Uchumi kanda ya ziwa waongezeka kwa asilimia 13

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,907
2,768
Uchumi wa mikoa ya kanda ya ziwa umeongezeka kwa asilimia 13, kutoka Sh20.6 trillion 2014/15 mpaka trillion 23.4 2015/16.

Sekta zilizochangia ukuaji huo ni madini, biashara, utalii na fedha. Watu waliotembelea mbuga za wanyama wamechangia pato kwa asilimia 21.3.

========

Uchumi wa mikoa ya kanda ya ziwa kwa mwaka 2015/16 uliongezeka kwa asilimia 13 na kufikia Sh23.4 trilioni kutoka Sh20.6 trilioni 2014/15.

Ukuaji huo uliochangiwa na Mkoa wa Mwanza kwa asilimia 36.1, umesababisha kuongeza uchumi wa Taifa kwa asilimia 25.7.

Meneja wa Uchumi Mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani Mwanza, James Machemba alisema kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), sekta zilizochangia ukuaji huo ni madini, biashara, utalii na fedha.

Alisema mauzo ya madini nje ya nchi yaliongezeka kwa asilimia 1.4 hivyo kufikia Dola 1,329.5 milioni za Marekani katika mwaka ulioishia Juni 2015/16 kutoka Dola 1,311.3 milioni mwaka 2014/15.

Alisema watu waliotembelea mbuga za wanyama walisaidia kuongeza pato la mikoa ya kanda hiyo kwa asilimia 21.3.

Chanzo: Mwananchi
 
How about Mtwara? Singida? Tabora? Tanga? ... Kweli Ukarimu huanzia Nyumbani ... CIA = Chato International Airport
Uchumi wa mikoa ya kanda ya ziwa umeongezeka kwa asilimia 13, kutoka Sh20.6 trillion 2014/15 mpaka trillion 23.4 2015/16.

Sekta zilizochangia ukuaji huo ni madini, biashara, utalii na fedha. Watu waliotembelea mbuga za wanyama wamechangia pato kwa asilimia 21.3.
 
vipi kwetu kwenye gesi uchumi umepanda au umeshuka,...

Njaa inatunyemelea huku umakondeni , Naona Ngosha unasimamia unachokisimamia..!
 
Uchumi wa mikoa ya kanda ya ziwa umeongezeka kwa asilimia 13, kutoka Sh20.6 trillion 2014/15 mpaka trillion 23.4 2015/16.

Sekta zilizochangia ukuaji huo ni madini, biashara, utalii na fedha. Watu waliotembelea mbuga za wanyama wamechangia pato kwa asilimia 21.3.
Izo pesa unazoongelea ni mapato, au kodi?
 
Juzi tu mmekuja hapa eti Mwanza ni masikini kuliko hata pwani Leo uchumi wa kanda ya ziwa umeongezeka?...

Nonsense
 
Watetea mafisadi chadema, mjue kabisa Magufuli siyo saizi yenu..

Kulialia kwenu kwenye mitandao ya kijamii hakuwezi kubadili jiwe kuwa barafu.

Chadema, chama la hovyo kuwahi kutokea duniani
 
Kanda ya ziwa ipi? Hiihii tuliyonayo? Inawezekana labda kwa hayo madini kwani pato lake wananchi wa kawaida wanasikia kwenye taarifa tuu zinazosomwa hata huo utalii kwani Mahoteli yanalipa kodi huko juu. Lakini kwa uchumi wa mwananchi wa kawaida hapo tusidanganyane. Hali ni mbaya kuliko ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita.
Isije kuwa ni takwimu kama zile za TRA
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom