Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Siyo siri, Maraisi hawa walipokabidhiwa nchi zao zikiwa hoi kiuchumi. Lakini kwa kuruhusu mijadala ya wazi nini kifanyike,walishinda majaribu. Hatimaye,uchumi wa nchi na watu wao ukaimarika bila kubanana au kulalamikia watangulizi wao. Mikakati yao ilishirikisha hata watangulizi wao wanaosadikika kuharibu uchumi. Tulishudia Obama na Bush wakija Tanzania katika ndege moja kusaka miradi ya kiuchumi. Tumeshuhudia "Sulivan Summit" wakiwepo kina Comrade Andrew Young wakija Arusha kujadili nasi,namna ya kujiwezesha uchumi wetu sisi weusi ukue. Tumeshuhudia wanaharakati wengi wa masuala ya kijamii na kisiasa katika enzi za maraisi hao zikiwa active kujadili,kushauri na kupingana kwa hoja,hadi muafaka kupatikana katika hali ya amani. Mfano,ni ule mpango kabambe wa kupunguza gharama za afya (Obamacare) kwa watu wa kipato cha chini na kati ambao hata Raisi Trump imebidi aridhie japo hakutaka.
Kwa maoni yangu, na kwa mtizamo wa dunia ya sasa, mijadala,makongamano,ushirikishwaji wa taasisi na wachumi mbalimbali ni jambo zuri katika kuweka mustakabali imara wa ukuzaji uchumi.
Kwa maoni yangu, na kwa mtizamo wa dunia ya sasa, mijadala,makongamano,ushirikishwaji wa taasisi na wachumi mbalimbali ni jambo zuri katika kuweka mustakabali imara wa ukuzaji uchumi.