wewe masikini unakitu kizuri na anahitaji kukunyonya lazima akusifu,manake wewe unampa madini bure,unamwita aje kuwekeza anakuja bila hata sumni unampa eneo lenye hati ili awekeze anaenda kwenye benki zenu anatumia ile hati uliyompa anakopa hela anazitumia kuwekeza,kujengea kiwanda anapewa msamaha wa kodi miaka 5,anabadilisha jina la kiwanda chake anapata miaka 5 tena ya bure bila kulipa kodi,kwa nini asikupige danganya toto ili uendelee kumjengea mazingira ya kuendelea
   
 10. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya mashirika yanatumiwa na mataifa makubwa kuweka mazingira muafaka katika nchi zinazoendelea ya kuwezesha makapuni makubwa ya nchi hizo kuhamisha rasilimali zetu kwa bei ya kutupwa. Hii ndiyo maana mashirika hayo huwa yanatuvisha kilemba cha ukoka. Chukua mfano wa mabilioni ya mikopo ambayo mashirika hayo yamekuwa yanamimina nchini mwetu eti kwaajili ya maboresho ya utumishi wa umma, yametoa matunda gani! Sana sana maudhi, hata hivyo mashirika hayo yako kimya kama kwamba hayajui kinachoendelea.
   
Loading...