nijuavyo mimi hiyo ni njia moja wapo ya kuthaminisha hiyo bidhaa ya plastic ili kupunguza kusambaa kwa mifuko hiyo coz mtu atakuwa ana uchungu nao na atautumia kwa shughuli nyingine.
Sawa kabisa. Wanafuata kanuni ya kulinda mazingira iitwayo " Mchafuzi kulipia uchafuzi" - Polluter Pay Principle. Hii ni kawaida sana kwenye nchi zilizoendelea kama hapa Ujerumani.
Hali hii nimeikuta leo nilipokwenda kupata mahitaji yangu.Mteja baada ya malipo anaulizwa kama anahitaji mfuko.Mfuko huuzwa 200.
Sio uchumi tu, nafikiri ni Supermarket zote wamepewa agizo toka serikalini. Niliona hilo tangazo TSN Supermarket na Game Supermarket