Uchumi Supermarket imeamua kuwauzia wateja wake mifuko

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
28
Hali hii nimeikuta leo nilipokwenda kupata mahitaji yangu.Mteja baada ya malipo anaulizwa kama anahitaji mfuko.Mfuko huuzwa 200.
 
Oyaa Mkuu Mbeyaman ,Halafu wenye vipesa vyetu vya upatu huko Supermarket mnaenda kutafuta nini.

Yaani 200 ya mfuko unapiga kelele?

Hembu tuzipe heshima Super markets,kila kitu kina hadhi yake.

Kuna watu juzi wamelalamikia mia mia,leo mia mbili za mfuko.

Kuna watu wengine huwa wakienda wanafanya kusudi pale na masifa kibao,wanaomba mifuko teleee kila bidhaa anataka ipewe mfuko wake.Wasumbufu sana,sasa ni bora kuweka huu utaratibu ili kufidia gharama za mifuko.
 
nijuavyo mimi hiyo ni njia moja wapo ya kuthaminisha hiyo bidhaa ya plastic ili kupunguza kusambaa kwa mifuko hiyo coz mtu atakuwa ana uchungu nao na atautumia kwa shughuli nyingine.

Sawa kabisa. Wanafuata kanuni ya kulinda mazingira iitwayo " Mchafuzi kulipia uchafuzi" - Polluter Pay Principle. Hii ni kawaida sana kwenye nchi zilizoendelea kama hapa Ujerumani.
 
Sawa kabisa. Wanafuata kanuni ya kulinda mazingira iitwayo " Mchafuzi kulipia uchafuzi" - Polluter Pay Principle. Hii ni kawaida sana kwenye nchi zilizoendelea kama hapa Ujerumani.

Aisee we Muota Ndoto upo Ujerumani au upo mbagala umeota upo Ujerumani.

Guten mogan(hahaha hapo nachapia cha huko sasa)
Guten naght
Aufidezen
 
Hali hii nimeikuta leo nilipokwenda kupata mahitaji yangu.Mteja baada ya malipo anaulizwa kama anahitaji mfuko.Mfuko huuzwa 200.

Sio uchumi tu, nafikiri ni Supermarket zote wamepewa agizo toka serikalini. Niliona hilo tangazo TSN Supermarket na Game Supermarket
 
Sio uchumi tu, nafikiri ni Supermarket zote wamepewa agizo toka serikalini. Niliona hilo tangazo TSN Supermarket na Game Supermarket

Ni kweli nimekutana nalo hilo nakumat na imalaseko ila pale shopaz plaza hawakuniuzia
 
Safi sana. Twende na vikapu vyetu sasa, plastics zimejaa sana mtaani na haziozi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom