Uchu wa madaraka jinamizi kubwa kwa viongozi wa Afrika

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
UCHU WA MADARAKA JINAMIZI KWA VIONGOZI AFRIKA

news_bKabila-Mugabe-300x204.jpg

Na Balinagwe Mwambungu,
Mtanzania

BAADHI ya viongozi wa Kiafrika wamekuwa ving’ang’anizi kama luba. Wakishaingia madarakani hawataki kuondoka, wako tayari kufanya chaguzi kwa gharama kubwa (ili kuwaridhisha wakubwa wa nchi za Magharibi), kwamba wanafuata misingi ya demokrasia huku wakiiba kura ili waendelee kutawala.

Ni nchi chache katika Afrika ambazo zimeweza kuendesha chaguzi za wazi na kufanikisha kubadili uongozi. Ghana inapigiwa mfano, imebadili uongozi wa juu mara tatu kupitia sanduku la kura. Jerry Rawlings alikuwa Rais wa kwanza kuondoka madarakani kwa hiyari. Akafuatiwa na John Mahama ambaye chama chake cha National Democratic Congress kilishindwa kwenye uchaguzi mkuu na kumwachia madaraka Rais wa sasa, Nana Akufo-Addo.

Nigeria ni nchi ya pili kuendesha uchaguzi huru na wa haki baada ya kustaafu Rais Olusegun Obasanjo, alimwachia kiti Goodluk Jonathan ambaye alikubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu na Jenerali Muhammad Buhari.

Nchi nyingine ambazo zimebadilisha utawala kwa njia ya kura ni pamoja na Malawi. Rais wa maisha, Dk. Hastings Kamuzu Banda, alishindwa kwenye uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi na Bakili Muluzi ambaye kipindi chake kilipokwisha pia aliachia ngazi.

Tanzania ni nchi pekee ambayo ina marais wastaafu wengi kwa kuwa inafuata Katiba yake kwa dhati. Rais anaruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili tu vya miaka mitano akitaka. Lakini Katiba iko kimya kuhusu rais mstaafu kurudi kwenye madaraka baada ya miaka mitano.

Katika nchi nyingine, kwa mfano Senegal, Rais Mstaafu, Abdoulaye Wade (90), ametangaza kuwa atagombea ubunge katika uchaguzi ujao pamoja na kwamba ana umri mkubwa. Viongozi wengine ving’ang’anizi ni Yoweri Museveni (73) wa Uganda na Joseph Kabila (47) wa DR Congo, walidiriki kubadilisha Katiba ili waendelee kutawala.

Museveni sasa anataka Katiba ibadilishwe tena kwa kuondoa kifungu kinachomzuia mtu mwenye miaka zaidi ya 75 kugombea urais.

Museveni ambaye hakuingia madarakani kwa njia halali, alishiriki kumpindua Iddi Amin na Milton Obote kisha kulibadilisha jeshi lake la msituni NRA (National Resistance Army) na kulifanya vuguvugu la kisiasa National Resistance Movement (NRM).

Museveni pamoja na kutangaza mwaka 2001 kwamba hatagombea tena, akagombea mwaka 2006 na anaendelea kutawala.

“Mzee huyu ambaye aliiokoa nchi, kwanini unataka aondoke? Nawezaje kuacha shamba la migomba nililopanda mwenyewe wakati linaanza kuzaa ndizi,” anasema Museveni.

Aliyekuwa Rais wa Marekani, Barrack Obama, aliwahi kuwaambia viongozi wa Kiafrika: “Asiwepo mtu wa kuwa rais wa maisha. Nchi zenu zitakuwa kiuchumi kama mnawaachia uongozi vijana wenye damu mpya na mawazo mapya.

Mimi bado ni kijana, lakini najua fika kwamba mtu mwingine mwenye nguvu na mawazo mapya ataifaidisha nchi yangu.”

Maneno hayo murua hayakuwaingia akina Robert Mugabe (93), ambaye pamoja na kuugua ugonjwa utokanao na umri mkubwa, (senility), bado anasema atagombea urais mwaka 2018!

Marais wa Afrika waige mfano wa Joachim Chisano na Amando Guebuza (Msumbiji), Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, wote wa Tanzania ambao waliheshimu Katiba na kung’atuka.

Kenneth Kaunda (Zambia), Bakili Muluzi (Malawi), Joyce Banda (Malawi), Daniel Arap Moi na Mwai Kibaki (Kenya), walikubali kuachia madaraka muda wao ulipofika kama ilivyokuwa kwa Festus Mogae (Botswana) na Sam Nujoma (Namibia).

Viongozi wasisubiri yawakute yaliyowakuta Hosni Mubarak (Misri), Blaise Compaore (Burkina Faso), El Abidine Ben Ali (Tunisia), Muammar Gadaffy (Libya), Joachim Opango (Congo) na wengineo ambao waliondolewa madarakani kwa nguvu.

Jose Edward dos Santos ameitawala Angola tangu mwaka1979, amesema hatagombea tena nafasi ya rais katika uchaguzi ujao (2018) kama hataiga mfano mbaya wa Rais Museveni.

King Mohamed II (Morocco), King Muswati III (Lesotho) na King Letsie (Swaziland), ni watawala wa jadi, lakini Abdelaziz Boutefrika (Algeria), Dennis Nguesso (Congo), Isaias Afweki (Eritrea), Omar Al Bashir (Sudan), Idriss Deby (Chad), Paul Biya (Cameroon), Teodor Obiang Nguema (Equatorial Guinea), wamekuwa madarakani kwa muda mrefu na hawana mpango wa kustaafu.

Hawa wanaweza kuitwa ni walevi wa madaraka, maana wataalamu wanasema jinsi kiongozi anavyokaa madarakani kwa muda mrefu, uwezo wake wa kufikiri na kutenda au kuamua mambo mazito ya nchi, unazidi kupungua. Mambo mengine huwa yanampita bila kujua na watu wajanja wanaamua kwa niaba yake na kumficha asiyajue.

Marie Antoinette aliyekuwa Malkia wa Ufaransa, alipoona maandamano makubwa jijini Paris, aliwauliza wasaidizi wake kwanini watu wanaandamana. Akajibiwa kwamba walikuwa hawana mkate. Akashangaa na kuwajibu: “Kwanini wasipewe keki?”

Mtu akiingia Ikulu atafanya yale yaliyokuwa yanamkera au kurekebisha wenzake walipoptoka, lakini jinsi muda unavyokwenda, vipaumbele vyake vinabadilika.

Mifano hai ni ya marais wetu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete, wote walifanya kazi nzuri katika kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili au cha ‘lala salama’, waliacha bora mambo yaende.

Ndio maana ilikubalika kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ataongoza kwa mihula miwili tu.

Wananchi wanafurahia Rais John Magufuli anavyofanya kazi na kufikiri kwamba akipewa muda mrefu zaidi ataweza kuipeleka nchi mbali zaidi kimaendeleo.

Miaka 10 iliyotamkwa kwenye Katiba inatosha. Rais Magufuli ayafanye makubwa aliyokusudia kuyafanya, ili kujenga msingi mzuri wa uzalendo na uwajibikaji kwa atakayefuata ajengee juu ya msingi huo. Lakini haya yatawezekana tu ikiwa atamalizia pale alipoishia mtangulizi wake kwa kuipatia nchi Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.
 
Makubwa anayofanya Magufuli ni yapi?

Kuna watu watatuambia sijiu issue ya makinikia,n.k.

Kwa ujinga wetu wa kiwango cha lami hatujiulizi mbona hata hizo ripoti zenyewe za maknikia tunambiwa eti ni siri ya Mkulu!!

Tujiulize wanatuficha nini!

Akili ya kujiuliza watu hawana wako busy tu kushangila wakidhani mzungu ana akili kama zetu atatulipa haya matrilioni.

Hili bara na watu wake ni shida sana!!
 
Hakuna chama kitapewa ridhaa na Watanzania kuchukua nchi bali ni wahuni na mafisadi wa MACCM tu!

Sasa kama mnalijua hili kwanini bado mnaiogopa katiba ya rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi? Kwanini unadhani pole pole alitamka hadharani kwamba kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki basi MACCM yajiandae kukabidhi Ikulu!?

Umeandika vizuri juu ya katika unawaita hivyo tena eeeeh

Unafikiri kuna chama kingine chochote cha upinzania kitapewa nchi na wananchi.. na hivi mlivyo endeleeni kuota tu
 
Kuendelea kung'ang'ania madaraka hakusaidii kitu.

Mtu kama Mugabe, aache muda wa kupumzika na family hata kidogo. Siyo muda wote ame u dedicate kwenye urais.

Mkuu, hivi Mswati ni wa Lesotho au Swaziland

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakuna atakayekujibu Mkuu. Yaani watu ni mazuzu mno! Kumsifia huyu lakini hawana hata moja la kuorodhesha alilolifanya kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania.
Yaani huyu bwana hata akifanya jambo la kawaida kama kuzindua barabara basi jambo hilo litakuzwa utadhani kina Kikwete hawakuwahi kujenga hata kilomita moja ya lami ila yeye ndio kawa wa kwanza!

Yaani ni full ubashite hata wahariri nao kazi ni kusifu na kukuza mambo wanasahau kabisa huyo ndio anaemlinda Bashite alievami chombo cha habari.

Sisi ni bure kabisa katika huu ulimwengu!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi hawa kijani tuwangoe kwa style gani?
Kwenye kura wanatuibia,vyombo vya dola vyte viko chini Yao,mahakama Yao ?

Ova
 
Tanzania ni nchi pekee ambayo ina marais wastaafu wengi kwa kuwa inafuata Katiba yake kwa dhati. Rais anaruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili tu vya miaka mitano akitaka. Lakini Katiba iko kimya kuhusu rais mstaafu kurudi kwenye madaraka baada ya miaka mitano.
Hii sifa inayoitofautisha Tanzania na nchi nyingi za Afrika ina dalili za kutoweka!!!
Katika nchi nyingine, kwa mfano Senegal, Rais Mstaafu, Abdoulaye Wade (90), ametangaza kuwa atagombea ubunge katika uchaguzi ujao pamoja na kwamba ana umri mkubwa. Viongozi wengine ving’ang’anizi ni Yoweri Museveni (73) wa Uganda na Joseph Kabila (47) wa DR Congo, walidiriki kubadilisha Katiba ili waendelee kutawala.
Huwezi kutaja ving'ang'anizi wa madaraka ukanda huu bila kumtaja Kagame... sijui kwanini Mwambungu kwamwacha PK!

Kagame aliongoza Rwanda as de facto leader kwa miaka 6! Mwaka 2003 akachukua urais through Arusha Accord! Mwama 2003 akachukua uraisi through new constitution ambayo ilikamilika the same year (2003). Akarudi tena 2010 (after 7 years term) ambapo ilibidi iwe hadi 2017!

Alipoona 2017 inakaribia, akatumia makuwadi wake kubadilisha katiba ili aendelewe kutawala kwa vigezo vile vile vinavyotumiwa na makinikia na makuwadi wa Pombe kwamba hakuna mwingine zaidi ya huyo!!!!

So, from 1994 as de facto leader to 2024 jamaa atakuwa amekaa miaka 30... kama hajaongeza tena basi!!!

Kuna mtu mmoja alikuwa anajiita Koba, sijui yupo siku hizi au anatumia ID gani!! Miaka kadhaa iliyopita tulibishana sana hapa JF nilipomuambia wazi kwamba kwa jinsi Kagame anavyopenda madaraka, hawezi kuondoka hiyo 2017 NEVER... na hatimae yametimia!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakuna chama kitapewa ridhaa na Watanzania kuchukua nchi bali ni wahuni na mafisadi wa MACCM tu!

Sasa kama mnalijua hili kwanini bado mnaiogopa katiba ya rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi? Kwanini unadhani pole pole alitamka hadharani kwamba kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki basi MACCM yajiandae kukabidhi Ikulu!?

BAK nikujuze, sasa ndio nafikiria nichukue kadi ya chama chao na kura nimpigie tena Mkulu kwa furaha. Kwa kweli ni hakunaga

Kumbe aliyasoma hayo... kweli ana akili maana nyie ndio mnazidi kuisha... mnajisahau siasa ya upinzani sifuri.

Na wengine wengi wanajidai upinzani kumbe wameisima meno haswa na hawana jinsi lolote kukosea tu eeeeh

Tundu Lissu:
Dear members.
Greetings from your President wherever you may be.

Bizi kumsifia eeeh anajali hicho cheoooo...ha ha haaaaa
 
madaraka matam..

mx_nature
Hakuna umaskini mbaya duniani kama upumbavu.
Ni upumbavu wetu watu weusi wa bara la Afrika uliowadhalilisha babu zetu katika biashara ya kuuzwa kama ng'ombe kwenda kutumikishwa Ulaya na Amerika kama wanyama wa nguvukazi wanavyotumikishwa.
Kikaja kipindi cha kuwatumikisha barani Afrika baada ya "kuonewa huruma" na wazungu waliopiga marufuku biashara ya utumwa. Kikafuatia kipindi cha viongozi wa kikabila "kuuza" sehemu za himaya zao kwa 'kuingia mikataba" na watu weupe (white people) kwa malipo ya shanga za kuvaa kiunoni na shingoni. Tunaona mikataba ya viongozi wasomi wa nchi za Kiafrika na watu weupe ilivyorudia makosa ya machifu wa kikabila wa karne ya 19.
"Vita ya makanikia" ni kama vita vilivyopiganwa na akina Kinjekitile walipogundua wameporwa "nchi" zao. Matokeo ya vita walivyopigana yanafahamika.
Afrika bado kabisa. Ujinga na upumbavu wa Mwafrika bado unamtesa sana. Uelewa mtu mweusi unapokuwa chini kupindukia, utambuzi wa mambo mema na ya hovyo unakosekana. Kila jambo yeye anaona ni jema. Niite mbaguzi wa rangi lakini ukweli unabaki kuwa watu weusi wa South Afrika walipoingia madarakani kuongoza wamepunguza kasi ya maendeleo ya nchi hiyo. Yamejitokeza ya Jacob Zuma na familia ya Gupta.

Hakuna jipya alilofanya Mhe rais mbali na kujitafutia sifa kuwaumiza wananchi na kutumia hofu yao kujijenga kisiasa. Tangu aingie madarakani hadi leo ni foleni za kubaini "vyeti bandia", watumishi hewa na kaguzi za kustukiza za kisanii. Mambo yote haya yangejengewa na kudhibitiwa kwa mifumo ya kiutawala tu badala ya kuyafanyia siasa. Gharama za maisha zimepanda; bei ya sukari hapa kijijini kwetu imefikia 3,400/=. Kifungua kinywa kinachusisha chai kimekuwa ni anasa kwetu. Maslahi ya watumishi wa umma hata ya kisheria yanafanyiwa siasa.

Hii ni laana?
 
Ata hapa Tz ngoma imeanza kurindima taratibu magu baki magu baki, hiyo ni strategy ya kutaka kubadili Katiba, wanaanzaga taratibu wakidai watanzania wanataka, hatutaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UCHU WA MADARAKA JINAMIZI KWA VIONGOZI AFRIKA

news_bKabila-Mugabe-300x204.jpg

Na Balinagwe Mwambungu,
Mtanzania

BAADHI ya viongozi wa Kiafrika wamekuwa ving’ang’anizi kama luba. Wakishaingia madarakani hawataki kuondoka, wako tayari kufanya chaguzi kwa gharama kubwa (ili kuwaridhisha wakubwa wa nchi za Magharibi), kwamba wanafuata misingi ya demokrasia huku wakiiba kura ili waendelee kutawala.

Ni nchi chache katika Afrika ambazo zimeweza kuendesha chaguzi za wazi na kufanikisha kubadili uongozi. Ghana inapigiwa mfano, imebadili uongozi wa juu mara tatu kupitia sanduku la kura. Jerry Rawlings alikuwa Rais wa kwanza kuondoka madarakani kwa hiyari. Akafuatiwa na John Mahama ambaye chama chake cha National Democratic Congress kilishindwa kwenye uchaguzi mkuu na kumwachia madaraka Rais wa sasa, Nana Akufo-Addo.

Nigeria ni nchi ya pili kuendesha uchaguzi huru na wa haki baada ya kustaafu Rais Olusegun Obasanjo, alimwachia kiti Goodluk Jonathan ambaye alikubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu na Jenerali Muhammad Buhari.

Nchi nyingine ambazo zimebadilisha utawala kwa njia ya kura ni pamoja na Malawi. Rais wa maisha, Dk. Hastings Kamuzu Banda, alishindwa kwenye uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi na Bakili Muluzi ambaye kipindi chake kilipokwisha pia aliachia ngazi.

Tanzania ni nchi pekee ambayo ina marais wastaafu wengi kwa kuwa inafuata Katiba yake kwa dhati. Rais anaruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili tu vya miaka mitano akitaka. Lakini Katiba iko kimya kuhusu rais mstaafu kurudi kwenye madaraka baada ya miaka mitano.

Katika nchi nyingine, kwa mfano Senegal, Rais Mstaafu, Abdoulaye Wade (90), ametangaza kuwa atagombea ubunge katika uchaguzi ujao pamoja na kwamba ana umri mkubwa. Viongozi wengine ving’ang’anizi ni Yoweri Museveni (73) wa Uganda na Joseph Kabila (47) wa DR Congo, walidiriki kubadilisha Katiba ili waendelee kutawala.

Museveni sasa anataka Katiba ibadilishwe tena kwa kuondoa kifungu kinachomzuia mtu mwenye miaka zaidi ya 75 kugombea urais.

Museveni ambaye hakuingia madarakani kwa njia halali, alishiriki kumpindua Iddi Amin na Milton Obote kisha kulibadilisha jeshi lake la msituni NRA (National Resistance Army) na kulifanya vuguvugu la kisiasa National Resistance Movement (NRM).

Museveni pamoja na kutangaza mwaka 2001 kwamba hatagombea tena, akagombea mwaka 2006 na anaendelea kutawala.

“Mzee huyu ambaye aliiokoa nchi, kwanini unataka aondoke? Nawezaje kuacha shamba la migomba nililopanda mwenyewe wakati linaanza kuzaa ndizi,” anasema Museveni.

Aliyekuwa Rais wa Marekani, Barrack Obama, aliwahi kuwaambia viongozi wa Kiafrika: “Asiwepo mtu wa kuwa rais wa maisha. Nchi zenu zitakuwa kiuchumi kama mnawaachia uongozi vijana wenye damu mpya na mawazo mapya.

Mimi bado ni kijana, lakini najua fika kwamba mtu mwingine mwenye nguvu na mawazo mapya ataifaidisha nchi yangu.”

Maneno hayo murua hayakuwaingia akina Robert Mugabe (93), ambaye pamoja na kuugua ugonjwa utokanao na umri mkubwa, (senility), bado anasema atagombea urais mwaka 2018!

Marais wa Afrika waige mfano wa Joachim Chisano na Amando Guebuza (Msumbiji), Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, wote wa Tanzania ambao waliheshimu Katiba na kung’atuka.

Kenneth Kaunda (Zambia), Bakili Muluzi (Malawi), Joyce Banda (Malawi), Daniel Arap Moi na Mwai Kibaki (Kenya), walikubali kuachia madaraka muda wao ulipofika kama ilivyokuwa kwa Festus Mogae (Botswana) na Sam Nujoma (Namibia).

Viongozi wasisubiri yawakute yaliyowakuta Hosni Mubarak (Misri), Blaise Compaore (Burkina Faso), El Abidine Ben Ali (Tunisia), Muammar Gadaffy (Libya), Joachim Opango (Congo) na wengineo ambao waliondolewa madarakani kwa nguvu.

Jose Edward dos Santos ameitawala Angola tangu mwaka1979, amesema hatagombea tena nafasi ya rais katika uchaguzi ujao (2018) kama hataiga mfano mbaya wa Rais Museveni.

King Mohamed II (Morocco), King Muswati III (Lesotho) na King Letsie (Swaziland), ni watawala wa jadi, lakini Abdelaziz Boutefrika (Algeria), Dennis Nguesso (Congo), Isaias Afweki (Eritrea), Omar Al Bashir (Sudan), Idriss Deby (Chad), Paul Biya (Cameroon), Teodor Obiang Nguema (Equatorial Guinea), wamekuwa madarakani kwa muda mrefu na hawana mpango wa kustaafu.

Hawa wanaweza kuitwa ni walevi wa madaraka, maana wataalamu wanasema jinsi kiongozi anavyokaa madarakani kwa muda mrefu, uwezo wake wa kufikiri na kutenda au kuamua mambo mazito ya nchi, unazidi kupungua. Mambo mengine huwa yanampita bila kujua na watu wajanja wanaamua kwa niaba yake na kumficha asiyajue.

Marie Antoinette aliyekuwa Malkia wa Ufaransa, alipoona maandamano makubwa jijini Paris, aliwauliza wasaidizi wake kwanini watu wanaandamana. Akajibiwa kwamba walikuwa hawana mkate. Akashangaa na kuwajibu: “Kwanini wasipewe keki?”

Mtu akiingia Ikulu atafanya yale yaliyokuwa yanamkera au kurekebisha wenzake walipoptoka, lakini jinsi muda unavyokwenda, vipaumbele vyake vinabadilika.

Mifano hai ni ya marais wetu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete, wote walifanya kazi nzuri katika kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili au cha ‘lala salama’, waliacha bora mambo yaende.

Ndio maana ilikubalika kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ataongoza kwa mihula miwili tu.

Wananchi wanafurahia Rais John Magufuli anavyofanya kazi na kufikiri kwamba akipewa muda mrefu zaidi ataweza kuipeleka nchi mbali zaidi kimaendeleo.

Miaka 10 iliyotamkwa kwenye Katiba inatosha. Rais Magufuli ayafanye makubwa aliyokusudia kuyafanya, ili kujenga msingi mzuri wa uzalendo na uwajibikaji kwa atakayefuata ajengee juu ya msingi huo. Lakini haya yatawezekana tu ikiwa atamalizia pale alipoishia mtangulizi wake kwa kuipatia nchi Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.
Wanachokiogopa ni kwamba atakaye tawala baada yake ni kutokuwa na imani naye kuendana na madhambi mengi aliyoyatenda ktk utawala wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom