Uchumi wa Kikwete vs Uchumi wa Magufuli

FisadiKuu

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
8,167
13,443
Leo napenda niwakaribishe Economist na Bush Economist tujadili hali ya uchumi ya sasa tukilinganisha na hali iliyopita awamu ya JK.. Sio lazima uwe na uelewa mkubwa sana wa Uchumi ili uchangie hapa kuna vitu vingine ni nadharia ndogo ndogo tu tunazoziona huku mitaani..

JK alipochukua nchi mwaka 2005 alikuta hali si nzuri sana ingawa wakati wa Mzee Mkapa shillingi ilikuwa ina thamani nzuri sana. Wakati huo ilikuwa ni ngumu sana kukuta mwananchi wa kawaida au awaye yeyote akimiliki nyumba na wakiishi kwenye makazi mazuri na ya kisasa. Mikoa mingi hali ilikuwa si nzuri hasa kwenye suala la makazi, maji, umeme na barabara. JK ndani ya kipindi kifupi tu alifanya kazi na aliweza kubadilisha vitu vingi sana ndani ya muda mfupi tu. Miji ikaanza kupanuka, pesa ikaanza kupatikana kwa wananchi, biashara maelfu kwa maelfu zikafunguliwa na mambo mengi sana ambayo awamu ya Mkapa yalionekana ni anasa yalianza kufanywa na kuonekana ni mambo ya kawaida tu. Utitiri wa bank za biashara zilifunguliwa na miradi mikubwa mikubwa ilianza kufanywa na serikali kama vile barabara zilijengwa kuunganisha mikoa na pia mikopo ikaanza kutolewa kwa urahisi kwa wajasiriamali kutoka kwenye benki ya biashara. Kwa kifupi wakati wa JK kulikuwa na juhudi nyingi sana zilifanywa kukuza uchumi wa watu na si uchumi wa vitu pekee.

Kuna mambo kadha wa kadha ambayo yalifanya kipindi cha JK kuendelea kuwa bora na hata pesa kupatikana bila ya kuvuja jasho sana lakini bado uchumi ulikuwa kwa kasi. JK ametuacha uchumi ukikuwa kwa asilimia 7 ambao kimsingi ni wastani mzuri tu kwa nchi zinazoendelea. Fedha kipindi cha JK zilikuwa nje nje kwasababu ya mambo yafuatayo:

1. UFISADI MKUBWA NA RUSHWA
2. BIASHARA HARAMU (DAWA ZA KULEVYA)

Kimsingi mambo haya ndiyo yalifanya pesa kupatikana kwa urahisi sana awamu ya JK. Ilikuwa haishangazi kukuta vijana wadogo tu wakimiliki magari ya kifahari na wakiishi maisha ya anasa pasi ya kuwa na shughuli muhimu za kufanya, ilikuwa si kitu cha kushangaza kuona vijana wakiwa na Passports kitu ambacho awamu ya Mzee Mkapa ni vigogo na wafanyabiashara wakubwa tu na watoto wa matajiri ndio walikuwa na uwezo wa kumiliki Passports na kusafiri huko duniani. Kipindi cha JK ilikuwa ni kawaida kukuta kijana wa 19-30 akizunguka duniani mara SA, mara Dubai, mara China haikuwa inashangaza kabisa. Kimsingi hizi pesa chafu hasa hasa za madawa zilisababisha ukuaji mkubwa sana wa Uchumi wa mtu mmoja mmoja. Vijana wengi walifungua Boutique shops na Bureau de Change za kusafishia hizo pesa chafu. Bar zilikuwa zinajaa kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 usiku, magari yalikuwa yanabadilishwa kila kukicha, miji ilikuwa inakuwa kwa kasi sana. Kimsingi maisha ya JK yalikuwa ni leisure faire lakini tija ilikuja kuonekana kwa pato la nchi kukuwa kwa asilimia 7. Madawa haya mengi ambayo yalikuwa yanaleta fedha nyingi nchini hayakuwa yanatumika nchini bali Tanzania ilikuwa kama kituo tu na karibia 80% ya hayo madawa yalikuwa yanatoka kwenda nchi za Asia na kwingineko.

Kufupisha ili tusipoteze muda ni kwamba kipindi cha JK uchumi wa mtu mmoja mmoja ulikuwa mzuri na hakuna aliyekuwa analia njaa. Tulikuwa tunalia na ufisadi na madawa ambayo yalikuwa yanaangamiza nguvu kazi zetu.

Tukija kwenye awamu hii; tukianzia kwenye hotuba ya kwanza kabisa ya JPM pale Bungeni, aliyasema mengi sana ambayo kuna wengine tuliingiwa na moyo sana nae na hata tulianza kumuunga mkono. JPM aliichambua sana awamu ya JK na wengi tulichokiona ni kuwa kipindi cha JK hakuna kilichokuwa kinafanyika zaidi ya kujipotezea muda tu. Tukaingiwa na shauku kwamba sasa neema imekuja.. Tukaaminishwa nchi yetu haipaswi kuwa omba omba bali sisi ndio inatakiwa tutoe misaada, tukaamini na kupiga makofi.

Lakini kwa kipindi hiki kifupi tu tumejionea mengi sana, tulioaminishwa hatupaswi kuomba leo hii tumeshawaomba Morocco, Rwanda, Ethiopia na leo tumemwomba South Africa. Yaani sasa tunawaomba mpaka maskini wenzetu ambao tulipaswa sisi ndio tuwasaidie kwa ile speech yake ya kwanza kuitoa. JPM ndani ya mwaka wake mmoja tu aliingia na kiroja cha kuamishia fedha hazina ili awe anaitumia anavyojisikia.. Hii ilisababisha benki nyingi za biashara kuyumba, huduma ya mikopo kufungwa kwa kipindi kirefu hali iliyosababisha biashara nyingi kufilisiwa na mzoroto mkubwa wa uchumi ambao unaendelea mpaka sasa. Sasahivi vitu vingi vimerudi kuwa anasa, uchumi wa mtu mmoja mmoja uko taabani na biashara zinafungwa kila kukicha na ambao wanakomaa ni wanabaki tu kwenye Break Even ili angalau huko baadae hali ikirudi kuwa sawa awe ame maintain wateja wake.

Hali mbaya ya fedha mitaani imesababishwa na serikali kwanza kuzuia fedha chafu kuingia kwenye mzunguko kwa kupigana vita ya kuzuia biashara ya madawa lakini pia kuzuia deals zilizokuwa zinapigwa. Lakini walichojisahau ni kwamba wakati hayo yanafanywa serikali wangetakiwa angalau wapandishe mishahara, na wafanye miradi mingi mingi ili fedha ziwafikie wananchi. Sasahivi tunajione serikali inajipa tender yenyewe na fedha wanabaki nazo wenyewe bila ya kuwafikia wananchi ili kuleta tija. Kwa hali hii serikali inatakiwa ifanye kazi kutuokoa sie tulioko huku chini. US Government mara kadhaa imekuwa ikishutumiwa kushiriki kufanya biashara za madawa kati ya miaka ya 60's, 70's na 80's kwa kipitia shirika lake la kijasusi la CIA na walijipatia fedha nyingi tu ambazo zilikuwa zinaingizwa kwenye mzunguko na kuwasaidia wananchi.

Sasa pamoja kwa kumtukana JK lakini mambo hayakuwa mabaya hivi, na tuna maswali kadhaa ya kujiuliza. Je; TISS yawezekana iliruhusu makusudi biashara ya madawa kufanyika ili tujipatie fedha? Kwanini JK aliwajua na alikuwa na orodha na hata siku moja hawakuwahi kushtukia na kubughuziwa kama sasa?

Je; kama sasa tumeamua kupambana na hizo fedha chafu, kwanini usiwe wakati wa kudouble mishahara ili hali irudi kawaida huku mitaani? Kwanini sekta binafsi ambayo ndiyo kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wananyanyaswa na kuonekana waizi na wapiga dili?

Lakini swali kubwa kuliko yote ni; Je, kama hali itaendelea hivi ilivyo sasa kuna mafanikio tutakayoyapata huko mbeleni? Je, tumemiss maisha tuliyokuwa tunaishi awamu ya JK?

CC: chige Eric Cartman Salary Slip na wengineo karibuni kwa michango yenu..
 
Hongera sana kwa uchambuzi mzuri sana ambao yoyote Anaelewa kwa namna Ulivyochanganua mada yako,kwa mtazamo Wangu awamu ya JK wakati anaanza alianza vizuri sana na kuvutia mno kwa utendaji wake kwa kauli mbiu maisha bora kwa kila Mtanzania,kiukweli wakati wa JK hela ilikuwepo lakini rushwa ambaye ni adui wa haki ilizidi ilikuwa balaa hata kwenye haki yako lazima utoe chochote si kwamba kulikuwa na mteremko,binafsi Nilichukia mno serikali kwa upendeleo wa wazi mwenye nacho alikuwa anaongezewa, lakini Nilipopata kazi hali ilibadilika uchumi Wangu ukaimarika vizuri kurudi nyumbani na 50,60 au 70 ilikuwa kawaida tu,hakika ilikuwa Neema,ilipokuja awamu ya tano kwanza kampuni ilipunguza wafanyakazi,mauzo yakawa madogo mno ilikuwa inauza milioni 20 kwa wiki sasa Nasikia ukiuza laki Tatu kwa wiki unapewa hongera ya elfu kumi,mauzo yameshuka mno lakini mwanzoni Tulipata matumaini makubwa mno kwamba mambo yatakuwa bomba lakini imekuwa issue Tunapambana mwezi wa saba Tusirudi kijijini kubwa Tumwombe Mungu atuvushe salama Tukiwa safarini kwenda Nchi ya ahadi.
 
Natumai mwezi wa 7 utachangia ukiwa upo kijijini. Hii meli ishapotea katika bahari kuu. Break ya kwanza lampedusa.
 
Simply ni kwamba uchumi haijalishi umechuma kihalali au kiharamu inachojalisha ni ongezeko la namba!

Ulaya na marekani tunazozikimbilia zimeendelea na Kukua shauri ya wizi na dhulma kwa Bara la Afrika na kwingineko....

JK alitumia formula mamboleo za uchumi ila Magu and his team wanatumia formula za kale ambazo ni hatarishi sana kwa Dunia ya leo...

Kuchota mabilioni ya shilingi kwenye mzunguko kuyapeleka nje kununua midege ambayo return yake huchukua miaka mingi ni wazimu!!

Kwa nchi maskini kama hii government expenditure ya ndani ni booster kubwa mno ya uchumi kitu ambacho safari hii kimefinywa.
 
Kwa hiyo kwa akili zako unaona ni bora Rushwa na Sembe viachwe viwe vyanzo vya mapato kwa serikali na wananchi!!?

Piga kazi hela utaziona tu bila kufanya mizengwe yeyote ile!!

Akili zako unazijua mwenyewe.

Nitarudi tena ... ... ...
 
Hongera sana kwa uchambuzi mzuri sana ambao yoyote Anaelewa kwa namna Ulivyochanganua mada yako,kwa mtazamo Wangu awamu ya JK wakati anaanza alianza vizuri sana na kuvutia mno kwa utendaji wake kwa kauli mbiu maisha bora kwa kila Mtanzania,kiukweli wakati wa JK hela ilikuwepo lakini rushwa ambaye ni adui wa haki ilizidi ilikuwa balaa hata kwenye haki yako lazima utoe chochote si kwamba kulikuwa na mteremko,binafsi Nilichukia mno serikali kwa upendeleo wa wazi mwenye nacho alikuwa anaongezewa, lakini Nilipopata kazi hali ilibadilika uchumi Wangu ukaimarika vizuri kurudi nyumbani na 50,60 au 70 ilikuwa kawaida tu,hakika ilikuwa Neema,ilipokuja awamu ya tano kwanza kampuni ilipunguza wafanyakazi,mauzo yakawa madogo mno ilikuwa inauza milioni 20 kwa wiki sasa Nasikia ukiuza laki Tatu kwa wiki unapewa hongera ya elfu kumi,mauzo yameshuka mno lakini mwanzoni Tulipata matumaini makubwa mno kwamba mambo yatakuwa bomba lakini imekuwa issue Tunapambana mwezi wa saba Tusirudi kijijini kubwa Tumwombe Mungu atuvushe salama Tukiwa safarini kwenda Nchi ya ahadi.
Mkuu million 20 mpaka Laki 3... Aiseee lakini ndivyo mambo yalivyo...

Watu wamehama kunywa Heineken na Windhoek sasa wako na Balimi na Safari ndogo..
 
Awamu ya JK consumer economy ilikua kubwa mnoo,na kimsingi consumer economy haileti maendeleo katika nchi inayotaka kuendelea.Unasema biashara zilikua zinafanyika sana,biashara zenyewe zilikua biashara za kipuuzi tu Maduka ya Nguo,Simu,Saloon,Mighahawa ya chakula na vinywaji yaani kwa kifupo biashara za kuwapeleka watu chooni tu na kuwafanya wapendeze.

Consumer economy inafaa katika nchi ambazo tayari ziko katika ile hatua ya mwisho ya maendeleo kama alivyosema Walt Rostov(Mass Production and Mass consumption)

Kwa sisi nchi masikini tusingefika kokote na style ile ya matumizi,inabidi tujikite katika uzalishaji kwanza na ujenzi wa miundo mbinu ya uzalishaji ili nchi iendelee ndio tuje kwenye mambo ya kula bata tu kama enzi za JK.
 
Simply ni kwamba uchumi haijalishi umechuma kihalali au kiharamu inachojalisha ni ongezeko la namba!

Ulaya na marekani tunazozikimbilia zimeendelea na Kukua shauri ya wizi na dhulma kwa Bara la Afrika na kwingineko....

JK alitumia formula mamboleo za uchumi ila Magu and his team wanatumia formula za kale ambazo ni hatarishi sana kwa Dunia ya leo...

Kuchota mabilioni ya shilingi kwenye mzunguko kuyapeleka nje kununua midege ambayo return yake huchukua miaka mingi ni wazimu!!

Kwa nchi maskini kama hii government expenditure ya ndani ni booster kubwa mno ya uchumi kitu ambacho safari hii kimefinywa.
lusungo after a long time naona unarudi kwenye ubora wako..

US Government through CIA walikuwa wanacontrol carles nyingi za madawa kuanzia Mexico, Honduras, Panama, Nicaragua, Venezuela na hata kufikia kuawa waamerica wenzao wa kitengo cha DEA waliokuwa wanoko na hawafahamu kilichokuwa kinafanywa na serikali yao.. Hapo bado hatuzungumzii kile unachokisema cha kutunyonya na kutuibia sie maskini huku..
 
Kwa hiyo kwa akili zako unaona ni bora Rushwa na Sembe viachwe viwe vyanzo vya mapato kwa serikali na wananchi!!?

Piga kazi hela utaziona tu bila kufanya mizengwe yeyote ile!!

Akili zako unazijua mwenyewe.

Nitarudi tena ... ... ...
Mkuu kuna jamaa hapo juu amesema kampuni yao iliyokuwa inafanya shughuli halali kabisa, kwa wiki walikuwa wanauza mpaka 20M lakini tangia awamu hii ianze kuuza laki 3 unapewa bonus kabisa na ofisi. Yeye anayasema hayo akiwa amepunguzwa kazini ili kampuni angalau ipunguze expenditures zangu kulingana na wanachokipata.

Sasa suala la msingi ni kuwa ni lini mtaturudisha kule tulikokuwa? Na mna mipango ipi ya kuturudisha huko? Kazi tunafanya si kwamba hatufanyi mkuu..
 
Aiseee, haya mkuu mambo yatakuwa vizuri muda siyo mrefu utafurahi na nafasi yako.
 
Awamu ya JK consumer economy ilikua kubwa mnoo,na kimsingi consumer economy haileti maendeleo katika nchi inayotaka kuendelea.Unasema biashara zilikua zinafanyika sana,biashara zenyewe zilikua biashara za kipuuzi tu Maduka ya Nguo,Simu,Saloon,Mighahawa ya chakula na vinywaji yaani kwa kifupo biashara za kuwapeleka watu chooni tu na kuwafanya wapendeze.

Consumer economy inafaa katika nchi ambazo tayari ziko katika ile hatua ya mwisho ya maendeleo kama alivyosema Walt Rostov(Mass Production and Mass consumption)

Kwa sisi nchi masikini tusingefika kokote na style ile ya matumizi,inabidi tujikite katika uzalishaji kwanza na ujenzi wa miundo mbinu ya uzalishaji ili nchi iendelee ndio tuje kwenye mambo ya kula bata tu kama enzi za JK.
Lakini JK aliunganisha mikoa yote kwa rami? alijenga chuo kikuu dodoma, alijenga daraja la kigamboni, alipanua uwanja wa mwalimu nyerere kwa awamu mbili mpaka hii terminal three, elimu ya chuo kikuu ilikuwa rahisi kufikika na alitoa mikopo kwa watoto wa maskini, Dangote alikuja kipindi cha JK, Viwanda vingi tu vilijengwa kipindi chake sababu kabla ya yote kiwanda au muwekezaji kuja anaangalia purchasing power ya huko anakoenda kuwekeza.

Tinga tinga mnayemwita mzee wa mabarabara ni barabara ipi amejenga kwenye bajeti yake iliyopita? Barabara zote walizokuwapa wakandarasi ni tangia kipindi cha JK.. Au kuna muwekezaji gani mkubwa kamleta nchini mpaka sasa? Au tunaishia kuomba misaada ya viwanja vya mpira na misikiti?
 
Kuanza kufananisha utawala ulioko madarakani kwa miaka miwili na utawala ambao ulikuwa madarakani kwa miaka 10 ni kukosa focus na kufikia hitimisho potofu. Ningekuelewa sana kama ungelinganisha baada ya utawala wa Rais Magufuli kumaliza miaka 10.

Kumbuka pia kila utawala unakuta changamoto zake za kiuchumi na kijamii ambazo ni tofauti na kwa maana hii kulinganisha baada ya miaka 2 ni kosa kimantiki.

Kwa kifupi Kumbuka wakati Kikwete anaingia madarakani alikuta hazina ina pesa nyingi wakati huo huo nchi ilikuwa imefutiwa madeni ya nje na mahusiano na vyombo vya fedha vya nje yalikuwa yamerejeshwa[rejea bajeti ya mwisho ya utawala wa Rais Mkapa]

Kazi aliyofanya ni kuanza kutumia hizo pesa kwenye miradi mbali mbali na kuajiri wananchi serikalini.

Rais Magufuli amekuta hazina haina pesa za kutosha huku nchi ikiwa na deni linalotakiwa kulipwa ili apate mkopo mwingine.

Serikali inatumia zaidi ya nusu ya makusanyo kwa ajili ya kulipa mishahara pekee serikalini hapo bado haijalipa madeni ya nje achilia mbali madeni ya ndani.
 
Back
Top Bottom