Uchumba sio ndoa muda wowote unavunjika hivyo ishi na mchumba wako kwa akili

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Jamani,hii ni kengele ya tahadhari kwa wapenzi mlio katika mahusiano zaidi ya miaka mitatu mkiwa wachumba.

Kibongobongo tunaita uchumba sugu ambao umeshaliza watu wengi kwani katika kipindi cha uchumba vijana hujifanya wanaekeza kwa wachumba wao vitu vya gharama, wapo wengine walizalishwa wakakimbiwa, wapo waliosomesha, waliofungulia biashara wenza na kuamini kwa kuwafanyia wakiamini kwa kufanya hivyo watapedwa zaidi na kuwekeza kwao wakuamini ndiyo security ili mpenzi wake asibabaike na mwanamke au mwanaume mwingine.

Usijifariji kuwa mtaoana baada ya kumpa mpenzi wako kila anachokitaka, hiyo ni sawa na kufuga kunguru wakati unajua kunguru hafugiki

Hivyo tunakumbushana tuu uchumba sio ndoa muda wowote unavunjika.
 
Ndoa zenyewe zinavunjika.Yaan hapo ungesema tusioe na kuoana tu ...sikuhizi mapenz ya dhati hakuna umebaki usanii
Kuna tofauti kubwa kati ya ndoa ya uchumba katika ndoa ni realistic ila uchumba ni unrealistic

Always kama kijana ni lazima utofautishe maisha ya ndoa na uchumba ndio maana kuna vitu utakiwa ufanye ukiwa ndani ya ndoa
Na ndio maana

1.Kuna tofauti kubwa kati ya kumsomesha mchumba na kumsomesha mke au mume

2.Kuna tofauti kubwa Kati ya kuzaa ndani ya ndoa na Kabla ndoa coz

2.Kuna tofauti Kati ya kumuhudumia Mwana ndoa mwenzako na mchumba wenzako
 
Kwa mahusiano kabla ya ndoa,
Wanaume tuishi na wanawake kwa timing ya hali ya juu Sana(mithili ya kunguru)

Mpe mchumba wako kile cha ziada,
Namaanisha kile ambacho hata mkiachana hakitakuuma.

Na sio kile unachokitegemea.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye ndoa,
Ruksa kujitoa kwa hali na Mali maana hata akizingua mtagawana.

Angalau utafidia nusu hasara.

Ila sio kwenye uchumba.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nini kifanyike?
Kila unachokuwa unampatia mchumba wako kuwa unaweka kumbukumbu, ili akikukimbia tu mpeleke mbele ya sheria.
Sheria za bongo zinaruhusu mtu kurudishiwa vitu vyake/gharama zote alizotumia kumhudumia/kumpatia wakat wa uchumba wenu, baada ya uchumba kuvunjika.

Pili, ni wazazi, walezi, watumishi wa dini wajitaidi kuwafundisha vijana kuhusu uchumba& mahusiano na thamani ya ndoa mara baada tu ya kijana kufikia umri wa kubarehe/kuvunja ungo
 
Na kaz anayo
Masikini naona hata huruma..embu tazama, Anakuja Mwanaume mwema, mwenye dhati anayehitaji umzalie Mabinti warembo na vijana wake ukiwa kama mke wake.

Anakuita moyoni mwake, lkn weee toka siku yakwanza, Unamuishi kwa hofu. Bila upendo, kwa hisia zako mwenyewe zilizopita.

Je aliyesema msiyaanze mapenzi mpaka wakati wa ndoa, Alikua Sahihi???

Kuyaanza mapenzi mapema, kumekuumiza nakukuondosha Moyo wakupenda, nabadala yake umebakiwa na Moyo wa Kusukuma Damu!!

Athari ya kua ivo ni moja...Mwenye dhat atakuja kwako, lkn kwakua unamuishi mguu nje mguu ndani, ataona anapoteza muda, naye atabadilika nakua mguu nje mguu ndani .

Mimi nadhani kwa Age yako ulonayo, ni yakua namtu umpende na Akupende.

Badilika na Umwambie Mungu, akupe Moyo wa kupenda
 
Mpaka naingia kaburini,siwez mpenda MTU kwa dhati...tutaishi tu
 
Mpaka naingia kaburini,siwez mpenda MTU kwa dhati...tutaishi tu
Je unajua kua Raha ya Ndoa pia ni mpendane, mioyo idunde pamoja ?

Unaweza ishi na mwanaume aliyekupenda kwa dhati hata km wewe humpendi?

Je faida yawewe kuingia kwa hayo maisha, ni Kuitwa "Mrs fulan? Ni kuhesabika umeolewa?? Ni kua na kwako ? Ni kua na watoto??.

Mimi naamini unayo nafasi na hujafikia iko kiwango ,semea tu bado hujampata mtu ambaye unaona "He is the One".
 
Back
Top Bottom