Uchumi Tanzania utaendelea kuporomoka 2017/18

Alpha M

Senior Member
Nov 8, 2016
165
155
Habari za jioni mtanzania mwenzangu, poleni kwa majikumu.

Kwa kuanza kabisa, inabidi tukumbushane kwamba benki za biashara ni vilainishi katika ukuaji wa uchumi duniani kote. Mfumo mbovu wa benki hizo unaweza sababisha "economic depression", mfano mzuri ni ule wa Marekani mwisho wa mwaka 2007. Kwa afupi, benki za biashara zilitoa mikopo mingi ya nyumba ambayo haiwezi kulipika. Wananchi walijipatia nyumba mathalani vipato vyao haviwezi kulipa mikopo hiyo.

Kwetu hapa Tanzania, mnamo mwezi Aprili benki kuu ilishusha "minimum reserve requirement" kiwango cha chini kinachotakiwa kubaki benki baada ya kutengeneza mikopo. Mfano "minimum reserve requirement" ya asilimia 10 katika kila Tzs. 10,000/- inamaana Tsh. 1,000 inabaki katika shelfu za benki bali zile Tzs. 9,000/- zinakua mikopo kwa wanaohitaji.

Faida ya mbinu hii ni kutengeneza mikopo ili kusaidia wawekezaji kuongeza uzalishaji. Shida yake ni kwamba, kiasi kinachobaki benki ambacho wateja wanawezatoa kupitia ATM na kadhalika kinapungua.

Tatizo hili lipo mpaka sasa ambapo mabenki mengi wanalalamika hawana pesa. Na sababu haswa ni kwamba mikopo iliyopo hailipwi itakiwavyo, ndiyo maana tunasikia makampuni kufungwa na kufilisiwa.

Kitu cha ajabu zaidi, BOT(Benki Kuu ya Tanzania) imeshusha "minimum reserve requirement" kutoka 10% hadi 8% aprili mwaka huu ili kuongeza mikopo kwa kufumba macho mikopo iliyopo haifanyi vizuri (hailipwi kwa wakati). Hii inarudisha nyuma mfumo huuhuu ambapo mnamo 2015 walipandisha "minimum reserve requirement" kutoka 8% hadi 10% ili kukabiliana na mfumuko wa bei. Kwa kiasi fulani walifanikiwa kushusha mfumuko wa bei mwishoni mwa 2015 mpaka katikati 2016 ndipo uchumi ukaanza kuzorota.

Wakati mwingine wanaweza sema mikopo nafuu ambayo ndio sababu kuu ya kushusha asilimia hizo mbili, lakini tatizo sio mikopo ya bei rahisi. Tatizo lipo kwa fedha zilizopo mifukuni mwa watu zinazowawezesha kununua bidhaa. Hapa Benki kuu imeingia chaka.

Tutegemee nini labda? Haya ni maoni binafsi kama mwanafunzi wa uchumi.

1. Mabenki zaidi kufungwa; mikopo inapokua hailipwi kwa muda sababu ya riba kuwa kubwa, haitakiwi utengeneze mingine ya bei rahisi bali utengeneze mazingira ya biashara kuwa mazuri.

2. Uchumi kushuka zaidi. Hapa naongelea uzalishaji na mauzo, wafanyabiashara wote huuza na kuzalisha kulingana na mahitaji. Tatizo lililopo la ukosefu wa pesa na mfumuko wa bei haliwezi tatuliwa na mishahara itakayoletwa na mikopo hii mipya ya bei rahisi. Kama wateja hawana fedha za kununua bidhaa, mauzo yatashuka na uzalishaji kudoda.

Nini kifanyike? BOT itafute namna ya kurudisha pesa mikoni mwa watu.
 
Kama sekta binafsi itakamuliwa,na hili la kodi za majengo na kodi za viwanja,na nyingine zitakazobuniwa,naiona kabisa ccm ikitangulia mbele ya haki.
 
Kama sekta binafsi itakamuliwa,na hili la kodi za majengo na kodi za viwanja,na nyingine zitakazobuniwa,naiona kabisa ccm ikitangulia mbele ya haki.
Itategemea zaidi wataenda kuwekeza wapi hayo mapato. Kama sekta watakayoilenga itakua na long term low rate return (mfano ATC na SGR) kwakweli tuanze kukaza mikanda zaidi.

Hili sio suala la siasa, ni wale wasomi wa BOT na Wizara ya Fedha ndio wahusika.
 
Back
Top Bottom