Uchomaji wa misitu na mashamba Lindi-Ruangwa upatiwe muarobaini

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,205
2,806
Habari zenu wadau

Kama kuna wenyeji wa Lindi mtakuwa ni mashahidi juu ya jinsi watu wanavyochoma moto hovyohovyo kwenye mashamba ya mikorosho, misituni (na milimani) hususani vijiji vya Ruangwa

Wengi utasikia "tunaandaa mashamba" wengine utasikia "tunafukuza wanyama hatari- wawindaji"

Lakini nimefuatilia nimeona ni tabia ya mazoea tu hakuna hakuna sababu ya kuchoma moto ila mtu akiona tu pori/nyasi kavu anatamani kuunguza

Kibaya zaidi ni kwamba mamlaka husika hazina hata mpango wa kushughulikia swala hilo. Watendaji wa vijiji wapo, maafisa mbalimbali wanaohusiana na mazingira wapo lakini sijawahi kusikia wala kuona hatua zozote dhidi ya vitendo hivi lakini haohao waunguzaji ikitokea moto umepitiliza ukaunguza mazao /mimea ya mmoja wao utakuta wanalipishana mda mwingine hata wanapelekana eti kwa mtendaji wa kijiji nae anawasikiliza

Nenda maeneo mbalimbali ya Ruangwa kipindi cha kiangazi utakuta alama za miunguzo tu kila kona ya mashamba milima mapori nk. Inatokea baadhi ya siku kunakuwa kweusi kabisa utadhani kutanyesha kumbe mawingu ya moshi... mara nyingine kunakuwa giza utadhani saa12 jioni kumbe ni athari za moto uliochomwa

Mbona sehemu nyingine wanafanya shughuli zao kama hizo lakini hawazihusishi na kuunguza mazingira hovyohovyo? nitakupa mifano kadhaa ya sehemu zenye mapori/misitu kama Ruangwa tu lakini wanatumia vizuri...

Nenda Tubugwe kule Kongwa Kibodyani wanawinda na kulima lakini hutaona moto wa hovyohovyo

Lengatei Kiteto kule ndo wanalima wanafuga wanarina na kuwinda lakini ukiingia misitu yao unaona kweli nipo msituni

Bombani kule muheza ndo kabisa usipime kwa uzuri wa mapori yao hutaona wakichomachoma moto hovyo

Nenda misitu ya Pwani utapenda sauti za ndege wanaopatikana kwenye mapori yao... na sehemu nyingine nyingi.

Huwa nawaambia sana waachane na katabia haka lakini nguvu yangu ndogo sana... huyo kiongozi wa kijiji ndo hata tuseme vipi tu ndo kwanza haelewi


Kwanini Nyinyi mshindwe kutunza napori na misitu yenu wenzenu wamewezaje?, mfano huko kwingine miaka ya nyuma nakumbuka tulikuwa barabarani mbali na makazi halafu maeneo hayo kulikuwa kunafuka moshi mara gari za halmashauri zikawa zinapita washkaji wakatimka mbio kuuliza naambiwa wewe baki hapo DC akubebe maana mwenzako huyo akikukuta sehemu penye kufuka moshi kama hivyo utaenda kujieleza kwanini kumewashwa moto hapo... sikukimbia akasimama yule DC lakini nilikuwa kachalii tu kwahiyo hakunifanya kitu alishuka akacheki tu yale maeneo akasepa
 
Mapori yaliyo mengi vijijini Ruangwa ukiingia hata baadhi ya misitu ya hifadhi kabisa na ukasikia sauti ya ndege au ukiona hata mjusi utajiuliza mara mbilimbili... yaani pamepoa halafu kweupe pe ni nyeusi ya moto tu utakayoona
 
Back
Top Bottom