Uchukuaji wa Sheria Mikononi, Je ni halali???

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
Wakuu, heshima mbele.... Nimesoma kwenye Thisday la leo kuna picha ya mwanamama amekamatwa (ameshutumiwa) kufanya "shoplifting" pale Imamalaseko. Binafsi nakiri kuwa adhabu aliyopewa ni kumdhalilisha kabisa kwani ameiba labda vimchele etc thamani ya maximum 20,000TZS kisha anapewa adhabu ambayo ni kwa kweli ni ya kinyanyansaji... Nimeshindwa ku copy picha lakini maelezo ni haya:

WHAT A SHAME: A city resident identified as Joyce Alfred Mbilinyi, alias Joyce Agness Mbwatila, is subjected to public embarrassment after being caught in the act of allegedly shoplifting various items at Imalaseko Supermarket in downtown Dar es Salaam yesterday. On her left in picture number (above) is the supermarketas security officer, Ephraim Massawe.

Picha ipo at:
http://www.thisday.co.tz/

Shame on us Tanzanians, hii ni zaidi ya unyanyasaji jamani kwani hakuna Polisi, Mahakama, nk? Je Serikali imeruhusu haya?? Kuruhusu hili manake ni kuruhusu unyanyasaji wa waTanzania.... HAKI ZA BINADAMU TANZANIA MPO???
 
Hiyo ndiyo Tanzania yetu unashangaa nini morani?. Huyo mama atapelekwa rumande, atafikishwa mahakamani na kisha kutupwa jela miaka miwili ama mitatu. Lakini mafisadi wanaoiba mabilioni yetu yanatunzwa, yanabembelezwa na kufichwa.

Tunahitaji kuamka Watanzania wote na kudai haki yetu kwa nguvu.
 
Mtambo, asante sana lakini mimi sipingi/sikatai huyu mama kupelekwa rumande, nakataa yeye kuwekwa pale na tangazo la eti mimi ni mwizi.... NAKATAA KUDHALILISHWA KWA HUYU MAMA..........
 
Mtambo, asante sana lakini mimi sipingi/sikatai huyu mama kupelekwa rumande, nakataa yeye kuwekwa pale na tangazo la eti mimi ni mwizi.... NAKATAA KUDHALILISHWA KWA HUYU MAMA..........

Angeiba kiwalani wangemchoma moto! Yale yale ya kujichukulia sheria mkononi.
 
Angeiba kiwalani wangemchoma moto! Yale yale ya kujichukulia sheria mkononi.

Fundi, hiklo sikatai lakini hata kwenye hizi established institutions/organizations jamani tufanye mambo kienyeji..... Unajua kinachofuata ni nini, "yale ya hausigeli apigwa mpaka kulazwa hospitali sababu aliiba nepi za mtoto" etc........

We just need to have a degree of "Sanity" at all levels jamani................. Is it that hard kwa serikali kuhakikisha haya yanatendeka?? Na kama kila mtu akifanya hivyo, Je Polisi/Mahakama etc vitakuwa na kazi/jukumu gani??
 
Jamani kuna msemo wakisheria unasemwa 'presumed innocent until the contrary proved'. Huu mtindo wa kujichukulia hatua ni mbaya sana, tuna uhakika gani huyo mtu amefanya kitendo kiovu? kwa nini tusisubiri mamlaka zichukue mkondo wake? Upande wa pili inabidi tujiiulize kwa nini huyo mama aliiba? siyo sababu ya kukosa elimu? siyo sababu ya kukosa mtaji? siyo sababu ya kukata tamaa? yote hayo yanatokana na nini kama si ufisadi? Milioni moja ya Chenge ingemsomesha huyo mamaa angeiba kweli? au laki mbili tu angenunuliwa cherehani angeiba kweli?
 
Back
Top Bottom