UCHUMI supermarket acheni hii tabia chafu mnatuboa!

Stoudemire

JF-Expert Member
Mar 24, 2012
839
207
Wanandugu,

Mimi huwa naenda pale Uchumi siku za weekend kununua mahitaji kadha wa kadha. Lakini kuna katabia pale ambacho huwa kinanikera sana. Mara nyingi wale cashier wao hawana chenji ndogo ndogo. Yani kila nikienda naacha sh 50, 100 au 200 kwa kudai eti hawana chenji. Na hii inanikuta kila siku nipitapo pale.

Sasa najiuliza ni uongozi umeamua usiwape chenji makusudi ili iwe ni sababu ya wao kupata "TIPS" au ni wao wenyewe wanaficha chenji ili wale fedha zetu sisi wavuja jasho?

Nawasilisha!
 
Aisee nami ishanitokea pale Shoprite Arusha, tuko kny Que alafu cashier anatangaza watu waje na chenji kamilia, kama huna imekula kwako.
 
tukiwa na umoja hii tabia haiwezi kupata nafasi. Tatizo ni ulimbukeni na haraka zetu. Najua watu wengi akiingia pale Quality au Mlimani city anajisikia aibu kukomalia sh. 200 au 500, lakini akienda duka la Mangi mtaani anakomaa kinoma.
Ulimbukeni tabu sana.
 
Baadhi ya supermarkets zimeweka boksi la pipi pale cashier. Unachukua pipi thamani ya change ndogo iliyosalia.
 
tukiwa na umoja hii tabia haiwezi kupata nafasi. Tatizo ni ulimbukeni na haraka zetu. Najua watu wengi akiingia pale Quality au Mlimani city anajisikia aibu kukomalia sh. 200 au 500, lakini akienda duka la Mangi mtaani anakomaa kinoma.
Ulimbukeni tabu sana.

(kwenye red) Ha ha ha ha nimecheka sana!
 
Kweli shoprite ya Arusha wanakatabia hicho. Ukienda shop rite ya kamata utafurahi hata iwe 10 ni mpya inang'aa.
Waarusha hatabidhaa ni juu kidogo wanahisi sisi sote ni watalii ama wa UN ama wanaapolo waliopiga mawe.
 
Back
Top Bottom