Ngushi
JF-Expert Member
- Jul 8, 2016
- 9,066
- 18,348
Kuna mtu niliona anasema Huyu Mzee ni msanii sana nikajua ana chuki Binafsi ila baada ya kufikiri vizuri naanza kuamini kama Mzee ameamua kula na kipofuPascal Mayalla majuzi nilimsikia Mzee mengi akitangaza kuleta wawekezaji na kuanza kazi ya kuunda magari Tanzania. Amesema wataanza mwezi March 2019.
Pia majuma mawili yaliyopita pia alionekana akisaini makubaliano ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza Smartphones nchini.
Huku Guardian moja ya magazeti ya Mzee Mengi yakiwa hayajalipa wafanya kazi wake mshahara kwa mwezi wa 3 !
Ama kuhusu Smartphone , Kampuni ya Huawei , moja ya Kampuni kubwa za mawasiliano duniani walikuja mwisho wa mwa utawala wa Kikwete na kuanza program kabambe ya kutengeneza simu zao hapa nchini. Ulikua ni mradi mkubwa sana ..Huawei wamekua frustrated na wamefunga virago mwishoni mwa mwaka jana.
Hivo haya ya Mengi na biwanda vipya ni kujibanza uzeeni kujinusuru na Jiwe.