Uchumi wa kati na nchi ya viwanda

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Kumekuwepo na mjadala mkali kuhusu dhana ya "nchi ya viwanda" na "uchumi wa kati". Huu uchumi wa kati tunaufikia vipi kama wakulima wetu wana hali mbaya?? Nchi ya viwanda kivipi wakati umeme ni wa mgao na unakatika katika mara kwa mara??

Nadhani ni wakati sahihi kwa serikali ya Magufuli ambayo imejipa jina la "serikali ya wanyonge" sasa ifanye kwa vitendo. Hatuwezi kurukia viwanda kama kilimo chetu ni cha JEMBE la mkono!

Tuna biashara zitokanazo na viwanda vidogo vya ndani lakini bado tuna thamini vya nje! Huku ndani tunabebeshana kodi kila iitwapo leo! Kwa mtindo huu hiyo nchi ya viwanda na uchumi wa kati itabaki kama hadithi kwenye magazeti na makaratasi!

Leo hii tunakosa ubunifu, tunatengeneza bajeti inayo egemea POMBE na SIGARA.. Uko wapi ubunifu mpya?? Uko wapi mkakati mpya wa kiuchumi wa kulivusha taifa??

Napendekeza yafuatayo yafanyiwe kazi ili hiyo nchi ya viwanda na uchumi wa kati visiwe ndoto za MFALME JUMA au matamanio ya ABUNUASI:

1. Serikali itoe ruzuku na fidia kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa malighafi. Kwa mfano, wakulima wa mazao ya nafaka, Pamba na mazao mengine wapewe ruzuku itakayo linda uzalishaji wao, kuongeza morali ya uzalishaji na pia kuinua uchumi wao hata kama soko likiyumba.

Kwa mantiki hiyo sasa ni wazi kwamba wakulima wataongeza uzalishaji ambao utavipa uhai viwanda vyetu. Lakini pia uzalishaji huu utatoa mwelekeo wa "priority" Kwa serikali juu ya viwanda gani ni vya msingi kuviimarisha. Hapa tutafikia hiyo nchi ya viwanda na uchumi wa kati.

2. Serikali ipunguze kodi zisizo za lazima kwa viwanda vilivyopo na vitakavyo anzishwa lakini pia ipunguze kodi kwa wauzaji wa bidhaa hasa wale wa chini.

Hii inasaidia kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa ili mwananchi imfikie bidhaa ambayo haina gharama kubwa. Kodi zisizo za lazima zina tabia ya kuongeza gharama za ununuzi na kupandisha gharama za maisha yaani inflation.

3. Baada ya kufanya hayo yote, sasa serikali iongeze tozo kidogo katika kila bidhaa itokayo nje. Hii itafuta UDHAIFU wa kibajeti wa kutegemea Pombe na sigara, angalau hii itakuwa ni mbinu mbadala kukabili UDHAIFU huo.

Bidhaa kutoka nje ya nchi zikiuzwa kwa bei ya juu na bidhaa ya nyumbani zikiuzwa kwa bei ya chini, hali hii inasaidia sana katika nchi inayo anza kujenga mifumo yake ya kiuchumi.

Hapa bidhaa za ndani ya nchi zitapata sana soko tena la uhakika. Yaani serikali isizuie bidhaa za nje, ila tozo ipande! Moja ya makosa ya Serikali hii ilikuwa ni kuzuia sukari isiingie nchini tukidhani ni UZALENDO lakini Matokeo yake kukawa na uhaba wa sukari nchi nzima.

Leo hii wakulima nchi hii ni masikini sana, nenda kule Kilombero kwa wakulima wa miwa, nenda Mtwara kwa wakulima wa korosho, nenda Geita kwa wakulima wa Pamba.... Yaani hali zao hazileti matumaini ya uchumi wa kati wala uchumi wa viwanda!

Kama wakulima na wazalishaji wa malighafi wana yumba yumba katika uzalishaji, malighafi duni, ubora na uthamani haupo.... Nchi ya viwanda gani?? Kwa uchumi upi?? Viongozi tazameni mambo haya ya msingi.

NB: Kuna mazao yalikufa kwa sababu ya kukosa mikakati mizuri na mahitaji ya viwanda. Kwa mfano zao la mkonge kule Tanga! Sijui tunalitumia kama makumbusho?? Sijui ni alama ya kihistoria?? Tunahitaji akili mpya!

Mwanahabari Huru
 
kuna wale wapenda sifa bado wataona ni bora kununua made in UK kwa laki 7 wakati made in TZ hio hio ni laki na ishirini kwa quality ile ile! Hao watu ndio majipuuuu!
 
Mkuu nilishawai kuleta hoja kama hii nikatukanwa na vijana wa Lumumba live kabisa,niliambiwa sio kipaumbele kwa sasa. Sasa wengi mmeshaelewa nini umuhimu wa kilimo kabla ya viwanda. Haiwezekani kilimo kinachoitwa kua ni uti wa mgongo wa nchi hii kinachangia 8% kwenye pato la taifa. Malengo yao yameshatimia wamekua Ma-DC,DAS,DED sasa kimya.
 
Mkuu wacha watukane tu lakini penye ukweli tutasema
 
Back
Top Bottom