Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer

Pascal Mayalla majuzi nilimsikia Mzee mengi akitangaza kuleta wawekezaji na kuanza kazi ya kuunda magari Tanzania. Amesema wataanza mwezi March 2019.
Pia majuma mawili yaliyopita pia alionekana akisaini makubaliano ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza Smartphones nchini.
Huku Guardian moja ya magazeti ya Mzee Mengi yakiwa hayajalipa wafanya kazi wake mshahara kwa mwezi wa 3 !
Ama kuhusu Smartphone , Kampuni ya Huawei , moja ya Kampuni kubwa za mawasiliano duniani walikuja mwisho wa mwa utawala wa Kikwete na kuanza program kabambe ya kutengeneza simu zao hapa nchini. Ulikua ni mradi mkubwa sana ..Huawei wamekua frustrated na wamefunga virago mwishoni mwa mwaka jana.
Hivo haya ya Mengi na biwanda vipya ni kujibanza uzeeni kujinusuru na Jiwe.
Kuna mtu niliona anasema Huyu Mzee ni msanii sana nikajua ana chuki Binafsi ila baada ya kufikiri vizuri naanza kuamini kama Mzee ameamua kula na kipofu
 
Hayo marekebisho yataisha lini? Halafu hii dhana ya kusema tulikuwa na uchumi wa wauza unga haiko sawa ni serikali kujaribu kukwepa majukumu
Serikali inarekebisha misingi ya uchumi wa nchi kuwa sustainable. Nchi ilendeshwa kwa pesa za wauza unga na watakatishaji pesa chafu kwa muda mrefu. The economy wa skewed. Uzalishaji halisi (manufacturing, extraction and construction industries) haukuwa unafanyika ipaswavyo. Private sector practitioners wengi walihamia kwenye services (public procurement) kupiga pesa za serikali na mashirika ya umma. Kwa hiyo, kwa sasa private sector wanapaswa kuwa dynamic and resilient. Katika kipindi hiki ni kweli kuna sectors zinata-suffer sana ila baada ya marekebisho zitatoka triumphantly. Nothing is done without cost.
 
Watanzania wanapitia magumu zaidi..
Broo pale bandari kuna maelfu waliokuwa wameajiriwa na kampuni za CLEARING AND FORWARDING sasa hivi wapo kijiweni wanapiga miayo..
Leo TRA hapa kitaa wamemkaba dogo mmoja mwenye kisaluni cha kunyoa..
Kwa siku ananyoaga wastani wa mtu mmoja kwa buku..
TRA wamemforce akakate leseni..
hahaaaa haaa !
pesa atoe wapi ?
hahaha...nimecheka ingawa sio mazuri....hao TRA si wameambiwa waache kumchonganisha mtawala na watawaliwa?? hawana adabu hao eeh..hahahahhaa

Na akipata leseni anatakiwa alipie na EFD machine...ambayo umeme tuu wa kuioperate unazidi hayo mapato ya huyo kijana kwa wastani wa siku...na akifunga biashara sasa , anaitwa mpiga dili
 
Cocochanel naona na wewe vyuma vimekaza au buku 7 pale Lumumba haitoki kwa wakati?

Kwa jinsi nilivyo humu na mnaninotiii na kupenda kunisoma.. na kupokea nayoandika kwa mikono miwili😃

Basi ningekuwa kwenye figa za juu sana tena kwa posti.. kama ningekuwa napokea pesa kutoka kwao.

Muache kunionea wivu.. mimi ni Magufuli oyeeee

Nikijiunga nao naamini wote mtanifata maana nitawapa nondo tamu haswaaa hata Magufuli 2020 mtampigia kura huku mkilia kwa furaha

Niambie najiungaje na CCM.. maana waliopo humo wengine wanaogopa kuona najiunga nao wakijua nitawapita kwa mengi na kuweka mambo vizuri... eeeeeeeh nacheka mie.. Cocochanel najipenda jamani
 
Wanabodi
Kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania ya Magufuli, ambayo umekuwa ukikua kwa asilimia zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ukuaji huu is not reflected kwa Watanzania wa hali ya chini ambao ndio walio wengi, tunaelezwa uchumi unakuwa, na ripoti ya juzi juzi ya UNDP inaeleza kiwango cha umasikini kinapungua Ripoti: Kiwango cha umasikini kinapungua kwa kasi - JamiiForums lakini hali za maisha kwa walio wengi, zinazidi kuwa ngumu siku hadi siku, uchumi wa taifa unakuwa, huku uchumi wa watu individual na sekta binafsi ukizidi kuporomoka ambapo sekta binafsi ambayo ndio inategemewa kuwa the drivers we uchumi wa nchi ikiwemo Tanzania ya viwanda, ndio mhanga mkuu wa mdororo wa uchumi na ndiye anaye suffer the most.

Kwa upande wa maendeleo, ni kweli nchi yetu inapiga hatua kubwa za maendeleo, majengo, miundombinu, mabarabara, flyovers, viwanda, midege mikubwa, SGR, Stigler Gorge etc, lakini haya yote ni maendeleo ya vitu na sio maendeleo ya watu.

Je, Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?-

Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?. - JamiiForums

Tena msije kusema kuwa tulinyamaza, Sisi jf tumesema sana, tumeuliza sana humu

Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT - JamiiForums

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi? - JamiiForums

Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Kwa sasa naona kama sisi sekta binafsi tuna suffer. Ku suffer huko kulianzia kufungwa kwa maduka makubwa ya bidhaa na supermarkets. Zilianza super markets za Shoprite, zikaja Uchumi, piteni maeneo ya Shoppers Plaza mshuhudie frames tupu wenyewe wamefungasha. Hata mtaa wa Samora lile jengo jipya la NHC mtaa wa Samora, lilikuwa full, sasa kuna mapengo.
Kuzorota uchumi: Stone Block wafungasha virago! - JamiiForums

Yakafuata baadhi ya mashirika na makampuni kufilisika hivyo kupunguza wafanyakazi,Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Yakaja mabenki. na sasa ni maduka ya fedha.

Wakati yote haya yakitokea, sisi media hatukuyaangazia vya kutosha kwa kudhani hayatuhusu!.

Sasa kibano hicho cha hali ngumu ya uchumi, kimeigusa sekta ya Media ambapo media kubwa kabisa nchini zimeanza kutikisika.

Kwenye media ilianza Star TV, kati ya wafanyakazi 500, ililazimika kupunguza wafanyakazi 100, mwaka 2016 wakabaki 400, mwaka jana wakapunguza 200 wakabaki 200, sijui mwaka huu, lakini kipindi chake most popular cha Jicho letu ndani ya habari, kinachoendeshwa na Mkongwe Dotto Bulendu, hakipo hewani!
Star Tv na Redio Free kupunguza wafanyakazi - JamiiForums

Leo kumepatikana taarifa ya wafanyakazi wa gazeti kubwa la the Guardian, hawajalipwa mishahara kwa miezi 3, hivyo kitakachofuata ni kupunguza wafanyakazi.Mti wa Xmas wazua simanzi kwa wafanyakazi wa The Guardian Limited - JamiiForums

Japo familia ya the Citizen Mwananchi, bado hawajatangaza kulia njaa, lakini kama hii ndio hali halisi ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, then hata Citizens, litakuwa halina jinsi, lazima nalo soon litatangaza kupunguza wafanyakazi.

Mimi mwenyewe na kale kajikampuni kangu ka PPR, ambapo tulibamba sana tenda za serikali, mwanzo tulikuwa na wafanyakazi 20, tukipangisha jengo la NHC pale Mtaa wa Mkwepu kwa kodi ya pango kwa mwezi, ya zaidi ya mshahara wa DC, sasa hakuna tena tenders za serikali, serikali inatangaza moja kwa moja na TBC, mwaka huu pia tenda zangu za kutangaza Maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane zimefutwa, hivyo tumepunguza wafanyakazi 15!, tumebaki 5!. Na Mtaa wa Mkwepu hapakaliki hivyo tumehama, tumehamia jengo la Posta House kwenye kajichumba.

Wito kwa waandishi wenzangu, walioajiriwa kwenye media industry, kwa hali hii ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, usitegemee ajira pekee na usisubiri kupunguzwa kazi, bali sasa kwa sisi wanaume tufuge kuku na njiwa, na Kwa waandishi wa kike ni mambo ya ndoo na kidumu.

Kwa sisi wanaume, kuku ni kazi ya kujiajiri) na njiwa (kazi ya kuajiriwa), ili njiwa akiruka, ubaki na kuku.

Kwa waandishi wa kike, kwenye kazi ya kuteka maji, teka maji kwenye ndoo (kazi ya kudumu) na kidumu (kujiajiri), ili maji ya kwenye ndoo yakimwagika, angalau unabaki na kidumu.

Kiukweli kabisa Media tuna hali ngumu!.
Mungu saidia.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki rais Magufuli aweze kukuza uchumi wa nchi yetu kwa Tanzania ya viwanda kifanikiwa, tuwe nchi ya uchumi wa kati, tukielekea kuwa nchi ya ahadi kwa mabomba nchi mzima yatatoa maziwa na asali
Jumatano Njema.
Paskali
Pole sana ndugu yangu Pascal Mayala. Lakini pongezi pia kwa kuwasemea wenzako. Kusema kweli media industry ime shake vya kutosha. Sikuamini siku nilipoona yale maandamano dhidi ya mmiliki wa Sahara media bwana Antony Diallo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza.
Kwa jinsi alivyoibeba CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 hakustahili kuwa alivyo kwa sasa.
Kile kipindi cha Jicho Letu ndani ya Habari nilikipenda sana. Na Dotto Bulendu alikitendea sana haki.

Alikuwa akiwaalika bwana Mathew na mwenzie Odero Odero panachimbika.

Siku hizi Star TV hata uwezo wa kuandaa vipindi imekuwa shida sana. Watangazaji mahili kama akina Ivona Kamuntu, Nyamwihura, Fredwaa na wengine kibao wamehamia kwingine kukimbia njaa.

Tuombe Mungu media houses nyingine zisikumbwe na matatizo hayo.
 
Zile bilioni 600 za korosho fedha za kigeni tulizozikosa ndio zinatuumiza namna hii, hizo korosho uzeni tu hatwa 2,000/= kwa kilo yaishe angalau fadha za kigen ziingie, kwani mikorosho si ipo itazaa tena? Shida iko wapi?
 
Reflection ya kukua kwa uchumi wa mwananchi itaanza kuoneka 2020 miradi mikubwa itakapokua imeanza
Si jambo la mchezo kufika Mwanza baada ya masaa manne Pasco,ama kuhusu media ku suffer hili linachangiwa sana na utandawazi hasa ukuaji wa IT wa kulaumiwa sio Magufuli ni teknolojia
Mwanza kwa masaa manne unafikaje mkuu....
Labda utajibu SRG ikikamilika...
Basi twende na data,SRG inayojengwa Tanzania installed capacity yake in term of speed Ni 140KPH..
Urefu/umbali ya SRG hiyo kutoka dar hadi mwanza itakuwa Ni zaidi ya KM 1600...
Kwa hiyo treni inakayo kimbia kwa speed kubwa ya mwisho ya uwezo wa reli 140kpm(kitu ambacho Ni unlikely and dangerous) na bila kusimama kwenye kituo chochote njia nzima (non stop) itatumia masaa 11 kufika mwanza...
Sasa sijui wewe hayo masaa manne umeyapata vipi.....

Logically na Mathematically SRG hii itakuwa treni inatumia 20 hours from dar to mwanza.....
 
Kwani Paskali biashara/shughuli za media ni za ujanja ujanja?

Maana shughuli zinazoendeshwa kwa ujanja ujanja ndizo tulihakikishiwa zitapotea kabisa...
 
Mwanza kwa masaa manne unafikaje mkuu....
Labda utajibu SRG ikikamilika...
Basi twende na data,SRG inayojengwa Tanzania installed capacity yake in term of speed Ni 140KPH..
Urefu/umbali ya SRG hiyo kutoka dar hadi mwanza itakuwa Ni zaidi ya KM 1600...
Kwa hiyo treni inakayo kimbia kwa speed kubwa ya mwisho ya uwezo wa reli 140kpm(kitu ambacho Ni unlikely and dangerous) na bila kusimama kwenye kituo chochote njia nzima (non stop) itatumia masaa 11 kufika mwanza...
Sasa sijui wewe hayo masaa manne umeyapata vipi.....

Logically na Mathematically SRG hii itakuwa treni inatumia 20 hours from dar to mwanza.....
ACHA KUTUMIWA NA MABEBERU,UNGA MKONO JUHUDI ZA JIWE HATA UKIAMBIWA ITATUMIA 15 MINUTES WEWE SEMA NDIYO,MZEE ANALALA NA MAFAILI KITANDANI UNADHANI MCHEZO?
 
Nikionaga thread yako ama comment yako napatwa na kichefu chefu... Nimeikalili tu hiyo avatar yako... Ni miongoni mwa watu wabinafsi sanaa wasio na utu...

Ni muimbaji mzuri wa pambio za kusifu na kuabudu huna utu kama wanamke uko radhi watu wafe na njaa... Ila mtu mmoja apewe sifa zisizo stahili...

Hali ya uchumi ni mbaya sanaa tax n fiscal policy zimefanya kudorora kwa kila kitu...

Dada jaribu kubadilika kwakweli penye fact tema fact.... Naumia Sanaa kuona unapindishaga mambo kwa makusudi
Hawa mabinti sijui wanamatatizo gani # ISIS # mudawote # Coco Chanel, wananitia kinyaa sana
 
[QUHaihi"Pascal Mayalla, post: 29491819, member: 17813"]Wanabodi
Kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania ya Magufuli, ambayo umekuwa ukikua kwa asilimia zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ukuaji huu is not reflected kwa Watanzania wa hali ya chini ambao ndio walio wengi, tunaelezwa uchumi unakuwa, na ripoti ya juzi juzi ya UNDP inaeleza kiwango cha umasikini kinapungua Ripoti: Kiwango cha umasikini kinapungua kwa kasi - JamiiForums lakini hali za maisha kwa walio wengi, zinazidi kuwa ngumu siku hadi siku, uchumi wa taifa unakuwa, huku uchumi wa watu individual na sekta binafsi ukizidi kuporomoka ambapo sekta binafsi ambayo ndio inategemewa kuwa the drivers we uchumi wa nchi ikiwemo Tanzania ya viwanda, ndio mhanga mkuu wa mdororo wa uchumi na ndiye anaye suffer the most.

Kwa upande wa maendeleo, ni kweli nchi yetu inapiga hatua kubwa za maendeleo, majengo, miundombinu, mabarabara, flyovers, viwanda, midege mikubwa, SGR, Stigler Gorge etc, lakini haya yote ni maendeleo ya vitu na sio maendeleo ya watu.

Je, Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?-

Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?. - JamiiForums

Tena msije kusema kuwa tulinyamaza, Sisi jf tumesema sana, tumeuliza sana humu

Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT - JamiiForums

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi? - JamiiForums

Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Kwa sasa naona kama sisi sekta binafsi tuna suffer. Ku suffer huko kulianzia kufungwa kwa maduka makubwa ya bidhaa na supermarkets. Zilianza super markets za Shoprite, zikaja Uchumi, piteni maeneo ya Shoppers Plaza mshuhudie frames tupu wenyewe wamefungasha. Hata mtaa wa Samora lile jengo jipya la NHC mtaa wa Samora, lilikuwa full, sasa kuna mapengo.
Kuzorota uchumi: Stone Block wafungasha virago! - JamiiForums

Yakafuata baadhi ya mashirika na makampuni kufilisika hivyo kupunguza wafanyakazi,Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Yakaja mabenki. na sasa ni maduka ya fedha.

Wakati yote haya yakitokea, sisi media hatukuyaangazia vya kutosha kwa kudhani hayatuhusu!.

Sasa kibano hicho cha hali ngumu ya uchumi, kimeigusa sekta ya Media ambapo media kubwa kabisa nchini zimeanza kutikisika.

Kwenye media ilianza Star TV, kati ya wafanyakazi 500, ililazimika kupunguza wafanyakazi 100, mwaka 2016 wakabaki 400, mwaka jana wakapunguza 200 wakabaki 200, sijui mwaka huu, lakini kipindi chake most popular cha Jicho letu ndani ya habari, kinachoendeshwa na Mkongwe Dotto Bulendu, hakipo hewani!
Star Tv na Redio Free kupunguza wafanyakazi - JamiiForums

Leo kumepatikana taarifa ya wafanyakazi wa gazeti kubwa la the Guardian, hawajalipwa mishahara kwa miezi 3, hivyo kitakachofuata ni kupunguza wafanyakazi.Mti wa Xmas wazua simanzi kwa wafanyakazi wa The Guardian Limited - JamiiForums

Japo familia ya the Citizen Mwananchi, bado hawajatangaza kulia njaa, lakini kama hii ndio hali halisi ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, then hata Citizens, litakuwa halina jinsi, lazima nalo soon litatangaza kupunguza wafanyakazi.

Mimi mwenyewe na kale kajikampuni kangu ka PPR, ambapo tulibamba sana tenda za serikali, mwanzo tulikuwa na wafanyakazi 20, tukipangisha jengo la NHC pale Mtaa wa Mkwepu kwa kodi ya pango kwa mwezi, ya zaidi ya mshahara wa DC, sasa hakuna tena tenders za serikali, serikali inatangaza moja kwa moja na TBC, mwaka huu pia tenda zangu za kutangaza Maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane zimefutwa, hivyo tumepunguza wafanyakazi 15!, tumebaki 5!. Na Mtaa wa Mkwepu hapakaliki hivyo tumehama, tumehamia jengo la Posta House kwenye kajichumba.

Wito kwa waandishi wenzangu, walioajiriwa kwenye media industry, kwa hali hii ya uchumi wa Tanzania ya Magufuli, usitegemee ajira pekee na usisubiri kupunguzwa kazi, bali sasa kwa sisi wanaume tufuge kuku na njiwa, na Kwa waandishi wa kike ni mambo ya ndoo na kidumu.

Kwa sisi wanaume, kuku ni kazi ya kujiajiri) na njiwa (kazi ya kuajiriwa), ili njiwa akiruka, ubaki na kuku.

Kwa waandishi wa kike, kwenye kazi ya kuteka maji, teka maji kwenye ndoo (kazi ya kudumu) na kidumu (kujiajiri), ili maji ya kwenye ndoo yakimwagika, angalau unabaki na kidumu.

Kiukweli kabisa Media tuna hali ngumu!.
Mungu saidia.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki rais Magufuli aweze kukuza uchumi wa nchi yetu kwa Tanzania ya viwanda kifanikiwa, tuwe nchi ya uchumi wa kati, tukielekea kuwa nchi ya ahadi kwa mabomba nchi mzima yatatoa maziwa na asali
Jumatano Njema.
Paskali[/QUOTE]
Tatizo vyanzo vipya vya mapato vimekuwa siyo vile vya kuongeza fursa za ajira kwa watu wa kipato cha chini,bali wanaongezewa mzigo wa kodi huku ajira zikiwa zinapungua kwa mtu wa chini kutokana na matajiri wengi kufunga ama kupunguza wafanyakazi ktk biashara zao.Haihitaji kujuwa kwamba tunatembea ndani ya tope lenye kina cha zaidi ya mita moja.
 
Pascal,
Kuna siku nilipanda mabasi ya ................ Dar- Mwanza, dreva wa kwanza alikuwa anaendesha taratibu sana sababu kuna tairi mbili hazikuwa nzuri sana, abiria wakawa wakigomba na kulalamika kuwa watachelewa kufika. Tulipofika Dodoma, akapokea dreva mwingine wanaita (shift). Tulivyokaribia Singida tairi moja ikapasuka basi likaanza kuyumba huku na kule ikawa inakaribia kupinduka dreva akawa anajitahidi kuirudisha barabarani sasa unajua inavyokuwa, abiria waliokuwa upande huu, wanahamia huku, watu wanagongana hovyo kuna abiria walirushwa nje na kujipigiza kwenye lami na kufariki, wengine wakajeruhiwa sana, waliopo ndani ya gari wengine wakajibamiza kwenye vioo na kupasuka ovyo, wengine wakapata shinikizo la damu, wengine wengi wakawa vigilant na kutoka salama baada ya dreva kufanikiwa kulimiliki gari na kuliweka sawa barabarani.

Wakati dreva anahangaika kuliweka sawa, wengine walikuwa wanamtukana , wengine kumsifia, wengine kumponda dreva wa awali kuwa angekuwa yeye tungekula mzinga, wengine kumsifia dreva wa sasa kuwa ni masta. Nilichomsifia yule dreva alikuwa focused hasikilizi maneno ya abria anaangalia tu jinsi ya kuwaokoa. Baada ya kufanikiwa kusimamisha gari abiria wote kwa umoja wao wakaenda kumpongeza dreva kwa kuyaokoa maisha yao.
Wakahuzunika kwa wenzao waliotupwa nje, wakajisemesha kuwa laiti wangefunga mikanda ya viti (seat belt) wasingetupwa nje.
Najua umeamua kutumia fasihi kufikisha ujumbe ila kumbuka chief hii hali bado haijakugusa naamin ikikugusa IPO siku utayakumbuka maneno Yangu hata paskal hakuwah kuguswa moja kwa moja lakn Leo ameguswa maslah yake ameona atoe yake ya moyoni nipase tu kusema WALIO KARIBU NA MH RAIS WANAMUOGOPA KUMSHAURI SABABU TU YA MISIMAMO YAKE LAKN WAKUMBUKE NA WAO N TIMU MOJA LAWAMA HIZI HAWAZIKWEPI .... IPO SIKU ISIYO NA JINA YAJA KILA MTU ATALIPA KWA UDHALIMU HUU TUNAOFANYIWA
 
Hivi mnataka kubisha kuwa Tanzania haikuwa na biashara za ujanja janja? Zilikuwepo sana na mengi ya yanayotokea sasa hivi ni ripple effect ya uzembe uliofanywa nyuma rather than mapungufu ya serikali ya sasa. Mtu kama Pascal Mayalla hicho kikampuni chake ni moja ya vi-media house vilivyokuwa vinaendeshwa kwa njia za kijanja janja vikitegemea michongo kutoka serikalini na mashirika yake.
Kuna kitu ambacho Watanzania wengi hatukijui kwenye ulimwengu wa Kibepari; kwa ufupi kazi kama hizo za kuandaa matangazo nk huko ulikozaliwa ubepari kampuni kama za kina Pascal Mayala na ile Benchmark ya yule mama wa BSS ndio hufanya hizo kazi. Uliisha wahi jiuliza kwanini Bill Gates hatengenezi computer but all computer factories/industries huchukua software kwake!? Tuache ushamba, dunia ndio inavyo kwenda, hata hili linalo sifiwa leo, halina future, soon tutarudi kule kule.
 
Kama ilivo Nyerere kuishi kishetani hii ni part two,viongozi toka Kanda ya ziwa wanaanini ktk umasikini ndio uzalendo.
 
Pascal Umesahau nini !!?? Nukuu hii ya Kikwete kuhusu kukuta wafugaji wako choka mbaya kwa dhiki ili hali za mifugo imenawiri . Na kama unavyojua tena Msukuma na mifugo .ni kama unauliza jibu vile !!!
 
Back
Top Bottom