Uchomaji moto misitu wilayani rufiji

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
23
Uchomaji moto misitu ni tatizo kubwa katika Bara la Afrika ikiwemo Tanzania. Inaelekea watu wengi wanachoma misitu ili kupata faida ya haraka. Faida zenyewe ni kuni, majengo, mbao na mkaa bila kusahau fedha. Faida hizi ni za muda mfupi. Kwani baada ya muda fulani misitu hiyo inayochomwa moto hutoweka kabisa. Kutoweka kwa misitu matatizo yafuatayo hujitokeza:
 Ongezeko la joto duniani
 Kuyeyuka kwa theluji kwenye milima mfano dhahiri ni Mlima Kilimanjaro ambao barafu iliyokuwa imefunika eneo kubwa imetoweka.
 Ongezeko la kina cha maji baharini
 Na wananchi kukosa kivuli na mandhari zuri ya kupumzikia.

Tatizo hili ni dhahiri kwenye misitu iliyopo kwenye wilaya ya Rufiji.Wananchi wa wilaya hii walipohojiwa walikiri kuhusika na uchomaji moto misitu ili kupata mazao yoliyoorodheshwa hapo juu. Wahojiwa wengi walikiri pia kuwa misitu ni minene sana ambayo ni ngumu kwa mtu kupita ili kupata mazao ya misitu. Suluhisho wanaloliona ni kuchoma moto misitu ili kupata urahisi wa kukata kuni, majengo na mkaa. Pia njia hiyo hutumiwa na wananchi ili kusafisha mashamba yao.

Uchomaji ovyo wa miti ya asili huleta madhara kama kupoteza species muhimu kwa ajili ya dawa, mazalia ya wanyama na mengineyo. Serikali kuu, serikali ya mitaa inabidi zifanyike juhudi za makusudi ili kunusuru misitu hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom