Uchu wa nyama ulivyopelekea kumkumbatia chui

Ze Rock

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
270
563
Wana jf salaaaam!

Kisa chenyewe.

Kuna siku wazee flan walipita maskani wakasema wanaenda porini kusaka kitoweo, nilivyosikia hivyo kidume mate yakanitoka hata kabla hatujakipata kitoweo chenyewe na kwa vile wale wazee nawajua ni wazee wa kazi hizo sikuwa na wasiwasi kabisa nikajua hapa ni uhakika, tukirudi yaani ni kushinda tu nadambua kitoweo kwa raha zangu. Mara nichome mara nitengeneze za mchuzi ili meadi tu kwenye vyungu hakukosi nyama nyama.

Basi bhana kidume nikaungana na wazee wa kazi, baada ya kutembea umbali kiasi tukawa tumeingia kwenye msitu mmoja heavy basi bila kupoteza muda wale wazee wakatoa nyavu zao pale na mimi nikawekwa kwenye kitengo cha nyavu. Yaani unakaa karibu na nyavu alafu wao wanaenda kuwa kurupusha wanyama then wanapokimbia wanajikuta wamenasa kwenye ile nyavu na mm bila kupoteza muda natakiwa kurukia kwenye ile nyavu na kumtaiti mnyama yotote atakaye kuwa amenasa huku ukitoa ishara ya yowe kuwa amenasa amenasa na wazee wa kazi wanakuja kumalizia kwa mkuki na hapo ndiyo sasa munafanya mchakato wa kumtengeneza nyama unaanza.

Baada ya kupeana majukumu hayo nikatulia pale kwenye section yangu na wale wazee wakanda kuwakurupusha wanyama kama dakika kumi hivi kinanipita kitu shwaaaaaa kwa speed ya jet fighter na mimi kwa kuwa ni kijana jemedari sikupoteza muda na fyaaaaa nikarukia ile net, kitu na box mnyama huyu hapa sikupoteza muda nikaanza kupiga yowe weyoooooo kanasana hukuuuuu njooooniiiii nimempiga ngeta yule mnyama aiseeee yaani yule mnyama kwa kweli kwa ile kabali alitulia sana. Na mimi nikiwa nimebania meno mara mzee mmoja aliyekuwa jirani na mimi nikamuona kaja ila cha ajabu nikamuona kadondosha mkuki wake na akachomoka kwa speed ya hatari akatoweka ktk mboni zangu na viunga vile.

Hapo mm naendelea tu kumkaba yule mnyama akaja mzee wa pili cha ajabu alipiga kona kama vile jet fighter fyuuuuu akarudi alikotokea pale nikaanza kuwaza kuna nini leo mbona mchezo wa leo siuelewi elewi na wote wawili hakuna aliyesema kitu zaidi ya kutoa mbio kama Mr. bolt.

Akaja mzee wa tatu alivyofika pale na mkuki wake na yeye hali ni ile ile alipotaka kumtandika mkuki yule mnyama akasita na akatupa kule ule mkuki doooh! Pale nikajua hapa kuna kitu siyo bure yule mzee akawa muungwana kwangu akaniambia weweeee kimbia huyo ni chui 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 bhana bhana pale pale mwili ukafa ganzi nikajikuta nimelegeza mikono yangu na network ikakata kwa kweli niliona malaika wengi sana kwenye upeo wa ubongo wangu.
Nikapoteza kabisa memory baada ya kama dakika kumi hivi nikajihisi nipo kwenye usingizi mzitooo na nikiwa sielewi kuwa nipo mawindoni nika feel kama nipo home najigeuza hivi naona ile net iko empty yule chui kumbe nilivyolegeza mikono na yeye akajitetea kwa kusepa so nikawa mm na ile net. Akili ikanijia nikasimama aisee nikiri tu pale zile mbio nilizotoa nilistahili kupata medali ya dhahabu Mr. Bolt asubiri fyaaaaaaaaaaaaaaaa visigino nahisi kabisa vinagusa kisogoni na break ya kwanza home hapo nahema watu wanashangaa kumbe na wale wazee walikuwa kwenye mbio wanasalimiwa na watu ila no majibu so waliponiona na mm wakahisi kuna kitu huko porini kwa kweli nilipofika home nilipitiliza ndani nikafunga mlango nikiwa nahema balaaa nikajikuta namsifu MUNGU kwa ukuu wake wa kunionea huruma na kunipa nafasi nyungine ya kuishi.

Kwa kweli baada ya kama lisaa hivi ndiyo nikaanza kuwasimulia watu kilichojiri huko kwa pori. Japo nilienda na wazee ila wazee wale wako vzr kwenye mbio khaaaaaa! Turbo zilifunguliwa si mchezo.

Wanakijiji walitupa pole ila walicheka sana 🤣🤣🤣🤣🤣 coz wazee wakitembea ni kama vile umri umewaacha sana ila kwenye zile mbio shaabashi wote tulikuwa vijana

Mimi ndiyo ilikuwa mwisho kwenda kuwinda.

Wale ma greater thinker tulieni na mbwembwe zenu za kukomenti

Wakishua pia tulieni
#Tufurahi tu kwa kweli life is too short

#Uchu wa nyama
Life kijijini🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Jamaa nowdays unakuja na vinyuzi vya kuchekesha sana🤣🤣🤣🤣

Daaah hatari sana, kwamba mlikuwa mnapigana mabusu na ibilisi chui😆😆😆
 
Hao wazee walipungukiwa utu, hekima na ujasiri, sasa walishindwa vp kutumia siraha zao kummaliza huyo mnyama.
 
Hao wazee walipungukiwa utu, hekima na ujasiri, sasa walishindwa vp kutumia siraha zao kummaliza huyo mnyama.

Ndugu yangu ujue bush sifa za chui ziko wazi alafu sema nn siku zote tulikuwa tunapata ila kile kitete cha kwamba huyu chui walijikuta wanalegea tu kwanza hawakuamini jinsi nilivyokuwa nimemkumbatia yaani ujasiri uliwaisha kabisa jombaaaa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Jamaa nowdays unakuja na vinyuzi vya kuchekesha sana🤣🤣🤣🤣

Daaah hatari sana, kwamba mlikuwa mnapigana mabusu na ibilisi chui

Chui alinipa kisogo mwenyewe ningejua kuwa ni chui sijui ingekuwaje? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Dah hii chai kabisa ya asubuhi chui umkumbatie tu hivi hivi ye yuko wapi anakuangalia tu duh

Jombaa kwa uwindaji wetu ungekuwa unaujua usingewekea shaka hata kidogo mwenyewe sikukujua kama ni chui na kwa jinsi nilivyokuwa nimemtaiti chui alisanda, kabali moja takatifu akatulia tuliiiii 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Jombaa kwa uwindaji wetu ungekuwa unaujua usingewekea shaka hata kidogo mwenyewe sikukujua kama ni chui na kwa jinsi nilivyokuwa nimemtaiti chui alisanda, kabali moja takatifu akatulia tuliiiii 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Hiyo ni wapi kwani tuanzie hapo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom