Mhache
JF-Expert Member
- Jun 20, 2008
- 345
- 25
Misitu ni muhimu sana kwa maisha yetu. Nilisikiliza kwenye vyombo vya habari juzi kuhusiana na Msitu wa Shengene uliopo Same/Mwanga Kilimanjaro. Watu wanakata miti na kuchimba madini kwenye vyanzo vya maji. Hii ni hatari sana. Kwani ni sawa na kuuwa watu. Iwapo hali hiyo itaendelea ina maana baada ya muda fulani watu watakufa kwa kukosa maji.
Serikali na wananchi wanatakiwa kujua madini hayo yatawapa faida ya muda mfupi kwani yatakapoisha wananchi wataendelea kupata wapi maji. Juhudi ya ziada inatakiwa ili kuwaelewesha wananchi umuhimu wa maji na adhari za faida za haraka.
Je serikali inafanya nini kutatua matatizo kama hayo? Sheria zipo? Na kama zipo zinasemaje kuhusiana na matatizo ya uharibifu wa mzingirA hasa misitu.