Uchumi wa Kati Tanzania. Nani Mkweli kati ya Dkt. Mpango VS Mwl JK Nyerere?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,216

Huyu ndio waziri wetu wa fedha was sasa hivi. Je, yuko sahihi zaidi ya Mwasisi wa Taifa Dr Julius Nyerere aliyezungumza haya ndani ya Bunge la Afrika Kusini wakati wa Mandela?

Na kati yao kuna mmoja kazungumza uongo, je ni kwa manufaa ya nani?

Msikilizeni na Dr Julius Nyerere aliyeheshimika duniani kama mwenyekiti wa South South Commission.

CCM haijawahi kuzungimza lugha tofauti ni wamoja.
Serikali ya CCM haitapumbazwa na mafanikio haya bali itaweka nguvu zaidi kuhakikisha kuwa kila mtanzania anajisikia yumo kwenye nchi ya kipato cha kati.
Tukumbuke kuwa Tanzania inatambilika kuwa nafasi ya juu ya uchumi jumuishi.
 
MODS Rekebisheni WAS to be wa katika heading. Please!
 
Waziri kasema nchi imeingia kwenye kundi la nchi za kipato cha kati kwa kuzingatia categorization za WB, Mwl. Nyerere kawaambia wasauzi pamoja na kuwa na wastani huo wa kipato bado wao ni maskini. Sijaona kukinzana kokote hapa, maana waziri katangaza kuingia kwetu kwenye hilo daraja, na hajasema kwamba sisi sasa ni matajiri.
 
Bali umeelewa maana ya tangazo lake lenye kumsifu JPM?
Fungua akili yako mkuu uelewe maana ya thread
 
Hizo takwimu ni kwa mujibu wa WB ie categorization, sioni tatizo lolote/ issue inakuja pale tu wengi wanapotumia hizo stats kujenga hoja zao za kisiasa. Leo hii hata miaka yote hiyo ya nyuma wamekuwa wanasema watanzania ni masikini sana kwa sababu wananchi wake wanatumia less than $1 kwa siku kitu ambacho hakikuwa na ukweli wowote ukilinganisha na nchi ambazo tunapakana nazo.

Hivi sasa wanakubali kwamba Watanzania wanatumia angalau $1.25 - $2.86 kwa siku ambayo kwa hali ya Watanzania wengi ipo sahihi zaidi.
 
Huyu ndio waziri wetu wa fedha was sasa hivi. Jee yuko sahihi zaidi ya Mwasisi wa Taifa Dr Julius Nyerere aliyezungumza haya ndani ya Bunge LA Afrika Kusini wakati wa Mandela?
Na kati yao kuna mmoja kazungumza uongo, jee ni kwa manufaa ya nani?
Msikilizeni na Dr Julius Nyerere aliyeheshimika duniani kama mwenyekiti wa South South commission.

View attachment 1498606

Dr. Julius Nyerere? Tangu lini? Aliitwa Mwalimu Julius Nyerere na ndivyo alivyotaka. Sio Dokta au Mheshimiwa bali Mwalimu.

Amandla...
 
Mkuu sasa unapagawa na siasa!!
Hao wote wapo sahihi kabisa. Kwanza hawazungumzi kitu kimoja kimantiki iweje uwalinganishe kauli zao?
Ingekuwa Dk. Mpango anasema nchi yetu kuingia uchumi wa kati wa chini basi nchi imekuwa tajiri na watu wote wana pesa kama iliyotajwa kwenye GDP yetu, hapo tungesema ni muongo.

Kukujibu swali lako wewe ndiye muongo, hao watu wote wapo sahihi hakuna asiye mkweli ktk maelezo yake.
 
Hizo takwimu ni kwa mujibu wa WB ie categorization, sioni tatizo lolote/ issue inakuja pale tu wengi wanapotumia hizo stats kujenga hoja zao za kisiasa. Leo hii hata miaka yote hiyo ya nyuma wamekuwa wanasema watanzania ni masikini sana kwa sababu wananchi wake wanatumia less than $1 kwa siku kitu ambacho hakikuwa na ukweli wowote ukilinganisha na nchi ambazo tunapakana nazo.

Hivi sasa wanakubali kwamba Watanzania wanatumia angalau $1.25 - $2.86 kwa siku ambayo kwa hali ya Watanzania wengi ipo sahihi zaidi.
Dola moja anatumia mtanzania alie wapi? Mana dola moja ni elf 2500 Nan anakula ela io bongo?
 
Dola moja anatumia mtanzania alie wapi? Mana dola moja ni elf 2500 Nan anakula ela io bongo?

Mkuu hizo ndio criteria za WB, hivi sasa tupo huo uchumi wa lower middler class ie watanzania wote utajiri wao ukigawanywa ndio wanatumia $1.25-$2.86 kwa siku. (Hio ndio maana yao). Sio mimi mkuu ni WB, kama unakumbuka Watanzania wengi walikuwa hawakubaliani na mawazo ya WB kwamba Tanzania wako masikini sana kwa sababu watu wao wanatumia chini ya dola moja kwa siku. (Debatable but that is what it is (WB).
 
Dr. Julius Nyerere? Tangu lini? Aliitwa Mwalimu Julius Nyerere na ndivyo alivyotaka. Sio Dokta au Mheshimiwa bali Mwalimu.

Amandla...
Hakukuwa na zuio la kumuita hivyo kisheria wakati alistahili hata kama hakupenda.
 
Hakukuwa na zuio la kumuita hivyo kisheria wakati alistahili hata kama hakupenda.
Anastahili kwa nini? Alipata wapi Ph.D? Kwa kwenda kinyume na matakwa yake ni ishara tosha kuwa haumthamini wala kumheshimu. Unamtumia tu kwa faida yako.

Amandla...
 
Hii mada mnaijadili kisiasa zaidi kuliko kiuhalisia.
Nyerere aliamini kuhusu usawa wa watu wote hasa kwenye huduma za jamii ndio maana alifanya huduma za afya na elimu bure pia hakupenda kuwepo pengo kubwa kati ya masikini na matajiri wakati wb na imf sera zao ni kumuinua mtu mmoja mmoja hata kukiwa na matajiri 10 katika watu milioni 50 kwao sio tatizo kuongezeka kwa wastani wa pato la taifa hakumaanishi kuwa watanzania wengi uwezo wao umeongezeka bali idadi ya mabilionea wameongezeka
 
Anastahili kwa nini? Alipata wapi Ph.D? Kwa kwenda kinyume na matakwa yake ni ishara tosha kuwa haumthamini wala kumheshimu. Unamtumia tu kwa faida yako.

Amandla...
Nimekuweka katika kundi la wasio elewa kitu.
Julius Nyerere ametunukiwa PhD zaidi ya nane za heshima kutoka vyuo mbalimbali vinavyo heshimika duniani.
Hilo nadhani hulifahamu kwa vile wewe ni "fundi mchundo"
 
Nakushukuru sana kwa kuniweka katika kundi la watu wasioelewa kitu. Ph. D za heshima sio sawa na za kusomea na mtu yeyote anaweza kupewa. Kwa vile hamna criteria za kitaaluma kuhusu nani anastahili kupewa hizi Ph.D za heshima kuna baadhi ya vyuo vinazitumia ili kujipendekeza kwa wale ambao wanaona wanaweza kuwasaidia. Ndio maana mara nyingi watu wanaopewa tuzo hizo za heshima hawatumii prefix ya Dr. Askofu Desmond Tutu anazo kibao na hata siku moja hutasikia akiitwa Dr. Tutu, vile vile kwa Mandela, Obama n.k. Na hata wale ambao wana Ph.D za kitaaluma kama Angela Merkel mwenye Ph.D ya Quantum Chemistry hatumii prefix ya Dr. Muenzi Mwalimu kwa vitendo vinavyoendana na falsafa yake na sio kwa kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kumpa sifa ambazo hakuzitaka wakati wa uhai wake.
Na mimi sio Fundi Mchundo tu bali pia ni Fundi Utumbo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom