Uchumi unaanguka wakati Barclays wanafungua matawi nchini!

Mimi furaha yangu kila siku ni kusikia habari kama hizi......

Sio Mara bank imefirisika,Mara viwanda vimepunguza wafanyakazi...........

Nikisikia taarifa ya uwekezaji mpya ndio furaha yangu.......

Nikisikia kampuni imefirisika ndio hasira zangu...........

Tupende kufurahia mazuri na kukosoa mabaya sio kila kitu kusifia au kila kitu kukosoa........
Sidhani kama hicho bado ni kipimo cha kuona kuna kukua kwa uchumi. Upo mfano mzuri kuwa Baclays wanaweza kuwa na tawi moja kubwa lenye wafanyakazi 100, kisha wakaamua kulivunja na kufungua matawi matatu ndani ya mji huo huo yenye watumishi 25 kila moja na kupunguza watumishi kwenye ajira 25.
Hicho kitendo hata kama mtasema sasa Benki ina matawi matatu badala ya moja kiukweli lazima kuna jambo nyuma yake kuhusu maendeleo ya benki hiyo na athari nyingine ni kuwa ajira 25 zimepotea
 
Hii ya kufungua tawi DSM ambako tayari yapo matawi yao kibao sioni kama ni kiashiria cha kukua Uchumi au ndio Modern Economies kwa nyie wataalam aaaaah nilidhani wamefungua Muleba na Ilula
 
Ajabu ni kuwa Barclays kipindi cha JK ilifunga branches nyingi sana. Hata mimi hapo sielewi.
 
Majibu ya jazba ni dalili ya kuishiwa hoja. Kama kufunga tawi sio uchumi kuangaka iweje kufungua tawi iwe uchumi kuimarika?

sasa si ujibu wew povu la nini kama kuanguka kwa mabank na mahoteli , unakimbilia huku kuja kueleza uchumi unaanguka ni kwa nin isiwe kinyume chake
 
Hio ni branch imehama kutoka pale karibu na itv bagamoyo road hio hio ndio wamehamia hapo Alpha house.

Ukienda kwenye hio branch utakuta notice kuwa wamehamia Alpha tower.
 
Ndiyo maana nilipoenda kwenye brunch yao ya pale Kinondoni nikaambiwa wamehama kumbe mmehehehe amia hapo
 
Kanywe maji ukalale basi, umafikiri ni kwanini hotel zinauzwa sana?

Je,wananchi wanalalamika unafiki kuhusu mzunguko wa fedha kutokuwa mzuri?

Nafikiri aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Fedha zimeadimika sana period!
Eti nikalale.

Tatizo lako unadhani dunia inaishia Tanzania na kwa maana hiyo huwezi kujua kama kuna sehemu zingine ndio kunakucha huku sehemu zingine kukiwa ni mchana. Kajifunze kwanza somo la geography kabla ya kuanza kujibu hoja za kiuchumi.

Mimi nimekupa mfano wewe unaleta mipasho.
 
Hawa barclays pia robo ya tatu wameripoti hasara ktk financials zao,iweje uamini kuwa hilo tawi ni kiashiria cha uchumi kuimarika.
Unajua hilo tawi wameanza lini kuliandaa?
Hao hao barclays uwaulize mabanda yao waliyokurupuka nayo yaliishia wapi?
 
Eti nikalale.

Tatizo lako unadhani dunia inaishia Tanzania na kwa maana hiyo huwezi kujua kama kuna sehemu zingine ndio kunakucha huku sehemu zingine kukiwa ni mchana. Kajifunze kwanza somo la geography kabla ya kuanza kujibu hoja za kiuchumi.

Mimi nimekupa mfano wewe unaleta mipasho.
Nadhani post #25 inakupa majibu yote. Sasa kama kuhamisha branchi toka sehemu moja kwenda nyingine ni kukua kwa uchumi basi hii mupya!
 
Wamefungua tawi jipya? Nani kakwambia? Wenzio wamehsmisha Tawi lililokuwa Pale Mwenge ITV ndo wamelipeleka huko.Wakati mwingine uwe unafanya uchunguzi kabla ya kuja kutapika huku
 
Tanzania ni nchi za maajabu sana!

Ukisoma kwenye baadhi ya mitandao unaweza kudhani nchi iko mbioni kufirisika!

Ukiwatafuta baadhi ya wanasiasa wanakuambia uchumi unaanguka.

Ukiwatafuta wachumi wanakuambia uchumi unaimarika.

Ukienda kwa wafanyabiashara makini kama Barclays ambao biashara zao zinategemea sana uchumi wa mtu mmoja mmoja nchini wanakuambia mazingira ya uchumi nchini ni mazuri ndio sababu wanaendelea kufungua matawi ya benki katika sehemu mbali mbali hapa nchini.

Nani anayesema ukweli?

02.JPG

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed (katikati), Afisa Usambazaji wa Barclays Africa Group Limited, Vimal Kumar (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara Reja reja wa benki hiyo nchini, Kumaran Pather wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la kisasa la benki hiyo lililopo katika jengo la Alpha House kando ya Barabara ya New Bagamoyo, jijini Dar es Salaam.
05.jpg

06.JPG

Baadhi ya maofisa wa Barclays wakiongozwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Biashara Reja reja wa benki hiyo nchini, Kumaran Pather (kushoto), wakiwa na baadhi ya wateja na wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi hilo uliofanyika tarehe 19 Desemba 2016.

The new branch is located at Alpha House on Ali Hassan Mwinyi Road. The bank said it will remain in the country following confidence in the growth and direction of Tanzania's economy.

Tanzanian business is the strongest Barclays franchise in Africa, the bank said in a statement yesterday. "Barclays is fully committed to serving the Tanzania's market. As you may have seen in the past two weeks.

With the opening of the new branch means we can leverage on the social and economic development in Dar es salaam region and beyond," said the bank's Managing Director Abdi Mohamed.

Mwezi wa sita walifungua pia matawi katika Jiji la mwanza.
01.JPG

03.JPG
ukifunga supermarket (macro) halafu ukafungua groceries shops (micro) utasema biashara yako inastawi?
 
Hali ya uchumi ni mbaya leo tawi la NBC UDSM ilikuwa kama unataka kutoa ndani zaidi ya laki tano ilikuwa inabidi uwapishe kwanza wengine wanaochukua kiwango kidogo.We unasubiri kwanza wengine wadeposit
 
Mbona menejimenti ya juu wote ni wahindi ambao siyo waTZ? Wamegundua namna ya kuchota dola zetu ambazo hazina uthibiti.
 
Walichokifanya Barclays bank ni kufanya branc merging hali yao ni mbaya sana wamefunga tawi la kinondoni pale karibu na kinondoni muslim, mwenge , na pale mikocheni chama wameshindwa kuendesha ndo wamefungua tawi ilo moja ... mimi ni client wao na nikifanya mihamala yangu sana hapa kinondoni na kwa sasa washafunga rasmi wametoa mpaka atm .... pia magomeni mapipa pale tawi nalo wamefunga
 
Matawi mawili kwa mwaka Mnasema wako confident na uchumi Barclays ambayo Hadi Mo Alitaka inunua baada ya kuendeshwa kihasara...haya Bana tutasikia mengi
 
Back
Top Bottom