Uchumi unatupeleka kuwa na awamu ya lishe wakati tu wazalishaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumi unatupeleka kuwa na awamu ya lishe wakati tu wazalishaji

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, Jan 29, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  Jamani mapumziko mema ya weekend, eat fresh, enjoy what your earn during the long week, stay safe and sober.
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hiyo chakula ya mdhungu....sijaona ugali na tumba ya maharage bana
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Yes,n i kitu tu cha kawaida kupima nini kinahitajika mwilini badala ya kushindilia tu tonge kubwa na kisha 75% ya tulichokula kuishia kutolewa nje kwa kutohitajika mwilini.
   
 4. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...hiyo kitu kubwa nyeupe ndo iliyonikuza naipenda sana,huku kwetu tunaiita "LA MWIDEBE" ukipata hiyo kitu{ugali} kwa Sangara chukuchuku,pilipili mbuzi na kachumbali kwambali...ah! chakuka ya asili tamu bhana...hayo mavyakula ya kidhungu ni yakutengenezea movies za akina Kanumba...
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hatuna maana ya kubeza tonge la ugali, ndilo lililotukuza tuwe tulivyo, lakini bora kufikiria siha kwanza badala ya sima kubwa ambayo hata nyau hawezi kuiruka. Unaona mboga kidogo mno kwenye sahani inayotosheleza tonge tatu tu, sasa ugali wote huo kitoweo kiko wapi?

  Tuna hulka ya kula sana kile ambacho hakitatumika mwilini. Mlo mzuri hasa kwa watu wanaoshinda ofisini ni mmoja na vinginevyo ni vya kupitiliza siku. Utashangaa asubuhi chai nzito, mchana ugali, jioni ugali thats too much. Wanaofanya kazi nzito mashambani, viwandani nk. hii inaeleweka.

  Niendapo kijijini huwa wananishangaa ninapokataa kula milo miwili ila mmlo mkubwa mmoja tu, pengine wanaona kama najivunga kumbe ndivyo nilvyozoea. Nikila mchana mlo mkubwa basi jioni ni vitafunio na juice inatosha najua nilichokula kiasi kikubwa kitatumika mwilini.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nikiona nakumbuka ule usemi unaosema kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unaweza kuna na ukweli na pengine sivyo. Mkulima ndiye mwenye nafasi ya kuitumia ardhi kwa uhuru zaidi, na ndiye aliyejaza nafaka na mbogamboga pale kariakoo na masoko mengine, kinachohitajika tu walao kupunguza ukubwa wa sima ya ugali na kuongeza mboga za majani, maana hata shibe ugali huwa nzuri kutokana na kitoweo cha mboga, na maharage.

  Kwa nini wasiweke kidogo na futari, kama mihogo kidogo, kiazi mviringo, jami la mchicha, chunga au embe mlo bomba kabisa na vyote nilivyotaja viko ndani ya uwezo wa wengi wetu.
   
Loading...