Uchomaji moto baa wazidi kushika kasi Zanzibar

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
8,814
7,589
Na Mwinyi Sadallah
14th August 2011

Zimelipuliwa baa sita, hoteli moja

Baa nyingine imechomwa moto katika eneo la Kisauni jana na kufanya idadi ya matukio ya ulipuaji moto baa na nyumba za wageni visiwani Zanzibar kufikia matatu katika muda wa wiki moja.

Walioshuhudia baa hiyo iitwayo Maisha Plus ikichomwa moto, walisema tukio hilo lilitokea saa moja usiku baada ya kundi linalokadiriwa kuwa na watu saba kuvamia baa hiyo katika Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Kabla ya kuchoma moto baa hiyo, watu hao wakiwa na silaha walimshikilia mlinzi Isaya Juma (29) na badaye kumjeruhi kwa kumkata mkono wa kushoto.
Tukio hili limekuja baada ya watu wengine wasiojulikana kuchoma moto Hoteli ya Matemwe Beach Villa katika eneo la Kiwengwa Jumapili iliyopita na baa ya Amani Fresh juzi katika eneo la Amani mjini Zanzibar.
Akithibitisha kutokea kwa tukio la jana ambapo baa ya Maisha Plus pia ilichomwa moto jana, Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema uhalifu huo ulitokea saa moja dakika 40.
Alipoulizwa juu ya mfululizo wa matukio hayo na kama kuna watu wamekamatwa kusaidia polisi baada ya kushukiwa, Kamishna Mussa alisema polisi haiwezi kukamata watu kabla ya uchunguzi.
"Hadi sasa hakuna mtu tuliyemkamata na bado hatujui sababu ya baa kuchomwa moto Zanzibar," alisema Kamishna Mussa.
Hata hivyo alisema vitendo vya uchomaji moto mali za watu ni uvunjaji wa sheria na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi. Alipoulizwa juu ya hatua zilizochukuliwa na polisi juu ya matukio mengine manne ya aina hiyo katika kipindi cha mwaka huu peke yake, kamishna Mussa pia alisema hakuna aliyekamatwa.
Mlinzi wa baa ya Maisha Plus aliyezungumza na Nipashe akiwa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mnazimoja, Juma alisema watu waliomvamia, mmoja alikuwa na bastola na wengine walikuwa na mapanga na marungu.
Alisema watu hao walimkata mkono wa kushoto kwa kutumia panga wakati akijaribu kuwazuia kumwaga mafuta ya petroli kutoka katika madumu mawili waliyokuwa nayo na baadaye kuchoma moto baa hiyo.
"Nasikia maumivu makali sana, naomba Uniache nipumzike, nasikitika mkono wangu umekatwa," alisema Juma.
Mmiliki wa baa hiyo, Jamilah Awadh alisema baa yote imeteketea pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani, ikiwa ni pamoja na majokofu, majiko, vinywaji vya aina mbalimbali, samani ambavyo hata hivyo hakuweza kukadiria thamani yake.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Home
 
Kama serikali itaendelea kukaa kimya just to buy goodwill kwa wapumbavu wachache wanaoharibu uislamu wakiongozwa na yule shehe burushi basi tutaishia kubaya zaidi

Haiwezekani kulazimisha watu wote waishi unavyotaka simply because of dini au imani kwa ujumla

Ukiona binadamu anashindwa kuvumilia maisha ya mwenzake, tena yasioingiliana na yake zaidi ya ku-share oxygen na infrastructure ujue huyo ni mnyama tu!!!
 
Hao ni wapuuzi wachache wasiofuatilia vizuri maneno ya dini yao na kukurupuka tu. Kama kigezo ni dini basi waende ktk ile kampuni ya ndege ya Emirates pia wachome moto! Silly!! Au kama wana mshipa Basi waende ktk zile hoteli a kitalii zinazowaingizia pesa nyingi sana ktk uchumi wa Zanzibar because of tourists, na waache kuonea wtanzania wenzao! Silly!
 
Wanaupaka matope uislamu na kuonekana dini yenye uharibifu na umwagaji wa damu.Ila sivyo.Swala la imani si la kumlazimisha mtu hata kidogo.Sasa hapa utasema mungu amekutuma kufanya haya?.Mungu amempa kila mtu nafsi inayoweza kufanya maamuzi.Sasa mkono wa ndugu huyu umekatika maskini.Dah, inatia huruma.
 
Nadhani sera ya jino kwa jino itumike what are we waiting for na sisi kuanza kuwa ng'oa meno na kunyofoa macho huku kwetu na kisha kuchoma nyumba zao haiwezakani wao wanafanya wanachotaka halafu kule hawataki watu watafute riziki zao
 
Hao ni wapuuzi wachache wasiofuatilia vizuri maneno ya dini yao na kukurupuka tu. Kama kigezo ni dini basi waende ktk ile kampuni ya ndege ya Emirates pia wachome moto! Silly!! Au kama wana mshipa Basi waende ktk zile hoteli a kitalii zinazowaingizia pesa nyingi sana ktk uchumi wa Zanzibar because of tourists, na waache kuonea wtanzania wenzao! Silly!

Busara hio!
 
Wanaupaka matope uislamu na kuonekana dini yenye uharibifu na umwagaji wa damu.Ila sivyo.Swala la imani si la kumlazimisha mtu hata kidogo.Sasa hapa utasema mungu amekutuma kufanya haya?.Mungu amempa kila mtu nafsi inayoweza kufanya maamuzi.Sasa mkono wa ndugu huyu umekatika maskini.Dah, inatia huruma.

Ni kweli kabisa!
 
Tatizo lililopo ni kwamba watu wanachanganya Arabic culture na dini ya uislam.
Mara nyingi watu wanafuata Arabic culture wakidhani ni dini ya uislam. Haya mapokeo sijui ni wapi tunaelekea nayo, na umaskini utachukua muda mrefu sana kukuondoka kama hujakombolewa kifikra.
 
And the govt through its police force must take a rational action towards those who are doing this, haiingii akilini kwamba vvitendo hvyo vinatokea for more than a year now na police hawajafanya lolote la maana kuvizuia, kibaya ni pale raia watakapoona police force is of no0 help to them wakaanza ku take acction ndo utaskia wajinga hawa wanaanza kuhubiri habari za raia kutojichukulia sheria mkononi, kimsingi hali hyo imefikia pabaya, inaonekana ndogo coz hakuna counter reaction, watu wakichoka tu tutayaskia
 
Ni frustrations za maisha tu zinawasumbua! kwani hao waarabu mbona wanauza mapombe kila kukicha at the same time wanafuata dini zao, nenda uarabuni ukajionee! Ni upungufu wa fikra tu!
 
Bado tunasafari ndefu hasa ya kujijua, culture zetu zilivurugwa mno na waliotutawala!
 
And the govt through its police force must take a rational action towards those who are doing this, haiingii akilini kwamba vvitendo hvyo vinatokea for more than a year now na police hawajafanya lolote la maana kuvizuia, kibaya ni pale raia watakapoona police force is of no0 help to them wakaanza ku take acction ndo utaskia wajinga hawa wanaanza kuhubiri habari za raia kutojichukulia sheria mkononi, kimsingi hali hyo imefikia pabaya, inaonekana ndogo coz hakuna counter reaction, watu wakichoka tu tutayaskia

Au serikali kuogopa kuharibu "muungano thabiti tulionao!"
Upuuzi mtupu!
 
Ni frustrations za maisha tu zinawasumbua! kwani hao waarabu mbona wanauza mapombe kila kukicha at the same time wanafuata dini zao, nenda uarabuni ukajionee! Ni upungufu wa fikra tu!

Tatizo ni uwezo, elimu na fikra duni tulizonazo, sijui hawa wachomaji wa bar za watu watagundua lini kuwa kuchoma moto sio suluhisho wala halitanufaisha maisha yao!
 
Back
Top Bottom