Uchomaji takataka katika hospitali ya Sekou Toure - Mwanza ni hatarishi

Bonson

Senior Member
Apr 20, 2013
183
147
Ndugu wana FJ,
Naandika uzi huu ili uweze kumfikia Mkurugenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza au Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na wadau wote wa utunzaji wa mazingira.

Siku chache zilizopita nilikwenda katika hospitali ya Mkoa kuchukua mwili wa ndugu yangu aliyefariki baada ya kuugua stroke. Jambo lililonishangaza ni kuona sehemu ya kuchomea takataka za hospitali hiyo ikiwa karibu kabisa na wodi za wagonjwa na chumba cha maiti. Moshi ulikuwa unazagaa kila mahali na kusababisha kero kwa watu wote maeneo hayo.

Nauomba uongozi wa Hospitali yetu hii wafanye jitihada za makusudi na za haraka ili kuhamisha eneo hilo la kuchomea takataka kwa sababu taka zingine huwa zikichomwa zinaweza zalisha sumu hatarishi. La sivyo, basi eneo hilo liboreshwe ili moshi usizagae hovyo.

Baada ya kusema hayo, niwapongeze uongozi wa Hospitali kazi kubwa wanayoifanya ya kuhudumia jamii ya Mwanza.

Mungu Ibariki Tanzania
 

Attachments

  • VID-20180719-WA0002[1].mp4
    9.1 MB · Views: 22
  • IMG-20180719-WA0005[1].jpg
    IMG-20180719-WA0005[1].jpg
    35 KB · Views: 36
  • VID-20180719-WA0002[1].mp4
    9.1 MB · Views: 18
  • IMG-20180719-WA0005[1].jpg
    IMG-20180719-WA0005[1].jpg
    35 KB · Views: 27
Back
Top Bottom