Uchomaji taka kiholela Tanzania

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
Wakuu leo tuongee uchafuzi wa mazingira unaofanyika hapa tanzania especially dar.

Hivi huwa najiuliza, swala la uchafuzi wa hali ya hewa kwa nn huwa watanzania tunalichukulia kawaida sana, ila kwenye sheria nyingine tunakua serious sana hadi watu kupigwa.

Ukiangalia baadhi ya sehemu Dar, uchomaji wa taka ni kila siku. Huwezi kaa dakika mbili bila kuvuta hewa ya moshi iliyochanganyikana na plastic na chemical nyingine nyingi.

Mtu anaweza kujiamlia tu kuchoma taka na hakuna wa kumkamata wala kumuuliza. Moshi unaweza kutanda mtaa mzima kwa muda wa masaa 6 lakini watu wanaumia kimya kimya hawaongei. Hadi wengine wanaugulia vifua.

Wakuu tatizo ni nn hapa. Taasisi husika kwenye haya maswala iko wapi. Au kama vipi hakuna sehemu moja maalum ya kuchomea taka. Mbona nchi za watu inawezekana huku inashindikana nini. Moshi tunaokula unaotokana na magari ni mwingi, ukiongeza na wachoma taka aisee tusitegemee vifua kuisha. Inasikitisha hata barabarani unapishana na gari inatoa moshi utafikiri inaungua ila traffic hawaikamati.

Kumbuka ulaya gari ikitoa moshi wa ajabu, haitembei, otherwise unagongwa fine na unasurubiwa mahakamani. Huku gari likitoa moshi ni fresh tu.

Hivi mkipima hewa inayovutwa Dar na mikoa mingine yenye mirundikano. Quality ya hewa itakua mbaya sana aisee. Ndo maana magonjwa ya vifua hayaishi. Watu wengi sana wanaumwa vifua. Na sababu ni hizi. Enyi NEMC, muamke basi jamani. Mfanye kitu.
 
Sijui, lakini Kuna imani za kijinga sana zinachangia.
Niliwahi kaa maeneo ya Keko, yeye alikuwa anasubiri usiku wa manane.
Mbaya sana alikuwa anachomea dirishani kwangu. Nilipata taabu sana!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom