UCHUMI SHIRIKISHI-falsafa mpya nchini ya PROF.LIPUMBA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UCHUMI SHIRIKISHI-falsafa mpya nchini ya PROF.LIPUMBA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MWIBA WA KATANI, Mar 12, 2012.

 1. MWIBA WA KATANI

  MWIBA WA KATANI Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo Prof.Lipumba ameongea na vyombo vya habari na kuelezea kuwa katika utafiti aliokuwa akiufanya imebainika uchumi shirikishi ndio njia pekee yakusaidia nchi zenye utajiri mwingi kama tanzania.Alitoa mfano ili kufafanua kwamba endapo kila mtanzania akifunguliwa akaunt na kupatiwa asilimia fulani ya mapato yanayotokana na madini,ges na maliasili nyingine nchini na asilimia fulani akawa anakatwa kodi na serikali,itamfanya mwananchi kuwa makini kwa maliasili yake na kuibana serikali kuhusu maliasili hizo.
  DSC08655.JPG
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Amezungumzia uchumi tu? kama kuna lolote amezungumzia kuhusu anguko la chama chake tujuze pia.
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapo nilipo bold unatafuta ugomvi na CCM. Ikiwa kama serikali inashindwa kutumia mali zake ipasavyo na kuachia watu wanajivunia maliasili kwa kupewa dola 4,000 na serikali kujikuta inashindwa hata kulipa wananchi wanaofanya kazi kwa wakati iweje kila mwananchi afunguliwe account yake?. Tanzania hata tungekuwa na reserve ya mafuta 10% of the world bado mantang'au wachache wasingeona umuhimu wa kulipa wananchi jobless allowances.

  Tatizo kubwa tanzania ni la kimfumo, yaani watu wachache wanaojiita CCM wamewahi na kukalia hazina ya taifa na kuitumia kwa faida ya kuendelea kuwa madarakani. Wanagawa umasikini na njaa halafu wakati wa chaguzi wanagawa chakula na alfu tatu tatu ili wapigiwe kura.
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  I think alikuwa anatolea mfano wa uchumi shirikishi kutumia mfano wa kufungua account. Ila nilivyoelewa mimi point yake kwamba, wananchi wakiona kuna manufaa ya moja kwa moja wanakuwa makini kulinda rasilimani. Mfano ukiwachangisha watu mtaani kwako kutengeneza mfereji na wakatumia nguvu zao na serikali ikawapa 50% hata siku moja hatafumbia macho wakimuona mtu anatupa taka. Kuliko serikali ikienda pale na 100% wakatengeneza huo mfereji.
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Rangi za CUF na Chadema ni sawa?
   
 6. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,438
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Uchumi shirikishi uanzie kwanza na kuondoa fikra mgando za watumishi wengi wa serikali kwamba mwekezaji ni mzungu/mchina/mhindi na mwarabu. Kuondoa kabisa rushwa miongoni mwa watendaji wa serikali ukianzia na jeshi la polisi.

  Kutambua umuhimu wa kuzalisha matajiri wamatumbi, kutoka matajiri wasasa na mifumo yao wanayoendeshea viwanda vyao inajenga kuzalisha mameneja weledi miongoni mwa watu wao na sio umma wa watanzania. Kwa maana hiyo ni vigumu sana kuzalisha mmatumbi industrialist labda cinema super star. Viwanda ndio vitakavyo tutoa, kuwaachia wahindi peke yao uchumi hauwezi songa na wao wataendelea kukaa upanga wamatumbi watasogea zaidi mpaka chole.

  Wanasihasa na wachumi nao pia waingie katika ujasiliamali, wasiendelee kupiga hela kwa kukaa na kuongea tu, kama sehemu ya watanzania wachache wenye kipato kikubwa kidogo wajikusanye na kuanzisha viwanda. Wahindi sasa wanakimbilia kuwekeza nje ya Tanzania kutoka kuwa huko kuna fursa zaidi za kibishara na mazingira mazuri ya kufanya biashara.

  Profesor sasa afanye tafiti za humu ndani ili kusaidia kukua kwa secta binafsi ya wazawa, isiwe batiki, jam na vinyago.
   
 7. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi hii mafisadi walivyowengi hawezi kukubali kwani itapunguza ulji wao.Kwao hii ya kimya kimya ndiyo safi
   
 8. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeona Chanel 10 muda mfupi uliopita Amesisitiza Nidhamu lazima izingatiwe ndani ya vyama ili kuunda vyama imara nchini,pia kasema waliofukuzwa CUF wamefukuzwa kihalali
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  angesema hawajafukuzwa halali na yeye wanegemfukuza
   
Loading...