Uchumi wa Kenya unategemea mahusiano ya kibeberu dhidi ya Tanzania

Haya ndio matokeo HASI ya ujamaa na kjitegemea wa TZ, hakika Kenya ilianza kunufaika na uchumi wa Tanzania baada tu ya Azimio la Arusha, Ile taifisha viwanda na mashamba, makampuni makubwa hawa wamiliki walichokifanya ni kuondoka na mitaji na wengine walihalishia viwanda kenya

Wakaendelea kutumia rasrilami gafi zile zile ila sasa kwa kuvuka mpaka,Ujasriamali, Raw materials, viwanda na watu na mitaji ile ile ya Tanganyika ikavuka mipaka na bidhaa baada ya uzalishaji zilivuka tena mpaka kuja kuuzwa soko lao la asili TANGANYIKA

Tangia hapo nachelea kusema kwamba Tanganyika iligeuka kuwa koloni la KENYA kiuchumi (inauma sana sana) kwa nini ? kila kilichozalishwa TZ kilicho bora kiliuzwa kenya au kiliunzwa Ng'ambo lazima kupitia kenya isipokuwa tu Pamba vingine vyote kenya, Ngombe mnono, ngozi yake, mahindi, kahawa, alizeti,kila mazao Dhahabu, Tanzanite, Samaki, Katani, kila kitu kwa wale watz wanaoshi mipaka ya kenya wanajua na sisi walituletea Sabuni, mafuta kula , mafuta kujipaka, vyombo plastic n.k

Siasa yetu ya UJAMAA ILIUA KABISA UJASRIAMALI(ENTREPRENEURSHIP) Hao Hao Wafanyabiashara tukawachukia tukawaita majina ya ajabu kenya ikawakumbatia ikawawezesha wafanyabiashara wanahamisha wanafyonza RASRIMALI ZOTE toka tz kwenda huko na hadi leo kwa kusaidiwa na serikali hiyo

Siasa ya Ujamaa ina faida nyingi kwenye jamii lakini kwenye Uchumi na maendeleo kwa ujumla wake HAIFAI KABISA hasa private sector usitegemee mafanikio, na hata hiyo jamii hiyo hiyo bado itahitaji au itategemea uchumi ulioimara kuifanikisha ambao kwa hakika unatokana na private sector kimsingi.

Ntaendelea . . . .
Kazi ya wajamaa ni kulia Lia bila kuja na suluhisho.

Ulimwengu wa kibeberu ni kupambana kibeberu hivyo hivyo sio kulia lia
 
Mbona China wako mbali na ujamaa wao?
Niambie, kuna nchi gani Afrika ambayo imefika mbali kwa sababu ya ubeberuni?
Usiwe kenge ,China ni wajamaa kwenye siasa zao za ndani ila siasa za nje ni mabeberu,siasa na sera za Uchumi ni mabeberu..

Kwani husikii China inachozifanya nchi mbalimbali kwenye mambo ya rasilimali na mikopo?
 
Mkuu haelewi anafikili China serikali imehodhi njia kuu za uzalishaji Mali
 
Usiwe kenge ,China ni wajamaa kwenye siasa zao za ndani ila siasa za nje ni mabeberu,siasa na sera za Uchumi ni mabeberu..

Kwani husikii China inachozifanya nchi mbalimbali kwenye mambo ya rasilimali na mikopo?

Bado hujawajua China, wee utulie tu.
 
Ila ujue ujamaa lengo lake ni kuhakikisha wananchi wote wanapata haki kwenye maendeleo kiuchumi na kwamba tofauti kati ya matajiri na tabaka la chini sio kiwango cha kupindukia.
Ujamaa ndio umetufanya watanzania kuwa Mazezeta na makondoo. Siasa hii ndio imegeuza viongozi wenye mitazamo ya kijamaa kugeuka kuwa mabepari uchwara. Leo hii tuna viongozi matajiri kwa wizi, lakini wanaoogopa ushindani, hivyo kujikuta wakitoa huduma na bidhaa duni. Sehemu kubwa wamebaki kuendesha hila na fitina zisizoendana na kanuni za ushindani wa soko.
 
Mbona China wako mbali na ujamaa wao?
Niambie, kuna nchi gani Afrika ambayo imefika mbali kwa sababu ya ubeberuni?
Taja iliyofika mbali kwa ujamaa. Afrika kusini iko mbali kwa ubeberu
 
Watoto wa siku hizi bwana?
Wee Unajua kuwa Afrika Kusini ina nchi mbili?
Moja Ilipata uhuru mwaka 1922 ba nyingine 1994?
 
Acha kulazimisha majibu, taja nchi iliyoendelea kwa huu ujamaa uchwara.
 
Mada kama hii huwa zinaumiza sana.

Mwishowe mtu unajiuliza, hivi hao Kenya wana mvuto gani na Tanzania, kiasi kwamba tumeshikiliwa na sumaku yenye nguvu tusiyoweza kujinasua nayo?

Nilishauliza swali humu, lakini sijawahi kupata jibu juu yake:
Tunao majirani wengi sana tunaopakana nao mipaka, lakini katika majirani wote hao, hakuna nchi hata moja ambayo, sijui kama ni kwa kujua au kutojua, tunao njia nyingi sana za kuingiliana nao ukilinganisha na njia tulizonazo na jirani yetu Kenya, tena njia hizo zinaendelea kuboreshwa kwa kiasi kikubwa, huku majirani zetu wengine ni kama hatuna habari nao.
Kwa nini imetokea kuwa hivyo, ni mipango ya hao wenye bahari yao wanaofanya mambo bila ya sisi kutambua?

Angalia mpaka wetu na Kenya, tuna barabara nzuri kuingiliana pale Namanga, nyingine ipo siyo mbali sana pale Horiri, na nyingine Holoholo, Tanga. Ziwani kuna meli kadhaa, na bado Kenya wanatafuta njia ya moja kwa moja ya kuingilia Serengeti. Pale Sirari kuna barabara nzuri kuingia Mara, Mwanza, Simiyu na maeneo mengi mengine toka Kenya.

Angalia ramani, Namanga na Horiri zimeunganishwa na Mombasa kwa barabara safi kabisa. Barabara hiyo ikitoka Mombasa, kuingia Arusha, inachepuka na kuteremka kwenda Singida kuungana na ile kuu kuelekea Tabora na kwingineko, kama Burundi na hata Rwanda. Barabara hiyo wenyewe waliwahi kusema ni barabara yao ya kwenda Burundi, tokea Mombasa, na muda si muda watadai kupitisha mizigo yao kwenda huko.

Bado hairidhishi, kuna barabara tunachukua mkopo wa AfDB, ijengwe toka pale mpakani Tanga , ikitokea Malindi, iambaeambae kando kando ya bahari ya Hindi ifike Bagamoyo. Tumechukua mkopo tujenge barabara hii, huku ikiwepo barabara nzuri tu toka Tanga hadi Dar.
Hii barabara ni ya nini, kutuletea wakenya pwani kwetu?
Hatuna mahitaji ya barabara nzuri kama hiyo na majirani zetu wengine, kama Uganda, Zambia, Malawi, na hata angalau kuweka meli kadhaa kuvusha ziwa Tanganyika kwenda DRC?

Kenya kuna nini tunachokifuata huko kila mara! Ni viongozi gani wanaotufunga na Kenya kiasi kwamba tunajisahau kuwa tunao majirani wengine tunaohitaji kufanya biashara nao?

Ninakubaliana na mada yako kwa jambo moja.
Kuna njama za namna fulani zinazotuvuta kuwa mkia wa Kenya.
 
Simple, zile nchi zilizo wazunguka hazina faida sana kiuchumi kwa Tanzania, ni fukara sana ukilinganisha., kwa mfano Burundi itapatia nini Tanzania ama Tanzania itauza mali kiasi gani kule ilhali mahitaji yao ni kidogo kwasababu ya uchumi ndogo?., Mahitaji yao ya imports ni kidogo sana yaani hata haiwezi kuipa Dar port faida, mali mingi yenye inapitia dar port inaingia Tanzania kwa matumizi., then zile chache mnasambazia akina Congo, Rwanda na Burundi., ni uchumi sio njama ama eti kuna kiongozi anae wafunga na Kenya, kwanza viongozi wenu na wanasiasa hawapendi Kenya ndio maana wanawalisha propaganda, ila wanabiashara na wakulima wanaona faida mingi Kenya wanajileta, pole pole mmeanza kukua mabepari kwa mpigo, kwa ajili ya forces of supply and demand, na sio siasa wala nini., Serikali ya Tanzania inajenga miundo mbinu kutokana na hitaji, kama usafiri na biashara kuelekea upande wa Kenya kwa wingi kushinda zile nchi zingine, wataboresha infrastructure huo upande, mbona wajenge barabara mingi kuelekea Rwanda, Congo na Burundi na pesa na ushuru kwa Tanzania ambazo biashara kutoka hizo nchi ni kidogo ukilinganisha na pesa taifa linapata na faida kwa wanabiashara kutoka Kenya?
Think outside the box, sio kila jambo unaona mischief, elewa economics. Wanasiasa wenyu ndio vikwazo kwa ukuaji wa Tanzania, wala sio wakenya ama serikali ya Kenya, la hasha.
 
Kwani ukilewa lazima uje huku jukwaani? Hizo ni nchi za kijamaa?

Unahitaji uende shule zaidi. There is no pure economic system on earth, all of them are graduated system. In China they have so called socialistic market economy, likewise Russia.
 
Nenda Botswana na Namibia, utanielewa.
Kwani ukilewa lazima uje huku jukwaani? Hizo ni nchi za kijamaa?
Unahitaji uende shule zaidi. There is no pure economic system on earth, all of them are graduated system. In China they have so called socialistic market economy, likewise Russia.
Kama aliyekwenda shule ni kama ww, bora mtu asiende.
 
Back
Top Bottom