Uchumi wa kati husababisha ongezeko la bidhaa kupanda juu na maskini kuishi kwa shida?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,343
2,000
Mwenye majibu ya haya atujuze maana tumeambiwa uchumi wa kati ni maisha kuboreka, maendeleo makubwa na maskini kupungua kwa idadi. Sasa haya ya upandaji wa bidhaa kama Mafuta, Sabuni, Unga wa ngano, sukari kwa sasa sh. 2,800 ndio majibu ya uchumi wa kati?

Kuna Wilaya imeanza kutumika kama sampuli ya kuweka kodi kwa wapiga picha, washereheshaji, ma MC, Ongezeko la kodi kweye magari ya kubebea maiti. Wilaya hii ikifanikiwa bila malalamiko basi mikoa yote itaanza pia kutoza kodi hizo.

Nauliza tena huu ndio uchumi wa Kati? Sikatai kutoza kodi hapana nakubali ila swali ni je, huu ndio uchumi wa kati au ni ile miaka 5 tuliyoambiwa inayokuja?
 
chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,090
2,000
Takwimu zimeshatolewa na IMF,word bank,nk.tuko uchumi wa Kati, reflection ya uchumi wa Kati ina vitu vingi mkuu.usi banwe na eneo moja tu .
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
14,247
2,000
Sukari kilo inapaswa iuzwe 2500...kwa maana mfuko wa kil0 50 unauzwa 116000...anayeuza 2800 anatafuta faida kubwa zaid
 
Simba zee 33

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
1,377
2,000
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia. Nchi yetu ipo Uchumi wa kati na maisha yamekua rahisi sana
Shule bure.

Huduma za afya bure. Yaani maisha yamekua mazuri sana kuanzia Wafanyabiashara. Wafanyakazi. Hata Wakulima maisha ni bam bam isipokua wapiga dili Ndio wapo hoi wanaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Simba zee 33

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
1,377
2,000
Nchi hii ni tajiri sana.

Tupo Uchumi wa kati.

Sisi tunatembelea mavieite.

Unaijua vieite wewe!!

IMG_20210101_160453.jpg
 
jailos mrisho

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
467
1,000
Mwenye majibu ya haya atujuze maana tumeambiwa uchumi wa kati ni maisha kuboreka, maendeleo makubwa na maskini kupungua kwa idadi. Sasa haya ya upandaji wa bidhaa kama Mafuta, Sabuni, Unga wa ngano, sukari kwa sasa sh. 2,800 ndio majibu ya uchumi wa kati?....
Mbona huna akili mzee baba kodi ni lazima ilipwee katika kaz yyte inayokuingizia kipato..ukitaka maendeleo na kuacha kuwa kupe kwa beberu. lazima kila sh inaingia kwa mtu iwe imekatwa kodi..sasa ww dunga embe unalala na kodi..unahusianisha na uchumi wa kati..hujielewii.

Kodi hamtaki kulipa huduma bora za jamii mnazitaka..nyie vip waafurika?

Yaan nilichokuja gundua kati ya watu weusi 10 mmoja ndo mwelewa wengine wote ni hewa.

Angalizo kodi iwe ya haki sio ya dhulma
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,934
2,000
Mwenye majibu ya haya atujuze maana tumeambiwa uchumi wa kati ni maisha kuboreka, maendeleo makubwa na maskini kupungua kwa idadi. Sasa haya ya upandaji wa bidhaa kama Mafuta, Sabuni, Unga wa ngano, sukari kwa sasa sh. 2,800 ndio majibu ya uchumi wa kati?

Kuna Wilaya imeanza kutumika kama sampuli ya kuweka kodi kwa wapiga picha, washereheshaji, ma MC, Ongezeko la kodi kweye magari ya kubebea maiti. Wilaya hii ikifanikiwa bila malalamiko basi mikoa yote itaanza pia kutoza kodi hizo.

Nauliza tena huu ndio uchumi wa Kati? Sikatai kutoza kodi hapana nakubali ila swali ni je, huu ndio uchumi wa kati au ni ile miaka 5 tuliyoambiwa inayokuja?

Sasa unaingia Uchumi wa kati.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom