Mahandeiboho
Member
- Dec 27, 2016
- 94
- 43
Tunaona ajira za vijana waliohitimu vyuo mbalimbali zinapatikana kwa shida. Kujiajiri kunataka mtaji ambao haupo kwa kila anayetaka. Fedha mfukoni hamna. Chakula hakitoshi, bei ya sembe inapanda watu wanashindia maembe. Mabenki yana hali ngumu. Watumishi wa uma hawana furaha na ajira zao. Mvua hakuna na haitabiriki inakuja lini na kiasi gani. Mifugo imeanza kufa maeneo ya wafugaji. Nyama dukani inachukua siku mbili hadi tatu kumaliza ngombe mmoja aliyechinjwa. Tumekosea wapi na jawabu ni nini.