Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,154
- 10,809
Mwaka 2019 bank ya dunia ilitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati miaka mitano mapema zaidi kinyume na ilivyokuwa imetabiriwa kwamba itachukua miaka kumi.
Je, kuwahi huku kuingia uchumi wa kati ilikuwa ni matunda ya nidhamu ya uoga? Kama nidhamu ya uoga ina matunda kiasi hiki kwa nini tuiogope sasa?
Kwa watoto wadogo na wasiojua mambo wanadhani hayati Magufuli alianza kuwa mkali alipokuwa rais wa nchi tu wakati ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa mkali na mfuatiliaji tangu akiwa naibu waziri, waziri na baadae rais wa nchi.
Katikati ya mafisadi wakubwa wa awamu za Mkapa na Kikwete lakini walimwogopa Magufuli aliwashughulikia kila wizara aliyopelekwa, swali la kujiuliza aliwezaje?
Hata baada ya kuwa rais na kufariki dunia mpaka leo mwaka umeisha si Chadema, ACT Wazalendo wala CCM waliokuja na ushahidi usiotia shaka juu ya ufisadi wake licha ya kwamba waliahidi pindi tu atakapotoka madarakani basi watakuja na mikataba ya ufisadi na rushwa kubwakubwa zilizosainiwa na yeye.
Mwezi March 2022 umetimia mwaka mzima tangu atutoke duniani lakini mahasimu wake ikiwemo, Lisu, Lema, Nape ,Makamba, Kigogo bado hawajawaletea watanzania ufisadi wa Magufuli.
Kinyume chake wanaendeleza mafanikio na miradi ya awamu ya tano kwa kasi kubwa, walipinga kila kitu lakini sasa wanatumia kila kitu walichokipinga!
Walioahidi kuifunika legacy kumbe hawana uwezo kuifunika hata kidole chake tu!
Muda utawaumbua zaidi.