Uchumi unapaa kuliko nchi zote Afrika, Safaricom ya Kenya wana faida ya Tril 1.2; TZ jumlisha mabenki na simu hatufikii

Kenya siyo tu ina Uchumi mkubwa klk TZ yetu bali pia ina purchasing power kuliko TZ tena pengo la purschasing power ni kubwa zaidi na hii ni kwa sababu ya UN.
Nairobi ni Makao makuu ya UN Afrika, UN ina ofisi nne tu Kuu Duniani, Geneva, Nairobi, New York na Vienna, sasa waajiriwa wa UN wanachangia kwa kiasi kikubwa sana purschasing ya Kenya, na imekuwa hivyo tangia miaka ya 60' huko, hivyo hakuna cha ajabu hapo!
Clearly your education system is the issue here
 
Hao ni kama bongo kwa kiasi fulani sema nao kwa wametuzidi kwa kiasi fulani kwa maana pia wanafaidika na kujiriwa kwenye hizo ofisi za UN kama local stuff lkn bado wanalipwa vizuri!
Oooh my this sort of weed should be banned
 
Kenya siyo tu ina Uchumi mkubwa klk TZ yetu bali pia ina purchasing power kuliko TZ tena pengo la purschasing power ni kubwa zaidi na hii ni kwa sababu ya UN.
Nairobi ni Makao makuu ya UN Afrika, UN ina ofisi nne tu Kuu Duniani, Geneva, Nairobi, New York na Vienna, sasa waajiriwa wa UN wanachangia kwa kiasi kikubwa sana purschasing ya Kenya, na imekuwa hivyo tangia miaka ya 60' huko, hivyo hakuna cha ajabu hapo!
Na kama ni hivyo itaongezeka zaidi mbeleni kwakuwa un inahamisha makao makuu pekee ya logistics yaliyo entebbe uganda kwenda nairobi. This logistic base serves as a center of logistic strategic reserve supporting peace keeping mission operations in africa. It is bigger than all un offices combined in kenya
 
Safaricom haioperate Tanzania wala hatuma share mle, why should we know it's annual profit? Tena hiyo habari inaletwa katikati ya sekeseke la yule mkenya kupigwa chini kuja kufanya kazi nchini. Ulishakutana na hizo habari ya faida ya safaricom humu JF in the last three years? Hapo ni ndo mzizi wa propaganda unapokuwa!
Usiogope kujifunza kwa hofu ya kuchekwa , acha wivu wa kijinga
 
Acha CHADEMA ifutwe kwanza! (poking).
Propaganda za Tanzania ni za 'old stone age'. Fuatilia tu miradi inayozinduliwa na mwenge, utaelewa namaanisha mini.
Pamoja na kwamba sifahamu Kenya vizuri, ila kwa Tanzania mambo mengi bado sana!
Hata fuatilia hoja zinazotolewa Bungeni, mtaani ....
Angola nayo inatuacha parefu.
UTAFITI UNAONYESHA KWAMBA HAKUNA MRADI WOWOTE ULIOZINDULIWA NA MBIO ZA MWENGE ULIODUMU HATA KWA MIEZI 6 , mfano halali ni mradi wa maji wilayani Kyela
 
Uchumi wa Kenya kweli ni mkubwa kuliko wa kwetu ......... lakini siyo kwa kiasi hicho. Uchumi wa Kenya wala siyo mara mbili ya uchumi wetu. Sasa kama kweli kampuni moja tu linavuta faida mara mbili ya makampuni yetu makubwa 14 combined, hapa kuna kitu inabidi tujiulize ...... Something, somewhere is not right!!
hao makombwea... kazi yao nikusifu tu mpaka ujinga ""
 
No wonder ulisema Air force one ndo ndege kubwa kuliko zote duniani!! Una usaha kichwani nyauba weh! Hapa bongo tuna ofisi ngapi za kibalozi? Yaani wafanyakazi wa UN ndo purchasing power ya Kenya? Mna laana si bure!!
hahaaa...."" MPE huyo "" hili bwege " kweli
 
Kenya kampuni ya simu ndio inatengeneza faida kubwa !!! Huku kampuni ya Bia ndio inatengeneza faida!!
Tunatofautiana sana na Kenya kwenye mtizamo na priorities za maisha
 
Mkuu,mzunguko wa Pesa unaletwa na serikali,ukuaji wa uchumi unaletwa na serikail,kazi kwa wananchi zinaletwa na Serikali...ndio maana ya serikali unatakiwa ufahamu hivyo

Mmeshikilia pesa za wizi,pesa za wizi,!! hivyo ndivyo mlivyozi-programed aliki zenu,Mfanya Biashara Karikoo kafunga duka lake kawasababu kodi kubwa,wateja hakuna utamwita alikuwa na hela za wizi...

Nikupe mifano Mkuu,..Nchi ya marekani katika miaka ya 80 au 90 uchumi ulikuwa unalega lega,..Mji wa Florida uchumi ulikuwa unakuwa kwa haraka sana,majumba yakawa yanajengwa biashara zimebumu,..

kitu kilichofanya uchumi wa Florida na jimbo kuanza kung'ara ilikuwa biashara ya Unga,serikali ilikuwa inajua hilo lakini kutokana na hali ilivyo hayo mambo waliyafumbia macho..ref "Cocaine Cowboys",..angaliia hiyo documentary utafahamu nini najaribu kukufahamisha

Obama alipoingia madarakani uchumi wa Marekani uklikuwa katika hali mbaya makampuni yanafungwa "Purchasing power" iko chini raia hawana pesa,alichokifanya Obama serikai yake ilikupoa katika "reserve bank" na kukopesha makampuni,..

Moja katika kampuni kubwa ambayo ilikukopeshwa ili isifilisike ilikuwa GM(General Motors).,Kuinua GM ni kuinua hali za watu,nikuwezesha serikali kukusanya kod,ni kuwezesha raia kulipa kodi:-"Mzunguko wa pesa"..

Katika Pesa zilikopa utawala wa Obama Kitu chengine kilichofanywa ,walianza kutengeneza miundo mbinu,kujega madaraja,na miradi mengie mikubwa mikubwa,ili watu wapate kazi,kampuni zipate kazi,watu wawe na uwezo wa kulipa kodi,Kampuni ziwe na uwezo wa kulipa kodi,serikali iwe na uwezo wa kukusanya kodi..:-"Mzunguko wa Pesa"..

Mkuu,Sera za serikali ndio inayoinua uchumi wa nchi,Sera za serikali ndio zinazo inua uwezo wa maisha wa raia wake,Sera za serikali ndio zinazo inua Elimu ya raia wake..,Sera mbovu za serikali ndio zinazofilisi nchi vie vile,...sasa kama unasema serikali sio inayoleta mzunguko wa hela inabidi upime IQ yako mkuu,samahani

Serikali inayoshindwa kuja na sera za kuinua Uchumi wa nchi, hiyo zerikali imefilisika kimawazo,haifai kuongoza,CCM imefilika kimawazo,CCM ni janga la taifa
Hongera " sana uchambuzi mzuri sana "" huyo popoma hawezi kukuelewa aisee"" amekunywa Maji ya Bendera "" huwa anabisha kila kitu "" kwaajili ya manufaa ya chama chake "" ambacho kimejaza " wa chumia tumbo ""
 
"Middle class" ndio wenye "Purchasing Power",Tanzania "middle class" ilikuwa inakuwa wakati wa utawala wa JK,Utawala huu kila kitu kimevurugika, "Middle class" imeanza kunyea (Shrink),.wenye maduka manafunga,wenye makampuni wanahamisha biashara zao nchi jirani..

Wakenya anajitambua sera yao ni "capitalism",juhudi zako ndio zitakazokutoa kimaisha,Tanzania wana sera za kila kitu kiwe kinamilikiwa na serikali,Wakenya wanazungumzia kuitawala anga,juzi tu wamerusha "satellite" angani,Tanzania bado wanaongelea hakuna madawati shuleni..,tukubali tu hawa watu wametupita..
madawati mashuleni" mafuta ya kupikia hakuna...hiii nchi ina watu wendawazimu "" na mbaya zaidi ndio wamepewa na fasi ya kukaimu uongozi
 
Acha CHADEMA ifutwe kwanza! (poking).
Propaganda za Tanzania ni za 'old stone age'. Fuatilia tu miradi inayozinduliwa na mwenge, utaelewa namaanisha mini.
Pamoja na kwamba sifahamu Kenya vizuri, ila kwa Tanzania mambo mengi bado sana!
Hata fuatilia hoja zinazotolewa Bungeni, mtaani ....
Angola nayo inatuacha parefu.
Hapa Angola imejichomekaje..??? Any reason ?
 
madawati mashuleni" mafuta ya kupikia hakuna...hiii nchi ina watu wendawazimu "" na mbaya zaidi ndio wamepewa na fasi ya kukaimu uongozi
Hawa jamaa wamekaa miaka mingi madarakani,wamaenza kujiona wao peke yao ndio wenye uwezo wa kutuongoza watanzania,wanauwezo wa kuwafanyia watazania chochote wanachotaka kwani wanajua wao ndio wenye uwezo wa maamuzi ya mwisho..

Wenzetu nchi zilizoendeke chamacha siasa hakiwezi kukaa madarakazi zaidi ya miongo miwili,usalama wa taifa,vyombo vya ujasusi(CIA),FBI na vyombo vingeni vya umma itafanya kila njia chama hakitawali miongo miwili,hii imetengenezwa kwa makusudi,wenzetu wanajua kuwa chama kikaa muda mwingi kwenye madaraka mwisho wake ni kutengeza udikteta..

Tizama sasa Tanzania tulipofikia,Tanzania imekuwa nchi ya "Kifashist",Ufaschisti maana yake serikali ina kontrol vyombo vyote vya umma,hizi sasa Tanzania Bunge ni la CCM,Polisi ni la CCM,Jeshi la CCM,Usalama wa taifa ni wa CCM,Mahakama ni ya CCM,sasa wanafanya kila njia kukontroli media..
"Full fascism "

Ndio utakuta sasa Tanzania Waziri anatolewa bastola hazarani hamna anaekamatwa,wanasiasa wanapigwa rissasi mchana kweupe hakuna aliekamtwa,watu wanaokotwa wamefungwa kwenye viroba pwani wakiwa wamekufa hakuna anaekamatwa,waandishi wa habari wanapotea hakuna anaekamatwa,..

Inasikitisha kuona nchi poa yenye watu poa kama Tanzania imefikia hivi,kwasababu tu walioko madarakani hawataki waondoke,wanang'ang'ani madaraka, wanataka wakae madarakani kwa njia yoyote ile,..

Uliona yale maandamano hewa yalivyogharamiwa yasifanyike Mkuu,majeshi yalimwaga barabarani,na kweli hawa watu wangeliua raia,kwani wameamua wake madarakani kwa njia yoyote ile,hata kwa kuua raia ...

Lakini bado najipa moyo kwani wahenga wamesema hakuna lisilo kuwa na mwisho,God Bless Tanzania,God bless Tanzanian,for the love of the nation one day we will see the light..
 
Naunga mkono hoja Mkuu,.."Purchasing power" hili ndio tatizo la Tanzania,Tanzania hamna mzunguko wa pesa,watanzania masikini,Sera za uchumi za serikali ya Tanzania inafikiri kuzidisha kodi kwa wafanya biashara ndio njia bora ya kukuza uchumi inasahau kuwa bila ya wananchi kuwa na pesa nani atanunua hizo bidhaa madukani!??

Kodi kumbwa kwa wafanyabiashar, wananchi hawana Pesa matokeo yake,maduka yanafungwa serikali haijui ukusanye kodi wapi,sasa tunawasikia wakuu wa mikoa na TRA wanawaomba waliofunga maduka wafungue,waliohamishia biashara zao nchi jirani wazirudishe Tanzania,hata hao wafanya biashara watafungua na kurudsha biashara za Tanzania nani atanunua bidhaa..

Njia zote za kufanya Pesa zizunguke wamezifunga,kampuni binafsi haziwezi kufanya kazi na vyombo vya serikali kama Jeshi na Magereza,..wafaayakazi wa serikali hawawezi kufanya vikao vyao kwenye hoteli za mtu binafsi,..Mabaa yanafunguliwa kwa muda fulani,.nk,kila kwenye kuleta mzunguko wa Pesa wameziba...,hivi sasa baadhi za bidhaa ziepanda,mfuta,Sukari ..nk

Vipi Uchumi utakuwa!!? Uchumi hauwezi kukua kama hakuna mzunguko wa Pesa kama hakuna "purchasing power"....huwezi kuwafanya raia wa nchi yako wawe masikini halafu utegemee ukuwaji wa uchumi.
Hivi kwa sera za kapok wananchi kipato na lumina bombadia ndo italeta purchasing power
 
Acheni kulinganisha faida za makampuni tu, linganisheni na tozo wanazotoa kwa wateja wao.
 
Back
Top Bottom