Uchumi wa Nchi unapodorora kama huu wa Tanzania, lawama ziende kwa Rais au Waziri wa Fedha?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,503
217,762
Sasa ni dhahiri kwamba maisha ya Watanzania yamekuwa magumu kuliko awamu zote zilizopita , familia nyingi sasa zinakula mlo mmoja tu, huku Maharage yakiwa Chakula Muhimu kabisa.

Ni kweli kwamba Mambo ya Utekaji, kuokota viroba vya maiti baharini na kwingineko na ubambikaji kesi za uongo, zilizoitwa za uhujumu uchumi na Utakatishaji fedha kwa sasa yamepungua (Hayajaisha), lakini maisha ya Raia yamekuwa kizungumkuti, hali ni mbaya mno! Mzunguko wa pesa ni kama hakuna , watu wamekuwa masikini mno ! Chakula Kikuu kimekuwa Mihogo na Maharage.

Hata sisi tuliobarikiwa kidogo ni kama tuko matatani, tunapigwa mno mizinga na wenye uhitaji kuliko kipindi chochote kile, shida ya nchi hii ni nini?

Sasa katika hali kama hii ya sasa nchini Tanzania ni Nani alaumiwe, ni Rais wa Nchi au Waziri wa Fedha?
 
Sasa ni dhahiri kwamba maisha ya Watanzania yamekuwa magumu kuliko awamu zote zilizopita , familia nyingi sasa zinakula mlo mmoja tu , huku Maharage yakiwa Chakula Muhimu kabisa .

Ni kweli kwamba Mambo ya Utekaji , kuokota viroba vya maiti baharini na kwingineko na ubambikaji kesi za uongo , zilizoitwa za uhujumu uchumi na Utakatishaji fedha kwa sasa yamepungua (Hayajaisha) , lakini maisha ya Raia yamekuwa kizungumkuti , hali ni mbaya mno ! Mzunguko wa pesa ni kama hakuna , watu wamekuwa masikini mno ! Chakula Kikuu kimekuwa Mihogo na Maharage .

Hata sisi tuliobarikiwa kidogo ni kama tuko matatani , tunapigwa mno mizinga na wenye uhitaji kuliko kipindi chochote kile , shida ya nchi hii ni nini ?

Sasa katika hali kama hii ya sasa nchini Tanzania ni Nani alaumiwe , Ni Rais wa Nchi au Waziri wa Fedha ?
Mi nafikiri haya ni matokeo tu ya alivyovurunda Magufuli.

Tena afadhali M'Mungu alituondolea mapema mana kama angeendelea kuwepo basi hali ingekuwa ni mbaya zaidi...
 
Back
Top Bottom