Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer

Business restructuring, kulikuwa na hela chafu zisizokuwa na tija mtaani- hizi zimepotea na madhara yake pengine ndiyo haya. Kufungwa kwa biashara zipo sababu nyingi maana hata kipindi kile unachodhani hali ilikuwa salama pia biashara zilikuwa zinafungwa na biashara mpya zinafunguliwa.
Una maanaa hizo biashara mpya ndio hivyo viwanda vipyaa 4000 viliojengwa na cha ajabu aliosimamia viwanda kujengwa nae kakosa kazi Mwijage !!??
 
Sasa ndugu yangu kwa hali ilivyo sasa nani atanunua hao kuku wetu au njiwa? hali mbaya kaka kuliko maelezo
 
Pandikizi limetumwa kuvuruga
Naam, naona akili zimeanza kuwajia sasa. Huyu Nduli hafai kabisa kuongoza nchi, ni afadhali hata ya Membe. Kwa bahati mbaya sana kwasasa hamna cha kufanya. Huyu ataendelea kutawala kwa MABAVU huku Tanzania ikiendelea kuvurugika.
 
Anachuki na waisrael umeona alivowabomolea kimara
Ninamshauri jiwe...awaweke waisraeli wa Tanzania kwenye serikali yake atabadilisha uchumi haraka sana...wale ni watu wanajua uchumi na biashara...weka mmoja waziri wa fedha na mwingine waziri wa biashara...utaona utakavyokubalika kwamba umejenga uchumi mzuri..."ni ushauri tu..ila ni muhimu sana...rejea uchumi wakati wa Mkapa"
 
Yeye amesema anapigania Wanyonge, sasa kama haupo kundi la Wanyonge pole.

Sasa inatakiwa utoke ulipokuwa mpaka uwe Mnyonge ndio utafaidi hii awamu.
Ndio hii style wafanyabiashara wamefunga maduka .wanauza kama wanyonge machinga sasaaa .okeee
 
LAKINI Umejitahidi sana leo kuandika japo kwa kuficha ficha hapo kwenye hitimisho.

Lbda kwa sababu na wewe umeumizwa.

Hivi Paskali Nini Tatizo.

Ni huyu Dereva wetu hana leseni ya Veta mbona tunayumba?

Kuna haja gani uchumi kukua kwa 7+ huku watu wanakufa kwa njaa na shida na maangaiko.


SASA kwa sababu na wewe umesema ukweli leo. Nimeamini kuna shida kubwa sana hata mkuu anashindwa kuicontrol.

Mkuu Kodi kodi kodi Inaendana na mazingira mazuri kwa wafanya biashara wakubwa kwa wadogo.

SASA kila mtu akifunga biashara yake utapata wapi kodi.

Leo hii Mkuu Rais kila pesa inaingia BOT na kila malipo yanatoka BOT, Mkuu haya mabanki yanayotukopesha sisi watafanyeje biashara?

Kumbuka katika nchi zote Source ya Pesa (flow) Inaanzia serikalini na kwenda kwenye mabenki sasa kama wewe umefunga mifereji yote ya uchumi kwa watu wa chini na wafanyabiashara uchumi utakuaje utakuaje?.

SASA ninaanza kumuelewa Zitto Kabwe kwamba huenda hizi takwimu za uchumi kukua zinapigwa madesa aka zinapikwa ili kumfurahisha Rais lakini ukweli si huo.
 
Kabudi anamwambia Jiwe bana hapo hapo watu wafanye kazi huku yeye anakula goodtime

Nilicho kigundua kwa jiwe akiona watu wanalilia hivi huwa anaenjoy kinoma
Ni hulka ya masychopath duniani kote watu kama Idd Amin , Mobutu , Joseph Stallin n.k , kiufupi rais Magufuli ni mental disorder kama za hawa madikteta
 
Pole sana Paskali, pole watanzania wenzangu, kwa msiba huu wa kiuchumi, kisiasa na kijamii tulionao, na ambao matanga yake yataendelea kwa miaka miwili zaidi. inawezekana Magufuli, kutokana na kuombewa anakoombewa, akawaonea huruma watanzania na kujiondoa kwenye kinyang'anyiro, na kuwaachia wengine miaka mitano ijayo, maana yeye hana uwezo wa kutuondolea msiba huu. Na kwa nchi yetu ilivyo, ni vigumu sana kumtoa rais ambaye hataki kutoka, mwenye mavyombo kibao na hakuna institutions za kubalance. Lakini kama akiendelea, basi matanga yataendelea, tutaendelea kuomboleza kwa miaka minane ijayo. Sasa hapo sijui itakuwaje, maana hata samaki wa baharini, tembo wa Selous, Simba wa Serengeti na Sokwe wa kule Kigoma, wote wataisoma namba. Nadhani CCM hawatarudia kosa kama hili asilani.
 
Wanabodi
Kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania ya Magufuli, ambayo umekuwa ukikua kwa asilimia zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ukuaji huu is not reflected kwa Watanzania wa hali ya chini ambao ndio walio wengi, tunaelezwa uchumi unakuwa, na ripoti ya juzi juzi ya UNDP inaeleza kiwango cha umasikini kinapungua Ripoti: Kiwango cha umasikini kinapungua kwa kasi - JamiiForums lakini hali za maisha kwa walio wengi, zinazidi kuwa ngumu siku hadi siku, uchumi wa taifa unakuwa, huku uchumi wa watu individual na sekta binafsi ukizidi kuporomoka ambapo sekta binafsi ambayo ndio inategemewa kuwa the drivers we uchumi wa nchi ikiwemo Tanzania ya viwanda, ndio mhanga mkuu wa mdororo wa uchumi na ndiye anaye suffer the most.

Kwa upande wa maendeleo, ni kweli nchi yetu inapiga hatua kubwa za maendeleo, majengo, miundombinu, mabarabara, flyovers, viwanda, midege mikubwa, SGR, Stigler Gorge etc, lakini haya yote ni maendeleo ya vitu na sio maendeleo ya watu.

Je, Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?-

Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?. - JamiiForums

Tena msije kusema kuwa tulinyamaza, Sisi jf tumesema sana, tumeuliza sana humu

Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT - JamiiForums

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi? - JamiiForums

Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Kwa sasa naona kama sisi sekta binafsi tuna suffer. Ku suffer huko kulianzia kufungwa kwa maduka makubwa ya bidhaa na supermarkets. Zilianza super markets za Shoprite, zikaja Uchumi, piteni maeneo ya Shoppers Plaza mshuhudie frames tupu wenyewe wamefungasha. Hata mtaa wa Samora lile jengo jipya la NHC mtaa wa Samora, lilikuwa full, sasa kuna mapengo.
Kuzorota uchumi: Stone Block wafungasha virago! - JamiiForums

Yakafuata baadhi ya mashirika na makampuni kufilisika hivyo kupunguza wafanyakazi,Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Yakaja mabenki. na sasa ni maduka ya fedha.

Wakati yote haya yakitokea, sisi media hatukuyaangazia vya kutosha kwa kudhani hayatuhusu!.

Sasa kibano hicho cha hali ngumu ya uchumi, kimeigusa sekta ya Media ambapo media kubwa kabisa nchini zimeanza kutikisika.

Kwenye media ilianza Star TV, kati ya wafanyakazi 500, ililazimika kupunguza wafanyakazi 100, mwaka 2016 wakabaki 400, mwaka jana wakapunguza 200 wakabaki 200, sijui mwaka huu, lakini kipindi chake most popular cha Jicho letu ndani ya habari, kinachoendeshwa na Mkongwe Dotto Bulendu, hakipo hewani!
Star Tv na Redio Free kupunguza wafanyakazi - JamiiForums

Leo kumepatikana taarifa ya wafanyakazi wa gazeti kubwa la the Guardian, hawajalipwa mishahara kwa miezi 3, hivyo kitakachofuata ni kupunguza wafanyakazi.Mti wa Xmas wazua simanzi kwa wafanyakazi wa The Guardian Limited - JamiiForums

Japo familia ya the Citizen Mwananchi, bado hawajatangaza kulia njaa, lakini kama hii ndio hali halisi ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, then hata Citizens, litakuwa halina jinsi, lazima nalo soon litatangaza kupunguza wafanyakazi.

Mimi mwenyewe na kale kajikampuni kangu ka PPR, ambapo tulibamba sana tenda za serikali, mwanzo tulikuwa na wafanyakazi 20, tukipangisha jengo la NHC pale Mtaa wa Mkwepu kwa kodi ya pango kwa mwezi, ya zaidi ya mshahara wa DC, sasa hakuna tena tenders za serikali, serikali inatangaza moja kwa moja na TBC, mwaka huu pia tenda zangu za kutangaza Maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane zimefutwa, hivyo tumepunguza wafanyakazi 15!, tumebaki 5!. Na Mtaa wa Mkwepu hapakaliki hivyo tumehama, tumehamia jengo la Posta House kwenye kajichumba.

Wito kwa waandishi wenzangu, walioajiriwa kwenye media industry, kwa hali hii ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, usitegemee ajira pekee na usisubiri kupunguzwa kazi, bali sasa kwa sisi wanaume tufuge kuku na njiwa, na Kwa waandishi wa kike ni mambo ya ndoo na kidumu.

Kwa sisi wanaume, kuku ni kazi ya kujiajiri) na njiwa (kazi ya kuajiriwa), ili njiwa akiruka, ubaki na kuku.

Kwa waandishi wa kike, kwenye kazi ya kuteka maji, teka maji kwenye ndoo (kazi ya kudumu) na kidumu (kujiajiri), ili maji ya kwenye ndoo yakimwagika, angalau unabaki na kidumu.

Kiukweli kabisa Media tuna hali ngumu!.
Mungu saidia.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki rais Magufuli aweze kukuza uchumi wa nchi yetu kwa Tanzania ya viwanda kifanikiwa, tuwe nchi ya uchumi wa kati, tukielekea kuwa nchi ya ahadi kwa mabomba nchi mzima yatatoa maziwa na asali
Jumatano Njema.
Paskali


Upo sahihi sana paschal Mayalla...
Watanzania tuna tabia mbaya sana ya kujigeuza watazamaji katika mambo yasiyotuhusu pasi na kujiuliza kuhusu kesho yetu.
Ukiwalaumu waandishi wa habari mimi nitakuambia kuwa hata wao kuna wanaowatazama tu wadhani hawataguswa na janga la mdororo wa uchumi.
Umoja wa Tanzania unahubiriwa majukwaani tu na kwenye majarida ila uhalisia haupo ndio maana utakuta huyu CCM yule CUF na mwengine CHADEMA, kwenye majukwaa ya kampeni utasikia hawa wakaskazini wale wamagharibi, Elimu na ajira utasikia hawa wakristu wale waislamu yaani hakuna umoja kabisa Tanzania zaidi ya kuishi pamoja.
Jambo la msingi ni kila mtu astuke na ajipange kwani hata taasisi zinazotegemea mgao wa serikali kama shule n.k nazo zinalia.
 
Kuna kitu ambacho Watanzania wengi hatukijui kwenye ulimwengu wa Kibepari; kwa ufupi kazi kama hizo za kuandaa matangazo nk huko ulikozaliwa ubepari kampuni kama za kina Pascal Mayala na ile Benchmark ya yule mama wa BSS ndio hufanya hizo kazi. Uliisha wahi jiuliza kwanini Bill Gates hatengenezi computer but all computer factories/industries huchukua software kwake!? Tuache ushamba, dunia ndio inavyo kwenda, hata hili linalo sifiwa leo, halina future, soon tutarudi kule kule.
Nadharia yako haiendani na hili swali. Hapa kuna corruption na kule kuna specialization. Vitu viwili tofauti. NB: Ufahamu: mimi sipingi kampuni binafsi kufanya kazi na serikali. Napinga kampuni zilizoundwa kijanja janja ili ku-tape fedha za serikali kwa kazi ambazo hazina umuhimu
 
Back
Top Bottom