Uchumba umevunjika baada ya kujua mdogo wake alitembea na mimi

The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
9,395
20,630
Mchumba wangu, mama wa mtoto wangu kakata kamba, hataki mawasiliano wala upatanisho. Aliniandikia ujumbe mmoja tuu akieleza kuwa, majukumu yangu kwa mtoto nifanye kama kawaida, chakula, matibabu na ada ya shule, nikitaka kwenda kumchukua nimchukue ijumaa jioni nimrudishe jumapili jioni.

Kisa ni mdogo wake, aliyekuwa anaenda chuo, alipitia kwangu tena kwa ombi lake dada mtu aje akae wiki 2 na huyu mtoto wa dada yangu aliyemaliza kidato cha nne,sababu yeye alikuwa anasafiri na asingeweza kumuachia nyumba. Dada wa kazi ni wa kuja na kuondoka

Huyu binti alivyofik alikuwa ana mitego sana, nilivumilia lakini nikashindwa, hata mpwa wangu alikuwa anayaona haya kiasi mda mwingine anamwambia kaa vizuri au anamletea kanga bila kujali hata mtoto wangu yupo hapo ilifikia kipindi akawa anamchukia kabisa, na huyu mpwa ndiye atakuwa kamwambia shangazi yake maana hiyo siku shetani alivyopita nilimpa hela aende movie lakini tulivyotoka ku do tukamkuta sebuleni

Tulikuwa tumepanga kuoana Mungu akijalia na alikuwa hataki kuish na mimi bila ndoa kanisani, sasa nimelivuruga baada ya mdogo wake kutembea na mimi, hata mama yake na kaka zake hawapolei simu zangu anatepokea ni huyu binti tuu, na yeye anasema ha regret kilichotokea

Nimekwama wakuu, shughuli haziendi, moyo unauma nifanye nini, yani huyu binti yangu naona hata aibu kumuuliza kama yeye ndio kasema au la,
 
Kama kulikuwa na mapenzi ya kweli. We tulia achana na huyo shemeji yako kabisaaa. We tulia tu nyumbani, hata mtoto uwe unamwagiza mpwa wako akamchukue na kumrudisha. Iko siku mambo yatakuwa sawa. Just give her time to take all that in. Ni mbaya sana, sawa na wewe usikie mdogo ako kamgonga mkeo mtarajiwa, lazima usitishe ndoa. Ila na yeye alikosea alipomtuma mdogo ake ambaye hajatulia ukae naye, i mean WTF? Just let her cool off usimsumbue utaharibu!
 
ushauri mzurii 100%
 
Asante kwa ushauri huu mkuu
 
What a stupid nasty girl? Ila jamani makaka zetu inabidi na nyie muwe na simile.! Kweli mdogo wa mwenzio? When will you learn not every hole is worth ..........Kuna vitu vya kusamehe ila vingine duh!!!!!!!!!!
 
Hakuna haja ya kuumia moyo wakati bado haukuwa tayari kwa kuoa. Endelea kuchovya chovya mkuu ukitosheka utatafuta wa kuoa.
 
Back
Top Bottom