Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,393
Mpaka miaka ya hivi karibuni mambo ya uchumba yalikuwa hayawezi kufanyika bila ya kuwepo wazazi na familia. Mitoko mingi na kualikana ilifanyika majumbani wakiwapo wanafamilia wote. Kujitokeza kwa usafiri na ugunduzi wa magari kumesaidia sana kuharibu utaratibu mzuri wa mitoko ya kimapenzi na uchumba kwa ujumla.
Magari si tu kwamba yamesababisha mitoko isifanyike majumbani, lakini pia yamesababisha ifanyike bila kuwashirikisha wazazi. Gari siku hizi limebadilishwa kuwa kitanda kinachotembea chakufanyia ngono wakati wa mitoko.Vijana wadogo sio kwa hapa nchini tu bali hata huko katika nchi za magharibi na ulaya wamejinyakulia uhuru mkubwa mno kutoka kwa wazazi wao, na kuzipondoponda chini mila na desturi ambazo ziliweka misingi imara katika kulinda maadili ya uchumba kwa vijana.
Lakini pia Teknolojia mpya na matumizi yake mabaya nayo imechangia kwa kiasi kikubwa kusambaratisha mila na desturi zetu zilizokuwa zikilinda maadili yetu. Simu na mitandao ya mawasilano, ni moja ya mabadiliko yaliyotufikisha hapa.
Imani na misingi ya kidini zilianza kupata mashambulizi makali toka kwa wasomi na wanafalsafa wa karne na karne. Charles Darwin na wafuasi wake walianza mashambulizi dhidi ya imani ya Mungu na mamlaka yake. Na hii ilipelekea wanatheolojia wa Ulaya kuanza kulegeza kamba kwa mambo muhimu ya kidini.Kupuuzwa kwa mila na desturi na maadili ya kidini kumechangia sana kuharibu tabia za vijana ikiwa ni pamoja na mambo ya urafiki, uchumba hadi ndoa.
Ni baada ya vita ya kwanza ya Dunia ndipo saikolojia na Sosholojia vilileta njia ya Kisayansi iliyoheshimika zaidi, nakuanzia hapo mamilioni ya watu walianza kuamini mafundisho ya akina Sigmund Freud, Margaret Mead na Alfred Charles Kinsey.