UCHOKOZI WA EDO: Tunaenda kuteketeza noti nyingine Singida

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
UCHOKOZI WA EDO: Tunaenda kuteketeza noti nyingine Singida
Edo+Kumwembe.jpg

Usijali sana unaposikia kwamba mkuu wa jengo la Dodoma hajui mbunge wake aliyepigwa risasi yuko wapi. Usijali sana. Kitu cha kujali ni pale anapofungua mdomo na kusema ‘Nimeamuru mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aitishe uchaguzi katika jimbo lake’.

Hii ni kauli ya mwanasiasa, kama ingekuwa kauli ya mchumi yeyote yule angeweza kuweka wazi zaidi kwamba ‘Tumeamuru tutumie zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya jimbo ambalo litatugharimu tena shilingi bilioni moja miezi 10 ijayo kwa sababu ile ile’.

Hapa ndipo ambapo Taifa limekwama. Mambo mengi yapo kisiasa. Sheria nyingi zipo kisiasa. Tungezitafsiri kiuchumi tungeokoa mambo mengi. Hata hivyo nchi za dunia ya tatu hazijali sana mambo ya uchumi. Zinajali siasa huku zikibembeleza wananchi wake na maneno matamu ya kulainisha ya ‘kujali sana wanyonge’.

Ukiuliza sana kwanini tusitengeneze sheria ambazo hazitaruhusu chaguzi za marudio kijingajinga utaambiwa ‘Demokrasia ina gharama zake’. Wakati una hofu Namba Moja atapata wapi pesa za kugharamia miradi mingi mikubwa aliyoanzisha, upande mwingine hauna hofu na matumizi ya namna hii ya chaguzi za marudio.

Kikubwa kinachobaki kwa sasa ni kupiga hatua mbili mbele, kisha hatua tatu nyuma na kupiga makofi ya kujipongeza. Katika hali halisi hakuna kitakachobadilika katika majimbo ya waliounga mkono juhudi au wanaoumwa, au walioamua kuwa watoro wa makusudi bungeni. Tunapiga siasa tu. Hata kama majimbo yao yangekuwa tupu mpaka mwisho wa awamu ya kwanza bado umaskini wetu utabakia pale pale. Kinachofanyika ni kuendelea kujitia umaskini usio na sababu kwa maamuzi yenye msingi wa kisiasa.

Waliotengeneza hizi sheria wanashangilia kwa sasa. Hawataki ziondoke kwa sababu kama hizi. Mwisho wa siku zinatudhihirishia tu jinsi tulivyo, jinsi ambavyo tupo bize na maneno matamu ambayo hayataondoa umaskini wetu.

Unapoona tunakwenda katika uchaguzi wa marudio huku tukitegemea kufanya mwingine ndani ya miezi 10 tu ijayo, halafu kuna watu wanagonga meza kwa nguvu pale Dodoma, unapata shaka na uwezo wa kufikiria wa watu wanaotoa maamuzi mazito katika nchi
hii.
 
Tuna Bunge KINYESI Watanzania tulio wengi tumeshika pua zetu kutokana na harufu mbaya inayotoka ndani ya hili Bunge lililowekwa mfukoni na nduli na dikteta wa Ikulu kwa kuwatumia vikaragosi vyake kikaragosi ndugai na kikaragosi tulia. Bunge UOZO Bunge DHAIFU.
 
Ni mwendelezo wa maamuzi ya kishamba na kuvuruga umoja na ustawi wa taifa letu kwa garama za Watanzania.Ni wapumbafu pekee wanasherekea ushirikina huu.
 
One of the big problems of this country is that,the smart and the intelligent people have only forums to express their views and ideas; whereas, the less intelligent, have both forums as well as power and mandate to implement their ideas even if those ideas are sometimes useless and meaningless.

However,today,it is sad that, even these forums for the smart and the intelligent ones is also under threat!
 
Kongole Sana Ed kwa bandiko hili lililojaa simanzi na huzuni kwa wanaojitambua na kulitakia taifa hili mema! Hapa huwezi kuwaona Lumumba wakichangia kwani hawana hoja thabiti za kuargue juu ya fikra zako pevu! Laiti wangesimama wao na kuukataa huu uhayawani nchi ingesonga japo nusu hatua mbele na siyo hatua Mia nyuma!
 
Tuna Bunge KINYESI Watanzania tulio wengi tumeshika pua zetu kutokana na harufu mbaya inayotoka ndani ya hili Bunge lililowekwa mfukoni na nduli na dikteta wa Ikulu kwa kuwatumia vikaragosi vyake kikaragosi ndugai na kikaragosi tulia. Bunge UOZO Bunge DHAIFU.
Mtaongea sana
sheria haina Hisani ya Mtu wala Wapuuzi fulani wasio taka kuifuata
Lisu sio Mbuge tena
mlie mkojoe hakuna namna
na mjifunze Sikunyingine Sheria ipo
 
Jamaa ametokea kuwa mwandishi mzuri sana aliyeweka mbele maslahi makubwa ya nchi yetu ukilinganisha na waandishi UCHWARA ambao wameweka umahiri wao pembeni na kuamua kuwa vikaragosi vya nduli na dikteta wa Ikulu ili kusaka teuzi waweze kujaza matumbo yao kama yule nanihii wa JamiiForums.

The guy nailed it perfectly
 
Mtaongea sana
sheria haina Hisani ya Mtu wala Wapuuzi fulani wasio taka kuifuata
Lisu sio Mbuge tena
mlie mkojoe hakuna namna
na mjifunze Sikunyingine Sheria ipo
Kwa mfano sheria ya kuzui shughuli za siasa kwa wapinzani tu na ile ya askari Polisi kushiriki viko vya CCM!!

Ni wapumbavu wenzenu tu ndio wanawaelewa!!
 
Tuna Bunge KINYESI Watanzania tulio wengi tumeshika pua zetu kutokana na harufu mbaya inayotoka ndani ya hili Bunge lililowekwa mfukoni na nduli na dikteta wa Ikulu kwa kuwatumia vikaragosi vyake kikaragosi ndugai na kikaragosi tulia. Bunge UOZO Bunge DHAIFU.
Unaweza kukuta Namba Moja hajawatuma bali ni kujipendekeza tuu. Si unajua jamaa hana vidole?? Labda ana tafuta kiki ya kuruhusiwa kurudi India. Ila Mungu yupo
 
Si rahisi Mkuu, huyo jamaa ana remote control ya hao vikaragosi vyake. Kama hajawatuma kwanini asitie neno?

Unaweza kukuta Namba Moja hajawatuma bali ni kujipendekeza tuu. Si unajua jamaa hana vidole?? Labda ana tafuta kiki ya kuruhusiwa kurudi India. Ila Mungu yupo
 
Niajabu kama uchaguzi utafanyika wakati muda uliobaki ni sawa na muda aliokuwa nao hospitali na hakuna kilichofanyika. Sijui huyo anayekuja atafanya nini ndani ya mwaka mmoja. Muda mwingine naona bunge kuingiliwa ni sawa maana mambo kama haya yanaumiza. Hakuna namna sababu tulio chagua ndyo tulio panga!
 
Jamaa ametokea kuwa mwandishi mzuri sana aliyeweka mbele maslahi makubwa ya nchi yetu ukilinganisha na waandishi UCHWARA ambao wameweka umahiri wao pembeni na kuamua kuwa vikaragosi vya nduli na dikteta wa Ikulu ili kusaka teuzi waweze kujaza matumbo yao kama yule nanihii wa JamiiForums.

Huyo nanihii ni Pascal Mayalla, kwa mtazamo wangu. Lakini mbona yeye siyo mahiri? Utakuwa unamaanisha mtu mwingine. Mzee Mwanakijiji? Let me keep loading...
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom